Mimi nimekaa Vyuo Vikuu hapa nchini kwa zaidi ya miaka 20 sasa! Nadiriki kukutukana! Sijui nikuite nini- Mwoga! Kawaida kabisa kila Chuo kina serikali ya wanafunzi, kamati mbalimbali na zaidi wapo walezi ama walimu au kupitia kurugenzi za Wanafunzi(Deans of Students). Unawezaje kukuaa kimya haya maujinga yanapotendeka bila kutoa taarifa! Hata jamani kutuma sms kwa wakubwa ili wakemee tabia hii! Mnatuchafulia jina sisi tunaofundisha na hao dada zenu ambao wanajitahidi katika masomo.
Wanafunzi wadhaifu ni waoga kumfuata mwalimu kuomba msaada wa ziada na hasa wanaume. Wanajisikia (self pride) kiasi kuona ni kujiangusha kwenda kutafuta maelezo zaidi kwa walimu. Wasichana hujituma na kumfuata mwalimu kujua zaidi. Sikanushi kabisa kwamba tatizo la walimu kuwa na urafiki na wanafunzi wao lipo, la hasha. Napata shida kuamini mwanafunzi anaweza akapasishwa kwa kulala na mwalimu. Kama mjuavyo UE sio kuamulia na mtu mmoja.
Kwa ajili ya mawazo finyu kama ya mwandishi huyu- vijisichana (nawatukana ndiyo!) vilivyoshindwa mitihani kihalali, hukata rufaa na kudai eti nilikataa kutoa hongo!
Mwisho tuwe wakweli, kama kuna wahadhiri wadhambi hawa ni kuwafichua kupitia njia nyingi zilizopo, ili waondolewe mara moja!