denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Habari zinazoripotiwa na vyombo mbalimbali wakati huu zinadai yule mshambuliaji hatari wa Borrusia Dortmund ya Ujerumani, Erling Braut Haaland, ametua rasmi Man City.
Amesaini mkataba utakaomuweka Etihad mpaka mwaka 2026 huku ikitajwa atapokea kiasi cha £375,000 kwa wiki, na kumfanya awe sawa na kiungo De Bruyne anayepokea kiasi kama hicho.
Man City wamempata baada ya kutoa kiasi cha £ 63 milioni kilichowekwa kwenye mkataba wake na Dortmund kwa timu ambayo ingemtaka. Sasa ni suala la kusubiri tuone kama atawika kama alivyofanya akiwa Ujerumani.