Ha ha haaaaaa ni Mulugo tena!

Ha ha haaaaaa ni Mulugo tena!

Status
Not open for further replies.
Mkuu.
Haya matokeo yame sahihishwa kikanda na matokeo hayo huwa hayawekwi kwenye tovuti ya Necta.

Nakushauri ufuatilia matokeo hayo kwa kanda husika.

Ubarikiwe mpaka upigwe na butwaa!
HAHAHA na mimi natamani kubarikiwa
 
Yule jamaa aliyekuja na muungano wa pemba na zimbambwe south Africa, leo amenifurahisha sana alipokuwa anatangaza matokeo ya kidato cha pili kwa mambo mawili<

1. Eti mikoa ya kanda ya ziwa ni Mwanza na Mara.
2. Ameshindwa kabisa kutamka neno Thaqaafa second. anatamka swafaka ee, swaaa, swaa................ hadi alipopata msaada wa waandishi wa habari jinsi ya kutamka neno hili.

Hapa sitaki tena na tena kuamini kwamba hii ni MISTAKE hii ni ERROR japo sina uhakika kama anajua tofauti ya maneno hayo.
we ndio kiraza mkuu kwani mara sio kanda ya ziwa???? hilo neno thaqaafa hata wewe ungekosea kwani ni mwarabu huyo hebu fanyeni vitu vya msingi bas au kama vipi muombeee baba yako apewe uwaziri na JK
 
MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA PILI, 2012


1.0UTANGULIZI
Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili ulifanyika nchini kote kuanzia tarehe 05/11/2012 na kumalizika tarehe 16/11/2012. Mwaka 2012 kulikuwa na jumla ya vituo 4,304 vilivyosajili watahiniwa, ikiwa ni ongezeko la vituo 117(2.79 %) ikilinganishwa na ile ya mwaka 2011.
2.0WATAHINIWA WALIOSAJILIWA, WALIOFANYA NA WASIOFANYA MTIHANI
2.1Idadi ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 430,327, kati yao wasichana walikuwa 205,476 na wavulana 224,851. Idadi hii ni upungufu wa watahiniwa 36,240 (7.76%) ikilinganishwa na mwaka 2011 ambapo walikuwa 466,567.
2.2Watahiniwa 386,271 sawa na asilimia 89.76 ya waliosajiliwa, walifanya mtihani wakiwemo wasichana 187,244 na wavulana 199,027.
2.3Watahiniwa 44,056 sawa na asilimia 10.24 hawakufanya mtihani, kati yao wasichana ni 18,231 na wavulana 25,825. Mwaka 2011 watahiniwa 47,527(10.19%) hawakufanya mtihani. Sababu za watahiniwa kutofanya mtihani ni pamoja na utoro, kuugua, kudaiwa ada, kufukuzwa shule, mimba na vifo.
3.0UFAULU WA WATAHINIWA
3.1Watahiniwa waliofaulu ni 249,325 (64.55 %) kati yao, wasichana ni 113,213 na wavulana 136,112. Kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 19.15 kutoka asilimia 45.40 mwaka 2011. Watahiniwa waliofaulu kwa kiwango cha A, B, na C walikuwa 127,981 (33.13%) na waliofaulu kwa kiwango cha D ni 121,344 (31.42%). Alama ya juu ya ufaulu ni 92%
3.2Wastani wa ufaulu kwa masomo ni 38%, wastani huu umepanda kwa asilimia 7 ukilinganishwa na mwaka 2011 ambapo ulikuwa 31%.
3.3Watahiniwa 136,923 (35.45 %) hawakufaulu mtihani, wakiwemo wasichana 74,020 na wavulana 62,903. Watahiniwa hawa watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013. Aidha, mwaka 2011 watahiniwa 228,759 (54.59%) hawakufaulu mtihani.
3.4Watahiniwa 23 matokeo yao yamefutwa kutokana na tuhuma za udanganyifu. Watahiniwa hawa wanatoka katika shule zifuatazo;
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]
Na
[/TD]
[TD="width: 156"]
Jina la Shule
[/TD]
[TD="width: 96"]
Kanda
[/TD]
[TD="width: 216"]
Idadi ya watahiniwa
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 49"]
1.
[/TD]
[TD="width: 156"] Kiyongwire[/TD]
[TD="width: 96"] Mashariki[/TD]
[TD="width: 216"]
2
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 49"]
2.
[/TD]
[TD="width: 156"] Nyashishi[/TD]
[TD="width: 96"] Ziwa [/TD]
[TD="width: 216"]
4
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 49"]
3.
[/TD]
[TD="width: 156"] Thaqaafar[/TD]
[TD="width: 96"] Ziwa [/TD]
[TD="width: 216"]
3
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 49"]
4.
[/TD]
[TD="width: 156"] Paroma[/TD]
[TD="width: 96"] Ziwa [/TD]
[TD="width: 216"]
2
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 49"]
5.
[/TD]
[TD="width: 156"] Murangi[/TD]
[TD="width: 96"] Ziwa [/TD]
[TD="width: 216"]
1
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 49"]
6.
[/TD]
[TD="width: 156"] Bukene[/TD]
[TD="width: 96"] Magharibi[/TD]
[TD="width: 216"]
7
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 49"]
7.
[/TD]
[TD="width: 156"] Kili[/TD]
[TD="width: 96"] Magharibi[/TD]
[TD="width: 216"]
1
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 49"]
8.
[/TD]
[TD="width: 156"] Binza[/TD]
[TD="width: 96"] Magharibi[/TD]
[TD="width: 216"]
1
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 49"]
9.
[/TD]
[TD="width: 156"] Kizumbi[/TD]
[TD="width: 96"] Magharibi[/TD]
[TD="width: 216"]
1
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 49"]
10.
[/TD]
[TD="width: 156"] Kolandoto[/TD]
[TD="width: 96"] Magharibi[/TD]
[TD="width: 216"]
1
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Watahiniwa hawa nao watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013.
4.0UFAULU KWA SHULE
4.1Shule Zilizoshika Nafasi Kumi za Mwanzo
4.1.1Shule za Serikali
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]
NA.
[/TD]
[TD="width: 204"]
SHULE
[/TD]
[TD="width: 216"]
KANDA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
1.
[/TD]
[TD="width: 204"] MZUMBE[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
2.
[/TD]
[TD="width: 204"] TABORA WAVULANA[/TD]
[TD="width: 216"] MAGHARIBI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
3.
[/TD]
[TD="width: 204"] ILBORU[/TD]
[TD="width: 216"] KASKAZINI MAGHARIBI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
4.
[/TD]
[TD="width: 204"] KIBAHA[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
5.
[/TD]
[TD="width: 204"] IYUNGA[/TD]
[TD="width: 216"] NYANDA ZA JUU[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
6.
[/TD]
[TD="width: 204"] MSALATO[/TD]
[TD="width: 216"] KATI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
7.
[/TD]
[TD="width: 204"] MALANGALI[/TD]
[TD="width: 216"] NYANDA ZA JUU KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
8.
[/TD]
[TD="width: 204"] IFUNDA UFUNDI[/TD]
[TD="width: 216"] NYANDA ZA JUU KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
9.
[/TD]
[TD="width: 204"] SAMORA MACHEL[/TD]
[TD="width: 216"] NYANDA ZA JUU[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
10.
[/TD]
[TD="width: 204"] KILAKALA[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
4.1.2Shule Zisizo za Serikali
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]
NA.
[/TD]
[TD="width: 204"]
SHULE
[/TD]
[TD="width: 216"]
KANDA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
1.
[/TD]
[TD="width: 204"] KAIZIREGE[/TD]
[TD="width: 216"] ZIWA MAGHARIBI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
2.
[/TD]
[TD="width: 204"] MARIAN WAVULANA[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
3.
[/TD]
[TD="width: 204"] ST. FRANCIS[/TD]
[TD="width: 216"] NYANDA ZA JUU[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
4.
[/TD]
[TD="width: 204"] DONBOSCO[/TD]
[TD="width: 216"] NYANDA ZA JUU KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
5.
[/TD]
[TD="width: 204"] BETHEL SABS[/TD]
[TD="width: 216"] NYANDA ZA JUU KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
6.
[/TD]
[TD="width: 204"] MARIAN WASICHANA[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
7.
[/TD]
[TD="width: 204"] DON BOSCO (MOSHI)[/TD]
[TD="width: 216"] KASKAZINI MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
8.
[/TD]
[TD="width: 204"] CANOSSA[/TD]
[TD="width: 216"] DSM[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
9.
[/TD]
[TD="width: 204"] ST. JOSEPH ITERAMBOGO SEM.[/TD]
[TD="width: 216"] ZIWA MAGHARIBI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
