Habari kwa Picha

Habari kwa Picha

IMG_20190224_201325.jpg
TATIZO LA KUKOSA USINGIZI (INSOMNIA) NA TIBA YAKE - Kwa kawaida mtu mzima anatakiwa kulala saa 7-8 kwa siku lakini kuna ambao hushindwa kulala kabisa au hulala kwa masaa machache sana kutokana na sababu mbalimbali - Insomnia ni tatizo la kukosa usingizi japokuwa una fursa ya kuweza kulala na huweza kuwa la muda mfupi au mrefu (miezi sita au zaidi) - Sababu huwa ni upungufu wa homoni ya melatonini ambayo husaidia kudhibiti mzunguko wetu wa kawaida wa kulala na kuamka na hurekebisha saa ya mwili(biological clock) - Nyingine ni magonjwa mbalimbali kama pumu, matatizo ya moyo, kipanda uso na kuwashwa au mzio, matumizi ya baadhi ya dawa kali zenye kemikali, upungufu wa hormone za kijinsia (estrogen), msongo wa mawazo, ugomvi na kelele na kuishi au kufanya kazi za usiku katika mazingira yenye mwanga kwa muda mrefu - Athari zake ni uchovu wa mwili au kuhisi mwili hauna nguvu, hasira bila sababu za msingi, maamuzi mabovu, kupoteza kumbukumbu na kupatwa na magonjwa ya shinikizo la damu au kisukari - Pendelea kula zaidi vitu asilia kama mboga za majani na matunda na punguza vyakula au vinywaji vyenye caffein, kunywa maji kwa wingi, kutumia asali mbichi vijiko viwili usiku, kuweka mazingira mazuri ya kulala na kutumia dawa zinazorekebisha kiwango cha melatonini mwilini
 
'Mchungaji' AlphLukau kutoka Afrika Kusini amezua gumzo baada ya kudai kumfufua mtu wakati wa ibada Februari 24. Imeelezwa kuwa mtu huyo aliyedaiwa kufariki tangu Ijumaa alikuwa akipumua ndani ya jeneza. Wananchi wametaka serikali iwazuie wachungaji hao wanaowahadaa kwa miujiza.
52337629_361873537987214_9203296945665038075_n.jpg
 
Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika mwenye miaka 81 na kwa sasa ni mdhoofu anayetembelea wheel chair, anatarajiwa kugombea tena kwenye muhula ujao kama ambavyo amejitangaza. Bouteflika yuko madarakani tangu mwaka 1999.
51651272_315004272553030_6130015291508663264_n.jpg
 
DAR ITAMUAGA JUMAMOSI: ATAZIKWA BUKOBA. Ndugu Kashasha ambaye ni msemaji wa Familia ya Mutahaba amesema kama mambo yakienda kama yalivyopangwa, mwili wa #RugeMutahaba utawasili jijini Dar es salaam kutokea Afrika Kusini siku ya IJUMAA (March 1/2019). Ikiwa hivyo wakazi wa Dar es Salaam watatoa heshima za mwisho na kumuaga mpendwa wetu siku ya JUMAMOSI (March 2/2019). . . Baada ya hapo: Familia imeamua kwamba Ruge atakwenda kuzikwa nyumbani kwao huko Bukoba siku ya JUMATATU (March 4/2019) (Jumapili mwili utasafirishwa kwenda Bukoba)
 
'Mchungaji' AlphLukau kutoka Afrika Kusini amezua gumzo baada ya kudai kumfufua mtu wakati wa ibada Februari 24. Imeelezwa kuwa mtu huyo aliyedaiwa kufariki tangu Ijumaa alikuwa akipumua ndani ya jeneza. Wananchi wametaka serikali iwazuie wachungaji hao wanaowahadaa kwa miujiza.View attachment 1031748
Aliyefufuliwa aumbuliwa na mfanyakazi mwenzake|| Baada ya kusambaa kwa habari zilizoleta sintofahamu kutoka nchini Afrika Kusini za mchungaji kumfufua mtu, mapya yanazidi kuibuka juu ya tukio hilo ambalo mpaka sasa imekuwa vigumu kwa wengi kuamini kuwa ni kweli limefanyika. Habari kutoka Afrika Kusini zilizochapishwa kwenye mtandao wa Eye Witness zinasema kwamba mtu huyo aliyefufuliwa anajulikana kwa jina la Brighton, ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya mbao ya PTY katika mji wa Pretoria, na tayari ameshakamatwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi. Akimuelezea Brighton, mmiliki kampuni hiyo Vincet Amoretti, amesema kwamba kwa mara ya mwisho Brigton alionekana ofisini Februari 19 huku akiwa amechelewa akitokea mazishini siku ya February 16 na 17, na alichelewa kurudi baada ya wazee kumuomba akae kwa siku moja zaidi. Vincent ameendelea kueleza kwamba si mara ya kwanza kwa Brighton kufanya hivyo kwa mchungaji wake (Alph Lukau), kwani alishawahi kumsaidia kwenye muujiza mwingine ambao alijifanya kiwete na kupata uponyaji, huku akimsifia kuwa ni mchapakazi kwa kuweza kufanya kazi sehemu mbili. “Unaweza kufikiria ni maisha gani alikuwa nayo!?. Alifanya kazi kwangu, akafa, akafufuliwa na sasa amekamatwa na polisi”, amesema Vicent. Hata hivyo tume inayoshughulika na masuala ya dini na utamaduni imesema haitalifumbia macho tukio hilo, na kwamba lazima hatua za kisheria zichukuliwe.
 
