Mimi nina miaka 31, na
mwaka 2000 baada ya
kutoka tanzania na ngozi
yangu asili (originol)
ambayo ilikuwa ni nyeusi
na ya kun'gaa, marafiki
zangu hapa texas,
walinishawishi niwe
mweupe ili nami ning'ae.
basi nikapata vidonge vya
kungarisha mwili, yaani
kuwa mweupe. Na kusema
kweli, nilibadilika ngozi,
nikawa mweupe sana, na
siyo rahisi mtu kujua kama
kweli nimetumia madawa,
isipokuwa walionifahamu
tangu utotoni ndio
wanaoshangaa uweupe
huu nimeutoa wapi. Sasa
nilipataga mimba, ambayo
ilikuja kutoka, ila sikujua
tatizo ni nini. Hapa majuzi
tena, nikashika mimba ya
pili bahati mbaya mtoto
kafa (yaani mimba
imeharibika) nilienda kwa
dakitari kutaka kujua tatito
liko wapi, hapo ndo
nikaambiwa kwamba kuna
chemicals kwenye mwili
wangu ambazo ndio
chanzo cha watoto wangu
kufa.
nimeambiwa kwamba hayo
madini ni mengi mno, na
nisipoangalia nitakufa na
cancer ambayo inaweza
kuanza muda wowote.
suluhisho linaweza
kupatikana nikisafisha
damu, na uwezo huo sina,
au kama naweza kurudisha
ngozi yangu ya zamani
kwa sababu sasa hivi ngozi
yangu haina kinga tena.
Sisikitikii weupe, kwa
maana nikitu ambacho
nilikitamani sana, kwa hiyo
mzigo lazima niubebe,
ombi langu ni ushauri wa
kuweza kutoa hizi kemikali
mwilini mwangu.kama ni
kufa basi tena. cha ajabu
ni kwamba mchumba
wangu ametishia kuniacha
kwani siwezi kuzaa tena.
yaani sasa hivi analala nje
full, naumia lakini sina
jinsi..... naombeni ushauri
wenu, niko njia panda
mdau, texas usa
~~~~~~~~###~~~~~##~~~~~~
Tafakari unywe au utupe!!!!