H. Baba msanii mwenye Jumba kali kuliko wote Tanzania

hahhahaha mi ndio siwezigi kumsifia mtu ili anione utaishia kumbwela mbwela ili akuone mwisho wa siku unarudia kumchukia. Kuwa real sifia kutoka koyoni
Anapambana na hali yake....
H-baba atakuwa anamkubari sana diamond
 
Hivi definition ya nyumba nzuri ni nn!?? Eti me huwa naona ni usingizi tu...!!! Maana hata ukijenga nyumba ya 10billioni,si utakuwa unaingia kulala tu sawa na mwenye nyumba ya tope yenye makuti,wote mnapitiwa na usingizi!!
 
Hongera yake, japo ni nyumba ya kawaida sana
 
Endelea kujipa moyo mkuu...
Kujipa moyo vp mkuu!!? Me nimeuliza,na hizo fikra ulizonazo ww ndo fikra za watanzania wengi. Me nakupa mfano,yule lugumi zile nyumba zake za thamani ya bilioni 1,zimemsaidia nn!?? Vp hiyo bilioni angejenga apartment!?? Kwa siku angekuwa na uwezo wa kuingiza si chini 5ml. Ambayo ni 15ml. Kwa mwezi na 180mil. Kwa mwaka. Yaani ukijenga nyumba ya kuishi kwa milioni 100. Na mwingine akajenga ya milioni 7. Tofauti yenu ni nini!?? Maana wote mnaingia kulala tu humo na wote mnapitiwa usingizi...!!!
 
Hivi definition ya nyumba nzuri ni nn!?? Eti me huwa naona ni usingizi tu...!!! Maana hata ukijenga nyumba ya 10billioni,si utakuwa unaingia kulala tu sawa na mwenye nyumba ya tope yenye makuti,wote mnapitiwa na usingizi!!
mawazo ya kimaskini hayo unajipongeza na fanta hapo ulipo
 
Hivi definition ya nyumba nzuri ni nn!?? Eti me huwa naona ni usingizi tu...!!! Maana hata ukijenga nyumba ya 10billioni,si utakuwa unaingia kulala tu sawa na mwenye nyumba ya tope yenye makuti,wote mnapitiwa na usingizi!!
Nakuelewaga sana mkuu
 
Kwa mtazamo wako wewe nyumba ni usingizi tu? Basi jenga banda tu ulale? Wenzio wanakazana kuhakikisha vitu vyote vinapatikana ndani ya majumba yao kuanzia movie theater, baa counter, indoor swimming pool, saloon ya nywele, uwanja wa basketball wa ndani, club ya dansi ya ndani, gym ya mazoezi, chumba cha pool table na table tenis, casino ndogo, chumba cha ofisi, sebule nne, vyumba vya self vitano, majiko mawili, lift ya ndani, chumba cha msikiti/kanisa, chumba cha jacuzzi na sauna, dining room tatu n.k ndani ya jengo moja wewe unawaza nyumba ni kitanda tuu.
 
Endelea kujipa moyo mkuu...
Hivi pesa unaitafuta kwa ajili gani? Iendelee kuzaana huku wewe ukiishi maisha ya tabu au ikuhudumie.
Ndiyo kuna tofauti kubwa ya anayelala kwenye nyumba ya milion 7 na anayelala kwenye nyumba ya milioni 200.
Nyumba ya milion 200, itakuwa na AC so joto halikutesi, itakuwa na heater za maji so waoga maji moto, itakuwa mpangilio mzuri ndani ukikaa hata nafsi yako inafurahi, itakuwa na vyumba vipana hewa ya kutosha ukilala walala usingizi usio na mashaka mashaka ya kung'atwa na wadudu, itakuwa na security systems vibaka wadokozi hawapiti ovyo ovyo.
Ni kujipa moyo kusema usingizi wa nyumba ya udongo na nyumba ya mls 200 unafanana.
Kuna usingizi na usingizi murua.
Hata vits ni gari ila anaye ride kwenye meredes benz ya mwaka 2017 anaenjoy zaidi japo zote zinawafikisha mwendako ila mwenzako anafika in a style.
Same applied to nyumba, kama una ela jenga mjumba bwana maana kazi ya pesa si kuzaana tu, itumie pia kuishi vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…