10.
[/TD]
[TD="width: 204"] CARMEL[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
4.2Shule zilizoshika nafasi kumi za Mwisho
4.2.1Shule za Serikali
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]
NA
[/TD]
[TD="width: 186"]
SHULE
[/TD]
[TD="width: 216"]
KANDA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 61"]
1.
[/TD]
[TD="width: 186"] MIHAMBWE [/TD]
[TD="width: 216"] KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 61"]
2.
[/TD]
[TD="width: 186"] DINDUMA [/TD]
[TD="width: 216"] KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 61"]
3.
[/TD]
[TD="width: 186"] KIROMBA [/TD]
[TD="width: 216"] KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 61"]
4.
[/TD]
[TD="width: 186"] MARAMBO [/TD]
[TD="width: 216"] KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 61"]
5.
[/TD]
[TD="width: 186"] MBEMBALEO [/TD]
[TD="width: 216"] KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 61"]
6.
[/TD]
[TD="width: 186"] KINJUMBI [/TD]
[TD="width: 216"] KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 61"]
7.
[/TD]
[TD="width: 186"] LITIPU [/TD]
[TD="width: 216"] KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 61"]
8.
[/TD]
[TD="width: 186"] LUAGALA [/TD]
[TD="width: 216"] KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 61"]
9.
[/TD]
[TD="width: 186"] MIGURUWE [/TD]
[TD="width: 216"] KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 61"]
10.
[/TD]
[TD="width: 186"] NAPACHO [/TD]
[TD="width: 216"] KUSINI[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
4.2.2Shule Zisizo za Serikali
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] NA.[/TD]
[TD="width: 204"]
SHULE
[/TD]
[TD="width: 216"]
KANDA
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
1.
[/TD]
[TD="width: 204"] MFURU[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
2.
[/TD]
[TD="width: 204"] PWANI[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
3.
[/TD]
[TD="width: 204"] DORETA[/TD]
[TD="width: 216"] KATI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
4.
[/TD]
[TD="width: 204"] KIGURUNYEMBE[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
5.
[/TD]
[TD="width: 204"] RURUMA[/TD]
[TD="width: 216"] KATI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
6.
[/TD]
[TD="width: 204"] AT-TAAUN[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
7.
[/TD]
[TD="width: 204"] JABAL HIRA SEM[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
8.
[/TD]
[TD="width: 204"] MKONO WA MARA[/TD]
[TD="width: 216"] MASHARIKI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
9.
[/TD]
[TD="width: 204"] KILEPILE[/TD]
[TD="width: 216"] NYANDA KUSINI[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"]
10.
[/TD]
[TD="width: 204"] KIUMA[/TD]
[TD="width: 216"] NYANDA KUSINI[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
5.0UFAULU WA WANAFUNZI
Wanafunzi Walioshika Nafasi Kumi za Mwanzo
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 511"]
[TR]
[TD="width: 43"] Na[/TD]
[TD="width: 222"]
JINA
[/TD]
[TD="width: 72"] JINSI[/TD]
[TD="width: 174"]
SHULE
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"] 1.[/TD]
[TD="width: 222"] MAGRETH KAKOKO[/TD]
[TD="width: 72"] KE[/TD]
[TD="width: 174"] ST FRANCIS[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"] 2.[/TD]
[TD="width: 222"] QUEEN MASIKO[/TD]
[TD="width: 72"] KE[/TD]
[TD="width: 174"] ST FRANCIS[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"] 3.[/TD]
[TD="width: 222"] LUKUNDO MANASE [/TD]
[TD="width: 72"] ME[/TD]
[TD="width: 174"] KAIZIREGE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"] 4.[/TD]
[TD="width: 222"] FRANK J NYANTARILA[/TD]
[TD="width: 72"] ME[/TD]
[TD="width: 174"] KAIZIREGE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"] 5.[/TD]
[TD="width: 222"] GRACE MSOVELLA[/TD]
[TD="width: 72"] KE[/TD]
[TD="width: 174"] ST FRANCIS[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"] 6.[/TD]
[TD="width: 222"] HARIETH MAKIRIYE[/TD]
[TD="width: 72"] KE[/TD]
[TD="width: 174"] ST FRANCIS[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"] 7.[/TD]
[TD="width: 222"] ROBINNANCY MTITU[/TD]
[TD="width: 72"] KE[/TD]
[TD="width: 174"] ST FRANCIS[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"] 8.[/TD]
[TD="width: 222"] HUMRATH LUSHEKE[/TD]
[TD="width: 72"] KE[/TD]
[TD="width: 174"] ST FRANCIS[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"] 9.[/TD]
[TD="width: 222"] MUKHSIN HAMZA[/TD]
[TD="width: 72"] ME[/TD]
[TD="width: 174"] KAIZIREGE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 43"] 10.[/TD]
[TD="width: 222"] ANASTAZIA KABELINDE[/TD]
[TD="width: 72"] KE[/TD]
[TD="width: 174"] KAIZIREGE[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
6.0HITIMISHO
Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili mwaka 2012, yanaonesha kuwa kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka asilimia 45.40 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 64.55 mwaka 2012. Aidha, watahiniwa 249,325 wataendelea na masomo ya kidato cha tatu mwaka 2013. Napenda kuwapongeza wanafunzi wote waliofaulu kuendelea na masomo na kuwataka kuendelea na bidii katika kujifunza.
Kwa upande mwingine, watahiniwa 136,946 ambao wameshindwa kupata wastani wa ufaulu wa alama 30 na wale waliofutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013. Ni vema ikaeleweka kuwa kukariri kidato si adhabu bali ni kutoa fursa nyingine kwa mwanafunzi kuweza kupata maarifa, stadi na ujuzi wa elimu ya sekondari kidato cha kwanza na cha pili kwa kiwango kizuri. Hivyo ni matumaini yangu kuwa wanafunzi hawa watafanya bidii katika kujifunza na kuzingatia masomo ili waweze kufaulu, pia walimu kuwasaidia Wanafunzi hao waweze kufanya vizuri.
Serikali kwa upande wake itaimarisha usimamizi wa elimu katika ngazi ya shule na kuziwezesha shule kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ikiwa ni pamoja na walimu kubadili mikakati ya ufundishaji na ujifunzaji na wazazi kufuatilia maendeleo ya wanafunzi.
Vilevile, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) itaendelea na jitihada zake za kuimarisha na kuboresha mazingira ya utoaji elimu bora kwa kujenga maabara za sayansi, kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu, kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kuimarisha usimamizi wa shule. Aidha, wizara itaendelea kutoa walimu kwa awamu kila mwaka ili kukabiliana na upungufu uliopo.
Mhe. Philipo Mulugo (Mb)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
11/01/2013

