Vyuo vyetu vinakosa ile nafasi nyeti ya idara ya ushauri. Vyuo vya majuu lazima idara hiyo iwepo ambayo imesheheni wataalamu wa kike na kiume ambao wanapigania haki za wanafunzi dhidi ya wahadhiri. Wahadhiri vyuo vya majuu wanaogopa wanafunzi wa vyuo kujihusisha kimapenzi kama ukoma, maana ikitokea ni kashfa nzito ya kupelekwa mahakamani na kuanikwa kwenye luninga na kuaibishwa hata mijusi wajue kilichojilia.
Hatuna ofisi za makada washauri katika vyuo,na wachache waliopo hawafanyi kazi kwa uzito stahiki, kwani wataalamu hao wangekuwa na nafasi ya kuwaelimisha wanafunzi na kutetea haki zao, na pale linapotokea jambo kama hilo wangetetewa, lakini mambo yanavyokwenda ni kama mwanafunzi akithubutu kufanya hivyo utaona wahadhiri wanalindana na kumsikisha adabu mwanafunzi kwa utetezi kwamba hakuna ushahidi kwa kuwa mambo hayo hufanyika kwa siri.
Kungekuwa na idara hiyo ya ushauri, litokeapo jambo kama hilo mwanafunzi anaweza kushirikiana na washauri kwa kuweka mtego wa picha na kinasa sauti mbinu ambayo majuu imewaangamiza wahadhiri wengi na kuishia kwenda kufanya kazi za construction au warehouse kuendesha folk lift kwa hisani tu.
Mkuu idara za ushauri na utetezi kwa wanafunzi zipo kiaina.
Vyuo vikuu vya umma hapa TZ vina ofisi za
dean of students, ambapo kunakua na mshauri na mtetezi wa wanafunzi.
Ila kusema ukweli idara hizo siwezi kuzilinganisha na idara kama hizo kwa majuu (ambako kuna students counseling services za hali ya juu mno). Hata hivyo, idara hizi katika vyuo vyetu haziwezi kukwepa lawama katika matatizo kama haya; kwani hazifanyi kazi zake ipaswavyo licha ya kua na wataalamu wa masuala ya ushauri (counseling and guidance). Pia mfumo wa hizi idara katika vyuo vyetu haupo katika hali ya kuweza kweli kuwatetea wanafunzi pale wahadhiri wanapokua na hatia; kwani ni wahadhiri hao hao ndio wapo katika nafasi za maamuzi katika idara hizo. Hivyo inakua ni sawa na kesi dhidi ya ng'ombe kupelekwa ikaamuliwe na nyati!! Mfano ni kesi ya mhadhiri mmoja pale UD ambae anasifika sana kwa kuongea maneno machafu (matusi) darasani; kesi ilipelekwa na masista ambao hawakufurahishwa na mwenendo wa mhadhiri huyo. Kesi ilifika kwa nyati, nyati na ng'ombe wakaelewana na kupeana madongo ya hapa na pale. Kisha mhadhiri huyo alirudi darasani na kujitapa kwamba anawashangaa hao walioenda kumshtaki; na aliendelea na tabia yake hadi kesho!!
