The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Ukimsikiliza vizuri askofu uchwara wa kujipachika Josephat Gwajima, unashangaa. SIku hizi, amendandia hoja iliyotaka kumzamisha ya utekaji. Anasema hapendi utekaji kana kwamba kuna mtu mwenye akili zake anayeupenda ukiachi wauaji wetu .
Kinachoshangaza ni kusema eti serikali na vyombo vya usalama haviteki watu. Hii, inamaanisha Gwajima anawajua watekaji na wasio watekaji kama siyo kutaka kung'ata na kupuliza ili aendelee kuishi maisha yake ya ndumilakuwili.
Kama vyombo vya usalama na serikali hawahusiki na utekaji, nani anateka watu?
Kuna haja ya kumfichua Gwajima aache uchawa, unafiki, upopo, utapeli, na kutafuta kiki. You can't be both clean and dirty at the same time. Tafadhali, Gwajima, onyesha unaposimamia badala ya kutufanya wote mazwazwa kama wewe.
NAWASILISHA.