Gwajima: Kutakuwa na Ugeni wa mzee kutoka kijiji cha KOROMIJE

Gwajima: Kutakuwa na Ugeni wa mzee kutoka kijiji cha KOROMIJE

AUDIO !! GWAJIMA: NINA VYETI VYA MAKONDA VYA JINA LAKE LA DAUDI BATISHE NA ALIFELI HILO MAKONDA NI LA VYETIVYETI

Tukisema huyu jamaa ni mwizi ameiba vyeti vya MTU tutakuwa tunamsingizia?

Tukisema huyu jamaa ni jambazi amebomoa nyumba ya Makonda tutakuwa tunamsingizia?

Tukisema huyu jamaa ni mwongo tutakuwa tunamsingizia?

Alipataje vyeti vya MTU mwingine? Kwa njia gani ? Kwa lengo gani? Lini? Alipewa na nani?alipewa wapi?

Naomba mnisaidie kujibu maswali hapo juu!!! Roho yangu isuzike!!! Kama ana vyeti vya Makonda naomba uplaod hapa tuvione!!! Tafadhali
kwa nn watu wanatumia nguvu nyingi sana kumchafua makonda kama hawana madawa kweli?kama amesema una madawa na huna si basi?
 
Sijui nchi ina laana gani? Hivi mtu mzima unawezaje kua na mawazo finyu kiasi hiki?? Utashangaa sana kusikia hata huyu mleta UZI nae ana digree walau moja. Hivi wakati mnatafuta kazi baada ya kutoka shule hua hamtawanyi vyeti vyenu kwa watu tofauti? Mbona mi nina CV na vyeti vya watu wengi tu wanaotafuta kazi? Mi siwezi shangaa kwa askofu Gwajima kua na vyeti si tu vya mkuu wa mkoa bali hata kama atakua na vya mtu mwingine; kwa maneno yake Gwajima, RC na askofu wanatoka kijij kimoja so cha ajabu ni nini hapo?
 
Wewe ndo hujui kabisa!!! Inawezekanaje akawa na original na feki za mh Makonda? Lini Makonda alitafuta kazi kwa Gwajima,??ningekuwa Mimi ningesweka ndani mpaka aseme alivipataje vyeti vya Makonda
 
kwa nn watu wanatumia nguvu nyingi sana kumchafua makonda kama hawana madawa kweli?kama amesema una madawa na huna si basi?
Jibu rahisi kwa suali lako ni kuwa Bashite ndie alieanza kuwachafua wenzake,angelifuata sheria haya yasingelimkuta,huwezi kuwatangaza watu kuwa ni wauza unga kwenye vyombo vya habari ukiwa huna uhakika

Serikali sio kama maskani ya kutuma salamu kwenye radio,sio kila kitu kipelekwe kwenye waadishi wa habari,Kweli huyu Bashite anajua ni maafa gani kawapa wenzake.

"Chuki zinazaa chuki","aliekuja kwa upanga ataondoka kwa upanga",hiii ni misemo ya kiswahili inabidi uifahamu
 
Vyeti Kumng`oa Rc Makonda? - Udaku Special Blog

Wakati Gwajima akidai kuwa na nakala za vyeti vyote viwili vya Paul Makonda, vikiwemo vile alivyotumia kuanzia kidato cha nne, upo mkanganyiko mkubwa kutokana na maelezo ya Paul Christian (mtu aliyedaiwa kumpa vyeti Makonda) aliyoyatoa kwa gazeti moja la kila siku la hapa nchini.

Paul Christian, anayedaiwa kuwa ndiye ambaye cheti chake kilitumiwa na Paul Makonda aliliambia gazeti hilo;

“Paul Makonda nimemfahamu kupitia habari na jina wanavyolitaja (waliotunga taarifa ya mtandaoni) wanakosea kwani mimi naitwa Paul Pierre Christian Kagezi, hatuna uhusiano, mimi Mhaya yeye Msukuma.”

“Taarifa hizo (za kumpa cheti Makonda) si za kweli kwa sababu huwezi kutoa cheti wakati umepata daraja la kwanza kidato cha sita, utakwenda vipi chuo kikuu? Sasa niliwezaje mimi kwenda chuo kikuu halafu kwa wakati huo nimpe naye aende chuo kikuu?”Alihoji.

Cristian aliendelea kudai kuwa katika kidato cha tano na sita, alichukua mchepuo wa sayansi masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), hivyo si rahisi kutoa cheti hicho kwani angeshindwa kumudu huko alikokwenda.

Alihoji kama Makonda hakufanya vema kidato cha nne au hakusoma kidato cha sita, akatumia cheti cha mtu mwingine, angeweza vipi kufanya vema katika mitihani yake ya chuo kikuu?

Alifafanua kuwa watu wamekuwa wakipika na kuoanisha majina yao, huku akiendelea kukanusha kuhusu taarifa hizo.

