Gwajima: Taifa tumekosa maono, inakuwaje kujenga reli kabla ya kuchimba chuma? Waziri Mwigulu ampinga

Kiwanda cha chuma ni muundo mbinu kama barabara, bandari nk. Huwezi kukiwekea mambo ya break even kirahisi.
 
ni lini ccm wakawa na maono ndio maana wakamuua mpaka Nyerere ili waweze kumuingiza mtu wao 2005
 
Kwa hivyo Gwajima anakubali Magufuli alikosa maono?

CCM unadhanj kuna watu inategemea wameamkaje siku hiyo hata kuwaamini tu ni kosa angekuepo jiwe asingetoa hiyo hoja, halafu hiyo hoja alishaisema zitto zamani sana
 
Kama chuma kinapatikana, uzalishaji unaanza halafu kwenye tenda kunawekwa kipengele cha kutumia chuma kutoka ndani ya nchi.
Kwa maneno mengine gharama inapungua, pia biashara na ajira vinaongezeka.
 
I hope you are just being sarcastic. I really do.

Amandla...
 
Kama chuma kinapatikana, uzalishaji unaanza halafu kwenye tenda kunawekwa kipengele cha kutumia chuma kutoka ndani ya nchi.
Kwa maneno mengine gharama inapungua, pia biashara na ajira vinaongezeka.
Naona kama kuna watu wanaamini kuwa chuma kinapochimbwa kinakuwa tayari kupelekwa site ili kitumike tunavyopenda.

Amandla...
 
Kipindi siku za nyuma Bw Zitto alizungumzia kuchimba Chuma kabla ya kuanza ujenzi wa reli!
 
Kama chuma kinapatikana, uzalishaji unaanza halafu kwenye tenda kunawekwa kipengele cha kutumia chuma kutoka ndani ya nchi.
Kwa maneno mengine gharama inapungua, pia biashara na ajira vinaongezeka.
Haya mawazo aliyatoa Ayatolla Zitto ila màgufool alimpuuza
 
Hii issue zito aliliongea sana tu sema ila ilikuwa ngumu sana kusurvive
 
Aliwaambia wananchi wake kuwa atajenga treni na pesa anayo😂😂
 
Nadhani wewe ndio ujaelewa hoja yake. Ni hivi Gwajima anashangaa kwanini tumeanza kujenga reli kabla ya kuvuna chuma ili reli tunayojenga vyuma vyake vitoke hapa hapa nchini badala ya kuagiza nje.

Ni kweli nchi nyingi zimejenga reli na hazina madini ya chuma ila sisi tunayo. Kwanini mradi wa reli usingesubiri uvunaji wa chuma ili chuma chetu kiwe na soko la uhakika?

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kiwanda cha chuma ni muundo mbinu kama barabara, bandari nk. Huwezi kukiwekea mambo ya break even kirahisi.
Kila kitu hapo ni investment inategemea unakiona ni merit good au business venture.

Muhimu nani anajenga ingekuwa barabara zinajengwa na watu binafsi kupita kungekuwa na toll charges, mchina akijenga bandari anataka return and so forth.

Tukiachana na hayo ata ukitafuta mwekezaji ajenge kiwanda cha chuma kwa hali ya umeme wa Tanzania atakwambia kwanza lazima ajenge na mitambo ya kuzalishia umeme wake.

Dangote tu ameweka umeme wake, hiyo ni saruji tu ili aweze fikisha production goals, sasa umeme unaotakiwa kwenye kiwanda cha heavy metal I ndustry tunaujua kweli au tunasikia tu.

Na break even kwenye kiwanda cha heavy metal is necessary ata kama huna lengo la kupata faida lakini uwezi kuzalisha kwa gharama zaidi kuliko unavyouza; vinginevyo utakuwa unatoa ruzuku kila mwaka ili kiwanda kiwepo tu; if you must know hizo ndio sababu asilimia kubwa viwanda vya chuma nchi nyingi vimekufa hasa za ulaya bora waagize China ambao wanatengeneza ata cheap (sasa usije jifananisha nao their economies of scale kwenye hiyo industry is at another level).

Ni hivi jengeni kama rahisi halafu muone kama mtaweza ata kuuza chuma Kenya au Rwanda kwa kushindana na bei za China.

Sisemi kwamba aiwezekani kabisa Tanzania kuwa na kiwanda cha chuma ila hatuna hizo resources, uchumi wa ku support hiko kiwanda na wala uwezo wa kushindana na China ata kuuza kwa nchi jirani tu let alone duniani.

Ni hivi hayo mambo sio rahisi kama mnavyoyaongea ukianza kukata namba zinazohitajika ili ufanikiwe ni mziki mnene.
 
Gwajima hayo maneno ungeyasema wakati ndugu yako aliyekupa ubunge yupo, ungevuliwa ubunge, angepewa Mdee
 
Duh

Ova
 
Aliwaambia wananchi wake kuwa atajenga treni na pesa anayo[emoji23][emoji23]

Alisema tutapelekwa japan kujifunza uvuvi na meli za uvuvi atatuletea pesa anayo, wengine tukaelezwa tutapelekwa marekani hadi leo kimya
 
Pia, busara ungetumika kuaanzisha bwawa kabla ya kugharimu project ya SGR? its like putting a cart before the horse???
 
China anatoa ores Australia kwa meli. Azikifua na kusafirisha steel duniani kote kuuza. Sisi huko liganga kinachimbwa na makaa yapo hukohuko ya kufulia. Gharama za uwekezaji mwanzo zitakuwa kubwa, pengine investors wataona siyo biashara. Kama ambavyo wanaona kujenga kitu kama barabara ni biashara kichaa. Lakini kikianza kuzalisha kina faida lukuki kwenye uchumi, kama barabara tu. Si lazima wauze bei pungufu, wanaweza uza bei inayoweza endesha kiwanda. Inaweza kuwa ya soko au chini.

Na usizungumzie Ulaya na Marekani. Gharama za uzalishaji huko, hasa za wafanyakazi na mazingira ni kubwa sana, ndiyo maana wanaagiza chuma. Si kwamba hawajui umuhimu wa kukizalisha. Utajiri na maendeleo yao leo yametokana na chuma.

Na si mpaka kuuza nje, tukijitosheleza wenyewe kwa nondo, vyuma vya mashine, reli, boats nk nk inatosha.

Nchi zote zilizotaka kujitosheleza kwa chuma ziliambiwa haziwezi na nyingine kunyimwa teknolojia. Hii ipo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…