Pascal Cassian awachana wanafiki wanaompamba Ruge baada ya kuaga dunia na ambao bado wanaendeleza chuki zisizo na maana... . . 'Hebu angalia Sasa huu upendo usio wakweli. Hebu angalia wale ambao wamempost TU kaka etu kwenye peg zao wakisema tutakukumbuka kaka tulikupenda kaka Sasa hizo post angeziona kabla hajalala mauti ingemjengea Nini huyu ndugu moyoni mwake ? Hakika angeona KUMBE kweli mchango wangu niwamhim KATIKA jamii lakini wakat ruge anahitaji msaada au pengine alihitaji maombi TU yawatanzania namaneno yamatumaini huenda Mbingu zingefanya Jambo juu ya kaka etu lakini tunangojea mtu akifa ndo unafiki unaanza kupost upendo WAUONGO Wala hazimsadii chochote kwani hasikii haoni kwanini tusifanye wema kwawatu wakiwa pumz haijatoka? Kwanini tunasubili kuonyesha ufahali wakati wamsiba? Nakwenye peg zatu hebu tujue yakuwa duniani Kila mmoja niwamhim nakishatoweka huwa hayupo wakuziba pengo hivyo tuacheni utim huyu niwahuku nayule niwahuku Sasa upendogani Sasa huu tunamuonyeshea malehem asie sikia ? Wengine wamesema AAA! Anatafta pesa TU huyo anapesa hawez kuchangisha unajuwaje? Kama anapesa? Jamani tutahukumiwa cku zamwisho hebu WWE ulikuwa unamchukia huyu ndugu hadi amekufa bado unachuki hamkutengeneza yungali hai Sasa Atakusamehe Nani Sasa umeshindwa kutengeneza nae akiwa hai? Mungu yupi atakusamehei ? Watanzania tujifunze kutokana na matatizo haya waimbji nawasanii sisi tunategemeana duniani hakuna spea yaruge leo poleni Sana crauzi kwamsiba mzito naona uchungu mnao upitia mtu mulilo kula nae mna cheka nae hata Kama alikuwa namapungufu ila inauma sana'
 
Watoto wa proffesor Mutahaba katika picha ya pamoja
51503835_2524801044197053_3096366792140275382_n.jpg
 
Pichani mwanadada huyo mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye ndevu ambaye hujiita malkia wa nywele ameachia muonekano huo mpya na kusema kwasasa hana mwanaume yupo singo.
51820254_310670302925310_8977068767662433675_n.jpg
 
Kiwanda cha Bora kilichopo barabara ya Nyerere, Dar es Salaam kimeungua moto tangu alfajiri leo Februari, 28 na jitihada za kuuzima zinaendelea.
51861677_544160162746461_6375813375737230323_n.jpg
 
Mtoto njiti aliyezaliwa akiwa na uzani mdogo zaidi duniani akiwa sawa na kitunguu au kiazi cha gramu 268g pekee ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kusalia hospitalini kwa miezi 6 tangu alipozaliwa mjini Tokyo nchini Japan.
 
