Habari marafiki wote wa jamii naomba msaada au wazo kuhusu vidonge vya kuwa mweupe

unlucky

Senior Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
199
Reaction score
56
Mimi ni mtanzania na nina watoto watatu sitaki kuzaa tena na nimechoka kutumia lotion za bei ghali nimeamua kununua glutathione ivory cost ya 1500 mg nimesoma net vinasifika na zimewafaa watu wengi ni herbal ni natural supplement inavyosema na haina side effect bado sijala nimeviweka tu je ndugu zangu mnanishauri vipi je hayo ya net kweli na hao waliouza pia washawauzia wengine pia wameona mafanikio je hapo nifanyaje mimi na nimenunua bei ya juu sana hizo vidonge.
 
Maskini weee hiyo ni dalili ya kujikataa, sijui kama unajua kuwa wewe ni unique, na aliyekuumba hakukosea!
 
Lol...never heard this before...thank God i love me#u need a confidence boost?????google Lupita Nyong'o#
 
Sasa unakuta huyo ni msomi kabisa tena ana Masters ama PhD anaomba ushauri awe mweupe maana hataki kuwa mweusi kisa lotion bei ghari sana,yaani mpaka hapa wewe thamani huna kabisa unataka uwe mzungu kwakunywa dawa?
Ukienda TFDA pale HQ unashangaa kabisa watu ni wakujichubua halafu ndiyo wasomi wa kuzuia vipodozi hatari kweli?

Tembelea maofisi yetu hapa nchi wamama na wadada wanahangaika na mikorogo inayopigwa marufuku na serikali halafu wanasema ni makeup. Dada tulia na ulivyopewa na Mungu maana weusi sio ugonjwa ila sasa huo weupe unaotaka wewe ndiyo ugonjwa,jiamini ili nasi tukuamini hivi nywele kwenda kuweka kwenye dryer ndiyo uzuri,ama weupe?Tulia wewe.
:nono:
 
Uzuri hutoka kwa MUNGU lakini utanashati ni sanaa
unachotafuta wewe ni uzuri sasa unafanya masahihisho kwa maana Mungu amekosea?
 
dada unahangaika nini yote hayo kutaka kumkosea Muumba wako?!mbona wadada wengi weusi wanavutia na kupendeza tu. hiyo dawa iwe iko na side effect nzuri au mbaya nakushauri usitumie(kama unamuogopa aliyeekuumba na unaamini ipo siku utarejea kwake) kinyume na hapo endelea unavyotaka kufanya dada kwani uamuzi ni wako.
 

Mwanamke mjinga huibomoa nyumba yake kwa mikono yake yeye mwenyewe ndiyo huyu sasa<kusoma hajui hata picha
 
once u go black u neva go back...!! jiulize kwann unataka weupe!!!? nan anaona weusi haukupendezi? ingia ndan yako jiulize (self introspection)
 
unataka weupe kwaajili ya kummvutia nani-?manake hata uwe mrembo vipi! Au mbaya vipi lkn mwisho wa siku unaishia kwenye himaya ya mwanaume,kwani hivyo ulivyo na weusi wako unadhani huwavutii wanaume? Hawo watoto ulipata mimba kwa kupiga punyeto?
Usibabaike na weupe,mwisoh wa siku mwanaume ndoo anachagua mwanake atakae mpendeza yeye,
Kama anataka mwanamke mweupe,mweus,mnene au mwembamba ni chaguo lake!
Na ndoo maana muumba akatuumba hivyo kwa flavour na mwonekano tofautitofauti,Juzijuzi tuu humuhumu jf kuna jamaa alikuwa anawasifia black beauty women,Sasa na kushangaa wewe ambaye hujikubali!

USHAURI
Kama uliweza kununua hivyo vidonge inaonesha,ulidhamiria kufanya hivyo,
Haya meza tuu,Ni vidonge vizuri tuu kama ulivyoshauriwa na aliekuelekeza ukanunue.mi naona wala haukuwa na haja ya kuingia humu na kutaka ushauri.
 
kukubadilisha rangi ya ngozi tayari ni side effect

jikubali ulivyo
 

Ridhika na jinsi ulivyoumbwa...Mungu ana kila sababu ya kukuumba hivyo...namshukuru Mungu mimi white but hatakama ningekuwa kama giza kamwe nisingejibalisha ngozi...
 
Sawa nishaelewa ss

Aisee! Nakuonea huruma sana!
Ndugu dawa zile si mzuri kabisa kwa afya ya ngozi yako!
Kwa hakika kumeza hizo dawa ni kuhatarisha afya ya ngozi yako na wewe mwenyewe kwa ujumla!
Inategemea na mtu, unaweza ubadilike uso na mikono tu huku kwenye papuchi na maeneo mengine ukawa kama ulivyokuwa mwanzo! Ukifikia hatua hiyo, unakuwa mzuri nje but ukivua tu vichekesho!
...
Vile vile ukimeza hayo madonge ujisabilie kuwa na ngozi kama ya kenge unless mapoda na makorokocho mengine yawe fullu time zote kabatini mwako na mwilini mwako! Hivi kweli kwa sababu ya weupe ndio ukubali utumwa wote huo?
...
Alafu ukitaka kumeza hayo madonge mpigie Mungu umwambie akuhakikishie hautopata ajali or kujikata sehemu yoyote itakayohitaji kushonwa!
...
Hem jikubali, you are black beauty! Tena uzingatie, uzuri sio rangi, uzuri ni ngozi! Ukiwa na ngozi mbaya hata uwe mweupe kiasi gani unabaki kuwa kituko tu!
...
Hem jiamini na umshukuru Mungu wako!
 
Hayo yote unataka tu uwe mweupe?wanawake wa hovyo kama wewe,wasiojiamin na rangi yao sijui kwa nin mlizaliwa,bora ungezaliwa fisi tu.

Mkuu Kichwa Ndio Mtu naona umechukia kweli, naona hapo kwenye red umeshidwa hata kujizuia hayo maneno kwa hasira!!! Ila hata ID yake inatoa msg kwamba hajiamini na amekata tamaa.
My dear unlucky jikubali ulivyo yaani kama mimi ni black kama mkaa ila najua weusi wangu ndio unaonifa maana sijawahi kukosa kuwa mrembo eti sababu ya rangi yangu.....Jikubali mamy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…