ndugu yangu, wakubwa waliingilia kati pamoja na familia wakawa hawataki iyo itokee, lakini kama wasingefanya ivyo, amina chifupa angerudi laivu, ..waliogopa mvurugano utatokea huko kwa wakubwa kwasababu kuna siri nyingi sana kwenye hiyo selikali yenu. hivyo ilibidi waombe jamaa asimrudishe..
umekichukia king'ora? au umemchukia alibebwa na ham'ma?
sijaona tatizo, ukiona hivyo si lazima uruhusiwe na mtu
kiongozi wa kiroho ni mkubwa kuliko, kiongozi wa kundi la wezi
hata ana kofia ya kuwa raisi, any way hii ni nchi yetu na wananchi ndiyo sisi,
hata mimi hakuna kitu kinachoniudhi kama makelele ya adhana
Kiongozi wa kiroho naye ni mwizi tu.
Kwanza hiyo roho iko wapi? Inakaa wapi katika mwili wa binadamu? Huyo mungu mwenyewe yuko wapi?
Uongo mtupu. Bora hata hao viongozi wa kisiasa wanadanganya kuhusu dunia hii, hao "viongozi wa kiroho" ndio majambazi wakubwa kwani wanadanganya watu kuhusu mbingu ambayo hamna mtu aliyefika.
Wewe unamdharau Askofu, eee! Unadhani ni mtu mdogo? Uliza wazee wako nao watakuambia. Acha apigiwe ving'ora bwana. Kwani nani mwenye hakimiliki ya hivyo vitu?
pa mfaranyaki" lugha gani hiyo ngohswe?
Niko Old Bagamoyo road nasikia ving'ora vinapigwa kutoka kwenye gari inabidi kuweka gari pembeni nikihisi ni Mheshimiwa au mgonjwa anapita nashangaa kuona Hummer nyekundu na msururu wa magari ukipita kwa kasi na hayo magari yamebandikwa Picha ya mheshimiwa askofu anakaribishwa nyumbani.
Sijui huyu bwana karuhusiwa na nani kwa kutupigia ving'ora na kupita kwa kasi kama kiongozi wa nchi. Sasa hata matapeli wanajidai hii nchi sijui tunaenda wapi?
Nkumbuka mwaka fulani 2003 au 4 niliwahi kuona msafara wa kiongozi fulani wa kihindi jina limehifadhiwa nae alipigiwa ving'ora kama huyu!
najaribu kuilazimisha akili ielewe hiki kitu bado ngumumagazeti ya Shingono
mimi ndugu zangu nashangaa kumuona Kiongozi wa Kanisa kuwa na Hummer nyekundu? Wakati Bwana Yesu Kristo alikuwa napanda Punda!!! Kweli tutakwenda Peponi jamani? Pesa za hiyo Hummer nyekundu Askofu huyu amezipata wapi?kama sio Michango ya Waumini? kazi kweli ipo. Bwana Yesu Kisto alisema (Tajiri hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu mpako hapo Ngamia aweze kuingia katika Tundu ya sindano) Viongozi kama hawa Wenye Ma Hummer nyekundu mimi kwa binafsi yangu siwaamini hata kidogo bora Uswali uwe nyumbani kwako kuliko uende kuibiwa pesa na Maaskofu Matapeli wanaotumia Jina La Mungu na Bwana Yesu Kristo kuwaibia watu Pesa zao.
Kuna huyo Chris Oyakhilome rai wa Nigeria mwenye Kanisa la Christembassy tunang'anganizwa kununu vitabu vyake vya Rhapsody of Realities hapa ofisini kila mwezi na waumini wake. Huwa najiuliza kwanini asingekuwa anatengeneza nakala moja ya mwaka mzima badala ya kuwafanya waumini wake wawe wachuuzi kila mwezi. bei 2000/=, usiponunua unanuniwa weee na kuonekana unamkana Yesu.