Wamechakachua live.
 
unasikia bwana mdogo, huwezi kumuondoa mtendaji muhimu wa serikali kwa hoja zisizo na mashiko!
hayo ni maneno ya kwenye vijiwe vya kahawa, tena kutoka kwa watu wasio na responsibilities zozote katika jamii zao.
labda ningewashauri tu, mjaribu kutumia muda wenu vizuri ili Taifa liondokane na umaskin

Umasikini utaondoka tukianzia na elimu. Huwezi kuondoa unasikini kwenye taifa ambalo elimu ni duni, na isiyo na mwelekeo na yenye kuyumbishwa kila leo.Tatizo mmeingiza siasa hadi kwenye vitu muhimu kama elimu, itaigharimu sana nchi hii. Km leo mwanafunzi anapata 70/250 anaitwa amefaulu, na km shule inaletewa wanaunzi wanoambiwa eetii wamefaulu kwa alama zaa juu sana, alafu hata kuandika ni tabu.

Kila nikiushirikisha ubongo wangu kikamilifu nashindwa kupata majibu.
 
Eheeeeeeeeeeeee asante sana kwa kujitokeza, wewe unatumiaje nafasi yako ili kuliondo taifa kwenye umaskini?
Unajua waliokwenye vijiwe wanauwezomkubwa sana hata wakati mwingine kukuzidi, chondechonde hiyo ni nafasi tu usijaribu kuwadharau watu, neno bwana mdogo tafsiri yake nini?

Naomba panga muda kama zito alivyofanya uje hapa Jf ujibu maswali ya GREAT THINKERS

Sidhani kama atakuwa na uthubutu wa kufanya hivyo. Let us wait and see.
 
Mi sina uhakika ila nasikia kuna naibu waziri wa elimu,kabla yake alikua STD 7 leaver,mwalimu wa UPE,sasa ni Regional commissioner.Hayakuanza leo atii.
:confused2:
 
Yule jamaa aliyekuja
na muungano wa pemba na zimbambwe south Africa, leo amenifurahisha sana
alipokuwa anatangaza matokeo ya kidato cha pili kwa mambo mawili<

1. Eti mikoa ya kanda ya ziwa ni Mwanza na Mara.
2. Ameshindwa kabisa kutamka neno Thaqaafa second. anatamka swafaka
ee, swaaa, swaa................ hadi alipopata msaada wa waandishi wa
habari jinsi ya kutamka neno hili.

Hapa sitaki tena na tena kuamini kwamba hii ni MISTAKE hii ni ERROR
japo sina uhakika kama anajua tofauti ya maneno hayo.

Mch. Msigwa alishasema, "akili ndogo haiwezi kuongoza akili kubwa".
Mkuu huyu jamaa hata mimi nilimuona akiangaika kutamka, nilijiuliza maswali mengi sana...
Huyu jamaa ni kiazi kabisa...
 
hivi ni kwa nini matokea yanatangazwa kwa kusema shule kumi bora za serikali na binafsi kwani mitihani inakuwa na utofauti au ndiyo utaratibu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom