Gwajima, Polepole na Silaa waitwa Kamati ya Maadili ya CCM

Gwajima, Polepole na Silaa waitwa Kamati ya Maadili ya CCM

Dodoma. Wabunge watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwamo Mbunge wa Kuteuliwa, Humpherey Polepole watawekwa kikaangoni leo na Kamati ya Maadili ya Wabunge wa CCM kuhojiwa kuhusu masuala tofauti.

Wabunge wengine watakaohojiwa leo ni Askofu Josephat Gwajima (Kawe) na Jerry Silaa (Ukonga) ambao Bunge lilipitisha azimio la kuwasimamisha kwa mikutano miwili kutokana na tuhuma za kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Vilevile, Kamati imependekeza Askofu Gwajima kufikishwa mbele ya kamati ya chama chake CCM na kuhojiwa kuhusu mwenendo wake.

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilipendekeza Silaa asimamishwe mikutano miwili ya Bunge la Tanzania na avuliwe uwakilishi kwenye Bunge la Afrika (PAP) kwa madai kuwa anaweza kusema uongo akienda huko.

Kilichomponza Silaa ni kauli yake ya kutaka wabunge wakatwe kodi kwenye mapato yao, jambo lililoelezwa kuwa ni uongo, kwani wabunge wanalipa kodi.

Kwa upande wa Gwajima, atatakiwa kujieleza kuhusu kauli anazozitoa katika Kanisa lake la Ufufuo na Uzima kuanzia Julai 25 mpaka Agosti 15 kuhusu chanjo ya korona.

Chanzo Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi Ina maana Jerry Slaa hawezi kusoma salary slip yake? Nauliza tu Jaman!
 
#2

Imani ya pili ya CCM....

"Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake"

✓Unaanzaje kuwa na HESHIMA kwa wengine ilihali UNAJITENGENEZEA HISIA ZISIZO NA USHAHIDI kuwa sisi wananchi TUNAOHIMIZANA CHANJO tumefuata mkumbo wa viongozi "WALIONUNULIWA" na MABEBERU......

✓Unaanzaje kuwa na HESHIMA kwa wengine ilihali UNAWAOMBEA LAANA YA KIFO madaktari wetu wanaotuhimiza chanjo ya UVIKO?!!!


#SiempreCCM
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
 
CCM ina taratibu zake....

Ni mwiko kumpinga MWENYEKITI WETU hadharani kwa njia za kumshambulia ,kedi na kebehi.....

#SiempreCCM
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#KaziIendelee
Mimi ni sisiem, na mwenyekiti hapingwi popote, iwe hadharani au kikaoni
Hakuna demokrasia hio ya kutofautiana na mwenyekiti
 
Anawananchi
Gwajima aende na clip ya jana Kawe akiwa na Samia, awaambie wananchi wake ndiyo wamemtuma........

Slaa aende na clip ya Bashe ambayo ipo kwenye hansadi za Bunge......

Pole pole aende na V8 ataeleweka
Ana wananchi gani?
Ungesema kondoo wa kanisani kwake,
Alipitishwa na mwendazake.
 
Yes.

Askofu Gwajima ana watu wasiozidi hata elfu 1 - wale waumini kanisani kwake (akiwemo johnthebatist)!

Pole pole ana watu wasiozidi hata 10 (mfano Musiba, johnthebaptist, Bashiru, Bashite, Mjalalani na wengineo wa aina hii)

Jerry Slaa ana Hoja, tena ni hoja nzito na yenye mashiko!
Ni ujinga kufikiri watu wa Gwaji ni wale wa kabisa lake
 
Unapopinga hoja za KISAYANSI basi uwe umefanya TAFITI za KISAYANSI.....

Kinyume chake ,hawa wapingao chanjo wanakuja na yafuatayo:-

1)Hoja za kiimani

2)Hoja za "kujishuku" kupitia "conspiracy theories"

3)Hoja za ndoto na ramli chonganishi

4)"Mbango" tu za kuwapinga "wasiowapenda ,wasiowaheshimu na kutotaka kuwatii"


#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#SiempreCCM
Uteuzi unakuhusu ndugu, au tayari umeteuliwa!
Sayansi bado haijathibitisha weledi wa chanjo ya kovid
Anayeshadidia ni labda anataka uteuzi, au Safari za nje au hofu ya korona
Mama mwenyewe ameleta chanjo kwa ajili ya diplomasia na si kuondoa janga la korona Tz, maana hatuna janga tuna maradhi ya covid Kama maradhi mengine
 
Wote watavuliwa uanachama CCM,pigia msitali utakuja nikumbuka.
Hawatavuliwa uanachama, wanangoja uchaguzi wawanyime ubunge, ccm hatutakagi mawazo mbadala, sote tunatakiwa tuseme ndiiooo kwa viongozi wetu
 
Watuhumiwa wamekiuka Katiba ya chama Chao kwa kiwango Cha juu, ni vema wakachutama Kama bado Wana mahaba na chama Chao, vinginevyo naona wanapewa talaka tatu,siyo wenzao.
 
Unasema chanjo zimetengenezwa na WABAYA wasiotupenda waafrika(conspiracy theories) halafu uko katika MFUMO WA BUNGE ambalo haohao ndio WALIOLIASISI na kulieneza duniani kote.....

Huku ni kukosa HOJA KUNTU
Huku ni kujiongezea UMAARUFU "KOKO"

Chambilecho mbunge mh."King" ,WACHAMBA WIMA".......

#SiempreCCM
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
Huo mfumo hawajaueneza, Bali tumeiga
Hoja ya usalama wa miili yetu dhidi ya chanjo ni hoja kuntu
Wameasisi haki za mashoga, vipi tufuate kwakuwa tunafuata Mambo yao mengine?
 
Back
Top Bottom