Gwajima: Siwezi kujitetea kwa mahubiri yanayotoka kwa Roho Mtakatifu

Huwezi kuyafanya mahubiri ya kanisani kama kichaka cha upotoshaji na wakati mhubiri mwenyewe wakati fulani ndiye pia alikuwa muumini wa kauli hii inayotumiwa mara nyingi na wanasiasa hata out of context: 'Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu' (Warumi 13:1). Waumini wengine ni askofu Gamanywa, Kakobe, Mzee wa Upako etc.
Huyo mungu anayeabudiwa bila shaka ndo huyo anataka tuchanje hakuna jingine..mimi simuabudu huyo mungu hivyo sichanji
 
Kwa hiyo Bunge lina mamlaka ya kusikiliza jinai? Shiiit!
Huku msikia spika alisema wao wata shuhulika na la kibunge na kwa jinai vyombo husika vichukue mkondo wake. Acheni siasa na huyo con man, kwenye dunia ya kistaarabu sio watu wa kuwa vumilia.
 
"Niliitwa na Kamati ya Maadili ya Bunge wiki iliyopita nilipotoka wengi mliniuliza kimejiri nini na nikasema sitosema hadi Kamati iseme kwanza na kwasababu Kamati imeshaongea acha nami nizungumze”

“Sababu ya kuongea ni kwasababu wameniongelea kama Mtu mbaya sana, Jitu baya sana ambalo kama lipo kama lilivyotajwa basi halitakiwi hata kuwa Kiongozi wa Kanisa”

“Mimi Mchungaji wa muda mrefu sana hapa tu Ubungo nipo kwa miaka 25, nilipoitwa kwenye Kamati yale niliyoitiwa ni kuhusu mahubiri ya Kanisani, Mimi nikawaambia sidhani kama Kamati mmefanya vizuri maana yote nimeongea Kanisani na hakuna mwenye Mamlaka ya kuuliza maswali juu ya Ibada ya Kanisani na imani za Watu na nikasema kwenye hili Kamati mmekosea”

“Niliwaambia Kamati mmesema mmesikia nimewaambia Watu wasichanjwe nikasema hiyo haibadiliki milele, nikaweka wazi kwamba sisi Ufufuo na Uzima chanjo ni hiari na sisi tumechagua hatuchanji sikupindisha nilisema hatutowaruhusu Waumini kuchanja na sababu zetu ni hatujapata taarifa za kutosha juu ya madhara ya chanjo ya muda mfupi, siku zijazo na siku nyingi”

“Kwahiyo kama nimeitwa mkorofi ukorofi wangu ni huo na kama huo ndio ukorofi basi ni ukorofi kwelikweli kwenye eneo hilo, wakaniambia jitetee nikasema sina la kujitetea, siwezi kujitetea kwa mahubiri niliyohubiri yanatoka kwa roho mtakatifu, nimefafanua ili mjue Gwajima sio mkorofi ”———-Askofu Gwajima

My Take
Bunge hapa lilichemka. Labda lingempiga pini kwenye chama

Mana II was uongo
 
Huwezi kuyafanya mahubiri ya kanisani kama kichaka cha upotoshaji na wakati mhubiri mwenyewe wakati fulani ndiye pia alikuwa muumini wa kauli hii inayotumiwa mara nyingi na wanasiasa hata out of context: 'Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu' (Warumi 13:1). Waumini wengine ni askofu Gamanywa, Kakobe, Mzee wa Upako etc.
Ana bahati sana kamkuta huyu ni Mama kaumbwa na msamaha kaumbwa na roho fulani ya kiungwana yenye msamaha. Kama angekutana na wababe wa afrika kina Paul Kagame au John Magufuli muda huu angekuwa keshang'olewa meno yote na anakunywa supu kavu ya pili pili kwa lazima.

Wakati mwingine tumshukuru sana Mungu anajua kuleta uwiano hata pale ambapo kwa macho ya kibinadamu unaonekana kutowezekana kuwepo.
 
Huwezi kuyafanya mahubiri ya kanisani kama kichaka cha upotoshaji na wakati mhubiri mwenyewe wakati fulani ndiye pia alikuwa muumini wa kauli hii inayotumiwa mara nyingi na wanasiasa hata out of context: 'Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu' (Warumi 13:1). Waumini wengine ni askofu Gamanywa, Kakobe, Mzee wa Upako etc.
Hata kiongozi wa serikali [iliyo na mamlaka] anaweza kutoka huko alikolala na mkewe au mumewe na kutoa amri kuwa;

"kuanzia kesho mimi Rais nasema, watu ruksa kulawitiana"

Je, kwa sababu hii ni kauli iliyotoka kwa kiongozi wa serikali "yenye mamlaka, iliyowekwa na mungu" basi watu watii tu, au siyo..?

Kama hii ndiyo maana yako, basi kumbe Mungu alikuumba na kukupa akili za bure tu badala ya kuzitumia kwa kazi ya kutambua JEMA na BAYA....!

Honestly, mimi naweza Kuku - describe kwa namna hii, kuwa, wewe ni "mjinga wa kiroho". Hujui usemalo. Huyajui maandiko. Nakushauri acha kupotosha watu kwa hili...!!

Ni wazi kuwa hujui. Kuwa, kwa taarifa yako ziko mamlaka zingine na zinaongoza serikali za kidunia, wala hazijatoka wala kuwekwa na Mungu Yehova. Zimejiweka zenyewe au kuwekwa na kale "kamungu" kengine na zinatumia maandiko haya haya kuongoza kipotoshaji na watu kwa ujinga wao wanakubali....

Ama kweli watu wa Mungu tunaangamizwa kwa kukosa maarifa ya kuyatambua na kuelewa maandiko ya Mungu....

Be carefully usije Julia na kujuta baadaye!
 
Sijakuelewa unasema nini: unanikosoa mimi kukosoa wanaotumia vibaya vifungu vya biblia au mahubiri kupotosha waumini au unawakosoa hao wanaotumia hivyo vifungu vibaya?
 
KWANZA; ungetoa basi hata "like" kwa comment yangu kwako. Hiyo ndiyo nidhamu ya mjadala hata kama hoja imelenga kukukosoa wewe...

PILI; kuhusu swali lako. Sijui ni kwanini hujaelewa maana nimetumia "nafsi ya pili" (second person) ikiwa na maana nimekulenga wewe...

Kwa mfano hata niliposema "huyajui maandiko wewe" kwanini usitambue kuwa I am referring you..?

Kwa hiyo, the straight forward simple answer for your question is: yes, all of my writings was about you...!!
 
Siwezi ku'like' jambo ambalo sijalielewa.
 
Back
Top Bottom