H-Pylori ni hatari sana. Kichwa kuuma kizunguzungu kama nataka kuanguka

Abdull hameed

Senior Member
Joined
Jan 29, 2025
Posts
126
Reaction score
230
Nimetimiza zile siku za kusubiria ili nikapime tena wakuu mdudu bado yupo ila hakuna kuumwa tumbo ni kichwa kuuma kizunguzungu kama nataka kuanguka, mwili kuchoka, kuhisi kama kuna kitu hapa kifuani upande wa kushoto aiseee huyu mdada atari mno..nimebadilishiwa dozi tena full madawa😭😭
 

Ukitekeleza hayo H. Pylori atajiondokea mwenyewe? Maana anamaanisha yupo kwa evidence ya vipimo
 

Pole Bro.

Hizo Dalili ndio ulikuwa nazo mwanzon kabla ya kwenda Hosp?
Uko Zanzibar?.
Ulipima kwa stool na ndio ukaambiwa ni Hpylori?.

kama ni ndio maswali yote hapo juu basi Badili hosp. 100% wamesoma kipimo vibaya.

Hata kama ni Hapana kwa maswal ya hapo juu . Kwa dalili hizo.
50% Sio huyo mdudu. Kwahiyo pia Badilisha hosp ukapime tena sehem nyingne kwa uhakika zaid.

Nina mashaka sana kama hiyo unayoumwa ni H pylori.
 
Vincenzo Jr njoo ushare experience na ushauri
 
siri yake ni ipi
 
huwa naamini sana kwenye kujaribu njia tofauti kama ulivyosema m,usizoe njia moja tu upo sahihi kabisa,abadili hospital ,abadili daktari ,abadili madawa ,abadili njia za matibabu,ukiona vyote vinagoma mtafute Mungu pia huponya magonjwa sugu
 
hivi visababishi virahishi vya h pylori ukiacha uchafuchafu ,hii mtu alienae akikushika mkono yu unaupata,mtaalamu mwenye kujuwa ajaribu kushare
 
Vincenzo Jr njoo ushare experience na ushauri
Kwanza nampa pole pili asikate tamaa hawa wadudu wanaisha endapo atafuata ushauri sahihi wa matibabu na wa maisha cha kwanza apunguze mawazo pili ale kwa wakati huku akipiga dozi aliyo pewa na dokta wake na apendelee sana kula maparachichi kulamba sana asali hapo atapata unafuu na anaweza kupona kabisa na asisahau kula bamia kila siku haya niliambiwa na daktari pale muhimbili na now nipo fresh hadi pombe natumia
 
jaribu chai yako ya asubuhi iwe na karafuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…