MTOTO ALIYEIBWA NA KUUZWA TSH 30,000 APATIKANA - Mtoto Shazira Yahaya aliyeibwa akiwa na siku saba katika Kijiji cha Likalangiro Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, amepatikana katika Kijiji cha Kokirie Wilaya ya MoshiVijijini mkoa wa Kilimanjaro, ambapo aliuzwa kwa Sh 30,000 - Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Gemini Mushy, alisema mtoto huyo ambaye sasa ana miezi mitano, aliibiwa Septemba 26, 2018 na alipatikana Moshi vijijini Februari 18, 2019 - Mtuhumiwa wa wizi huo Abrahamu Kilewa (20) mkazi wa kijiji cha Mahanje na alienda kumuuza mtoto huyo kwa Anosiata Luambano (36) ambaye ni mfanyabiashara na ni mkazi wa Marangu - Hadi sasa watuhumiwa wote wanashikiliwa na Polisi huku taratibu za mtoto huyo kukabidhiwa kwa wazazi wake zikiendelea.
52412137_370494083788591_525713724270428245_n.jpg
 
VIOJA VYA KALE: KODI YA NDEVU : Kule Uingereza miaka ya 1533 alikuwepo mfalme mmoja alijulikana kama King Henry VIII. Mfalme huyu kimtaa mtaa vijana wangemuita bedui. Kwanza alikuwa analala na sururu ndogo. Alikuwa analala na sururu kwa sababu hakuwahi kumwamini sana kila mtu aliyekuwa karibu yake hasa hasa wake zake. : Alifanikiwa kuoa wake 6 kwa nyakati tofauti tofauti. Wawili walionyongwa kutokana na kushukiwa na uzinzi, ambapo mmoja wao kaka yake aliuawa pia kwa kuhisiwa kula njama na mke wa mfalme ili kumuua mfalme. Mmoja alidumu nae miaka 24, wawili walipewa talaka na mmoja alifariki. : Mfalme huyu pia aliidhinisha kodi ya ndevu. Kwa mwanaume yeyote mwenye ndevu lazima ulipe kodi. : Mbali na historia yake ya kibabe, kwenye masuala ya dini hakuachwa mbali. Kumbukumbu zinasema huyu ndiye mfalme wa kwanza kabisa kumjibu Martin Luther Sir aliyeandika majarida na kuanzisha midahalo ya kulipinga kanisa katoliki. : Mfalme Henry ndiye aliyekuwa mtawala wa kwanza wa Kiingereza kukubali biblia ya Great Bible ambayo ndiyo biblia ya kwanza ya kiingereza kusomwa makanisani. : Baadae alitangazwa kuwa mlinzi wa Imani na Papa Leo X. Hata hivyo kanisa lilimfutia uwezo wa kupokea sakramenti kama komunyo na kumtenga kama mkatoliki. : Hii ilitokea mara baada ya kumshurutisha Papa amsaidie kutoa talaka kwa mkewe Catherine. Papa aligoma. : Mgomo huo ndio uliotenganisha kanisa la Anglican (Waanglikana) na ukatoliki na Mfalme huyo akajitangaza kuwa kiongozi wa kanisa la Kiingereza (Anglican)
54248109_298960794106893_375967585083439669_n.jpg
 
Mwanamuziki Jennifer Lopez amevishwa Pete ya Uchumba kwa mara ya 5 na mchumba wake Alex Rodriguez. Mara ya kwanza Jlo alichumbiwa mwaka 1997 na Ojani Nia penzi halikudumu sana baada ya mwaka wakaachana. Cris Judd aliyekuwa dansa wake kushika hatamu ndani ya mwaka mmoja tu penzi chaliii. Mwingine aliyewahi kulamba asali na pete akamvisha ni Muigizaji Ben Affleck couple iliyopewa jina Bennifer ndoa yao ilidumu kwa miaka miwili tu na kuvunjika. Baadae Jlo alichumbiwa na Muimbaji Marc Anthony na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili mapacha
53584792_1686558348112602_5957254124184436820_n.jpg
 
Sababu Zinazopelekea Mashabiki kumkataa Boy Friend Mpya wa Nicki Minaj. - Kenneth Petty yupo kwenye orodha ya watu hatari zaidi waliotenda makosa ya Kingono 'Level two registered sex offender' mjini New York, Polisi wanaimani ni mtu atakaye fanya makosa hayo tena na atakuwa kwenye hio orodha maisha yake yote. - April 1995 Kenneth Petty alihukumiwa kifungo cha miaka 4 na miezi mitano jela kwa kosa la kutaka kufanya ubakaji dhidi ya binti mwenye umri chini ya miaka 16. Muda huo Kenneth alikuwa na miaka 15. - Kenneth alikubali kosa la kuua bila kukusudia baada ya kumpiga risasi Lamont Robinson mwaka 2002, alitumikia miaka saba jela, mitatu chini ya uangalizi wa polisi na alikuwa mtu huru rasmi May 2018. - Nicki Minaj anamjua Kenneth toka utotoni ndio maana anaimani naye na anamfahamu kuliko mashabiki zake, Aliwahi kujibu kuwa >Watu kwenye Internet hawawezi kuendesha maisha yangu, nyie wenyewe hamuwezi kuendesha maisha yenu
 
Back
Top Bottom