Sababu Zinazopelekea Mashabiki kumkataa Boy Friend Mpya wa Nicki Minaj. - Kenneth Petty yupo kwenye orodha ya watu hatari zaidi waliotenda makosa ya Kingono 'Level two registered sex offender' mjini New York, Polisi wanaimani ni mtu atakaye fanya makosa hayo tena na atakuwa kwenye hio orodha maisha yake yote. - April 1995 Kenneth Petty alihukumiwa kifungo cha miaka 4 na miezi mitano jela kwa kosa la kutaka kufanya ubakaji dhidi ya binti mwenye umri chini ya miaka 16. Muda huo Kenneth alikuwa na miaka 15. - Kenneth alikubali kosa la kuua bila kukusudia baada ya kumpiga risasi Lamont Robinson mwaka 2002, alitumikia miaka saba jela, mitatu chini ya uangalizi wa polisi na alikuwa mtu huru rasmi May 2018. - Nicki Minaj anamjua Kenneth toka utotoni ndio maana anaimani naye na anamfahamu kuliko mashabiki zake, Aliwahi kujibu kuwa >Watu kwenye Internet hawawezi kuendesha maisha yangu, nyie wenyewe hamuwezi kuendesha maisha yenu