“Kama wanataka kumpata huyo bwanamdogo (Makonda) kwa njia hiyo wamemkosa, kwani kwa mantiki nimekuuliza ukipata daraja la kwanza kidato cha sita lazima uende chuo kikuu?” alihoji.

“Huyo bwana anajitegemea yeye kama yeye na walichokifanya wao (waliosambaza taarifa mtandaoni) kwa makusudi yao bila shaka wana lengo lao, wao wametaka kuingiza hoja ambazo hazina mshiko
 
Gwajima umepotoka :Acha kuchanganya ya KAISARI na Mungu.Mchungaji Gwajima umepotoka na unawaangamuza watu wa Mungu.Unakwenda kanisani unaanza kuhubiri mambo ya KAISARI.Biblia takatifu inasema ya KAISARI mwachie KAISARI.Leo wewe unachanganya ya KAISARI na ya Mungu.Je, umeshindwa kuilewa biblia inayotuongoza wakristo.?Watu wangu wanaangamia kwa kukosa ufahamu wa neno lako.
 
Kumaliza fitna vyeti vitolewe tu hadhani. Simpo
Mchungaji Ana result slip mbona kwenye ile audio yake mwisho ni aliconclude kwakusema. Uzuri siku hizi ukiingia kwenye mtandao naukiwa unahitaji Matokeo ya mtu ni sekunde tuu, mbona hsmtaki kujishughulisha,? Embu ingia kwenye mtandao wa necta ila uweunajua shule Bashite aliyosoma au namba ya hiyo shule na mwaka aliomaliza mbona ni sekunde tuu hata wewe utayaona hayo Matokeo ya division faafaa naukitaka kuyaprint unayaprinti tuu, hii ni simple case nandio maana huyo Bashite wenu domo limekua zito
 
Hakuna cheti kwa mtu aliyepata Zero, Gwajima anapiga porojo tu na kuna baadhi ya nyumbu wa Mbowe wanaitikia nyimbo yake.
 
Gwajima umepotoka :Acha kuchanganya ya KAISARI na Mungu.Mchungaji Gwajima umepotoka na unawaangamuza watu wa Mungu.Unakwenda kanisani unaanza kuhubiri mambo ya KAISARI.Biblia takatifu inasema ya KAISARI mwachie KAISARI.Leo wewe unachanganya ya KAISARI na ya Mungu.Je, umeshindwa kuilewa biblia inayotuongoza wakristo.?Watu wangu wanaangamia kwa kukosa ufahamu wa neno lako.
Kama yeye amekosea,,,, atahukumiwa kwa dhambi zake,,,,,
Mwenye kuhukumu ni Mungu mwenyewe
 
Umesahau kuna mtu alijinasibu akisimama yeye ni mungu amesimama????
Acha watumish wa MUNGU wamtofautishie kati ya MUNGU na mungu
 
Gwajima umepotoka :Acha kuchanganya ya KAISARI na Mungu.Mchungaji Gwajima umepotoka na unawaangamuza watu wa Mungu.Unakwenda kanisani unaanza kuhubiri mambo ya KAISARI.Biblia takatifu inasema ya KAISARI mwachie KAISARI.Leo wewe unachanganya ya KAISARI na ya Mungu.Je, umeshindwa kuilewa biblia inayotuongoza wakristo.?Watu wangu wanaangamia kwa kukosa ufahamu wa neno lako.
Huyo Kaisali anashambulia nyumba ya Mungu na watumishi wake, hata Yesu hakukubali nyumba ya Baba yake kugeuzwa pango la walanguzi, ALIPIGANA.
 
Mchungaji Ana result slip mbona kwenye ile audio yake mwisho ni aliconclude kwakusema. Uzuri siku hizi ukiingia kwenye mtandao naukiwa unahitaji Matokeo ya mtu ni sekunde tuu, mbona hsmtaki kujishughulisha,? Embu ingia kwenye mtandao wa necta ila uweunajua shule Bashite aliyosoma au namba ya hiyo shule na mwaka aliomaliza mbona ni sekunde tuu hata wewe utayaona hayo Matokeo ya division faafaa naukitaka kuyaprint unayaprinti tuu, hii ni simple case nandio maana huyo Bashite wenu domo limekua zito
Matokeo ya kwenye mtandao ndio result slip ? Makonda amemaliza form 4 early 2000s, je matokeo yalikuwa yanawekwa kwenye mtandao muda huo? Ingia na wewe kwenye mtandao basi utuletee hayo matokeo.
 
Dunia ya sasa ya kaisari na mungu yanaenda sambamba mwacheni Gwajima aseme na familia yake kuhusu yaliyojiri kijijini Koromije miaka kadhaa iliyopita.
 
Roho yako isuuzike??? Au na ww unafanya jitihada za kumsafisha?? Kama kweli makonda hajanunua vyeti si atoe vyeti vyake tuu tumalize utata maana hili swala linafanya vyombo vya habar kila siku vinaacha kutoa habar za msingi vinatoa habari za bashite
 
Back
Top Bottom