Pia kuna jambo jingine ambalo hata wakuu humu wameligusia; nalo ni kuwepo kwa wanafunzi ambao wanatumia kila mbinu ili kuwa tempt wahadhiri katika kufanya ngono kwa manufaa ya kufaulu. Na wakati mwingine kuna extreme cases ambapo wanfunzi hao wameweza hata kutengeneza scenarios za kubakwa ili kuwa tempt wahadhiri wawepe maksi nzuri. Mifano ipo mingi sana; pale UD kuna wahadhiri watatu ambao walishakumbwa na visa vya kusingiziwa wamebaka wanafunzi (kusingiziwa na wanafunzi wanao claim kubakwa). Mmoja wa kitivo cha sheria, mwingine wa kitivo cha elimu na mwingine kitengo cha Archaeology
Kuna mwanafunzi mmoja wa shahada ya pili (alikua dada kutoka nchi moja ya Afrika Magharibi), kwa mujibu wa supervisor wake, huyo dada alikua academically weak. Hivyo alikua akipata shida kuweza kuandika chapisho (thesis) lake vyema; basi katika kuweza kutafuta njia za mkato, huyo dada pamoja na mhadhiri mmoja wa kike katika kitengo hicho hicho alicho supervisor wake, wakapanga kutengeneza scenario ya kubakwa. Yule mhadhiri wa kike ana ofisi katika floor moja na ilipo ofisi ya supervisor wa yule dada, ingawa kuna ofisi kama nne kati ya ofisi zao. Basi katika zoezi hilo, dada alienda katika ofisi ya supervisor wake katika kujaribu kumshawishi supervisor alegeze kamba juu ya chapisho lake; kwa mujibu wa supervisor huyo, yeye alikataa, ndipo dada akararua nguo zake na kupiga kelele kwamba anabakwa. Na mtu aliesikia kelele hizo ni yule mhadhiri alie ofisi kama ya tano kutoka ofisi ya supervisor, yeye ndie alikua wa kwanza kuja kwenye eneo la tukio. Na yeye ndie akawa shahidi wa dada yule!! Basi maskini mhadhiri wa watu akawa suspended akisubiri kesi kusikilizwa. Wakati wa kesi, watu wenye
common sense wakauliza ilikuaje mtu alie na ofisi mbali vile asikie kelele za mtu kubakwa ilhali kulikua na watu wenye ofisi karibu ambao hawakusikia kelele hizo!?! Basi badae mdada alikuja kukiri na kusema namna walivyopanga na mhadhiri yule wa kike.
Pia pale kitivo cha sheria; kwa wale waliopita UD wanajua namna gani wahadhiri wa sheria wanavyobania maksi. Basi kuna mdada moja nae alitengeneza scenario ya kubakwa; alienda kwenye ofisi ya mhadhiri mmoja kudai apewe maksi nzuri, mhadhiri akagoma. Basi binti alifunga mlango na kuweka funguo ndani ya brassiere, akararua nguo yake ya juu na kuanza kupiga kelele za kubakwa; watu kusikia kelele, wakaja na kukuta mlango umefungwa na binti funguo katia chobisi!! Sasa kwa hali hiyo kweli mpaka huyo mhadhiri akaaminiwe si itakua kazi!! Pia ni udharirishaji wa hali ya juu kwa mhadhiri ambae ana sifa, familia na marafiki!!
Kwa hiyo mkuu, wakati mwingine wanafunzi ndio uwa wakorofi na wanajaribu kila mbinu ya kuwawezesha kupata maksi nzuri. Njia ya kuepusha scenarios kama hizo ni kuwa na umakini katika namna ya kudeal na watoto wa kike. Kwa mfano, Palamagamba pale UD ana utaratibu wa kwamba, daima haachi funguo katika mlango wake akiwa ofisini na pia endapo binti anashida ya kuja ofisini kumwona, ni aidha aje na mwenzake (yaani wawe wawili). Na hii ni kutokana na aibu aliyoipata mhadhiri mwenzake.
Kwa upande mwingine wa shilingi; ni kweli kuna wahadhiri ambao wanawashawishi mabinti katika kufanya nao ngono ili wapate maksi nzuri. Pale SUA kuna profesa mmoja alikua na mchezo huo sana, kiasi kwamba kukawa na utani kwamba, binti yeyote atakaeitwa na huyo profesa ofisini kwake, basi ajiandaa kabisa kwa kubeba condom!! Pia UDOM kuna kesi za wahadhiri kuitwa shemeji na wanafunzi kutokana na wao kutembea na wanafunzi wa kike!! Hadi kuna mhadhiri mmoja nasikia aliandikiwa barua na wanafunzi wa kike (barua zilisambazwa kila ofisi!!) kutokana na tabia yake ya kutembea nao.
Kwa hiyo mkuu licha ya hizo case mbili, kuna haja ya kufanyika utafiti wa kina kabisa (nashangaa watu wanaosoma sociology au psychology wanasubiri nini hapa!!) katika kutafuta ukweli wa jambo hili. Pia kuna haja ya idara za ushauri na utetezi wa wanafunzi kuongozwa na watu wasio wahadhiri (watu watakao kua neutral).