Gwajima, Polepole na Silaa waitwa Kamati ya Maadili ya CCM

Kila mtu anastahili heshima, Ila ukweli hauvunji heshima, Kama kweli wamenunuliwa huo unabaki ukweli na aliyenunuliwa ndie amevunja heshima yake
 

Yes, wahojiwe. Wameyataka wenyewe
 
CCM ya sasa ni ya wajinga,haina meno.Wanaigiza tu
 
Huo mfumo hawajaueneza, Bali tumeiga
Hoja ya usalama wa miili yetu dhidi ya chanjo ni hoja kuntu
Wameasisi haki za mashoga, vipi tufuate kwakuwa tunafuata Mambo yao mengine?
Haki za mashoga si matibabu Wala tiba....

Basi kataeni na MATIBABU YA HOSPITALI na mjikite kwenye tiba za asili na ramli.....
 
Mbunge anahamasisha wabunge nao walipe kodi anaitwa kwenye kamati ya maadili Nchi hii ina Wazalendo wachache mno...
 
Sekretari ya Ccm sasa inaongozwa na vikaragosi hata havijielewi. Polepole wanamhoji nini kama sio kujipendekeza kijinga. Kuna watu wako kwenye uongozi wa juu ccm wala hata hawakielewi chama. Hawaelewi itikadi ya ccm na wala hawajui kwa uhakika ccm inasimamia nini. Na wala hata huyo mama samia hawamuelewi.
 
Hamna kitu hapa.
Kuna hoja Ccm na serikali yake wana kwepesha.
Ccm huzima hoja kwa matukio.
 
Karma is real.
Leo polepole anahojiwa.
Bado bashiru aliyemhoji Makamba na Kinana kwa dharau sana. Hakujua Makamba Ni mzee wa Mahezanguu.
 
Safi Sana maana hukumu ya Gwajima ilifanyika pale Kawe rais aliposimama kuwasalimia wananchi.

Gwajima Oyee ilikuwa na maana.

Moja kuupima upepo au mtazamo wa wananchi au wapiga Kura wa Gwajima,baada ya kutofautiana na mwenyekiti wake juu ya chanjo.

Mambo yaliyotazamiwa na rais,Kama Gwajima angezomewa ilikuwa kuonyesha wananchi wamechukizwa na kitendo chake Cha kumpinga rais.
Kama atashangiliwa Ina maana wananchi wanamuunga mkono Gwajima.
Ndiyo maana aliposema Gwajima Oyee kelele zikawa nyingi,rais akasoma upepo akaangukia kwa Gwajima kiana kwa kusema Gwajiboy oyee,kelele zikazidi zaidi.

Akajua Gwajima Ana watu kwa hiyo kumfukuza ni kutengeneza tatizo zaidi nafuu kumkemea kwenye chama.

Pili rais alitaka kuupima upepo Kama wananchi wanataka chanjo,jibu la watu wengi hatuchanjwi lilimaliza nguvu ya Vita juu ya Gwajima.

Kwa hivyo wakiamua kwa kudemuka huu ndo mtaji wa CHADEMA,ndiyo maana kelele za afukuzwe nyingi si za wanna CCM ni za wapinzani,ukiondoa wanazi wachache wa CCM.
 
Wote watavuliwa uanachama CCM,pigia msitali utakuja nikumbuka.


Itasaidia nini ?

Itasaidia kufufua sera ya viwanda au ?

Mambo mengine bora wangekuwa wanafanya kupita Mbona bunge limeshawaazibu?

Adhabu zinatolewa mara ngapi?

Shughukieni kutatua matatizo yanayowakabili waTZ ni mengi sana ikiwemo wanafunzi wa kukosa mabweni, zahanati kuwa mbali na makazi ya wengi , n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…