Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

Habari mbaya kwa walaji wa Kitimoto: Huenda wengi wao wakaja kupata kifafa!

waislam naona mnapinga sana kitimoto coz mnajua kuwa kinafukuza majini misikitini
 
MBUNGE ANAYEDAIWA KUONGOPA ELIMU YAKE:
Jalada lafika ofisini kwa DPP


  • Ilikuwa wakati wa kampeni za uchaguzi
  • DCI asema tayari upelelezi umekamilika

Na Esther Mvungi

MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) amepokea jalada la mbunge anayedaiwa kutoa taarifa za uongo kuhusu elimu yake wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana.

Akizungumzia suala hilo ofisini kwake, Mkurugenzi wa Mashitaka, Geoffrey Shaidi, alithibitisha ofisi yake kupokea jalada hilo.
"Jalada limefika leo mezani kwangu… limepokewa ofisini Juni 6," Shaidi alisema jana.

DPP ambaye hakuzungumzia undani wa jalada hilo, alisema ofisi yake italishughulikia na hakutaka kutaja jina la mbunge kwa wakati huu.


Awali, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, akizungumza na Uhuru alisema ofisi yake imekamilisha upelelezi kuhusu mbunge huyo na kuwasilisha jalada kwa DPP.

Manumba alisema ofisi yake ilipata taarifa za malalamiko kuhusu mbunge huyo na si kweli kwamba inawahoji wengine kadhaa.

Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kuwa wabunge kadhaa wamehojiwa na polisi kwa kughushi vyeti vikiwemo vya elimu.

............................................................................................................
 
Mkuu hapa naona ni kama vile unapiga upepo rangi, utapoteza muda wako tu. Piga ua, walaji wa Noah katu hawatoacha kumla huyo mnyama. Labda waambiwe wakila watageuka matoashi may be ndio wataacha kumla Noah.
Ushauri wangu: Wewe waache tu waendelee kumla noah

Swadaktaaaa.

Asiejua maana hata ukimwambia maana ataona kama unamtukana.
 
Aaah! Jamani eeh! Huyu nguruwe 'swine', si ameharamishwa katika vitabu vya dini. Kwenye biblia hadi kuraan.
kuna maelezo yanasema sababu za ki-mazingira, kwamba kuharamishwa huko ni kutokana na magonjwa haya yalipokuwa hayaeleweki chanzo chake maeneo ya mido-isti, na kwasababu ya ujinga, ikabidi wale viongozi wajuu watangaze kuwa mungu amekataza, nao wakaamini.nchini china wanakula nguruwe miaka nenda rudi hawajapata tatizo lolote. na kwa nyongeza nyama inayoongoza kwakuliwa sana ulimwenguni ni ya kitimoto.
pia kiafya wanashauri kuacha ulaji wa red meat mfano nyama ya ng'ombe na kwa usalama zaidi wanashauri ulaji wa white meat kama nyama ya nguruwe.
 
kutokana na takwimu ulimwenguni nyama ya kitimoto ndio nyama inayoongoza kuliwa ulimwenguni kuliko aina nyingine ya nyama yaani kuliko kuku,samaki, dagaaa,bata, mbuzi,kondoo, ngombe,sungura, nyani, mbwa, n.k. kitimoto inaongoza kwa kuliwa na watu wengi sana ulilmwenguni, china, ulaya mshariki, ulaya magharibi, marekani, latino, afrika, gosh,
nchi ya misri naongoza kwa export ya kitmoto afrika nzima,sasa kama watu wote hawa hawajadhurika kuna haja gani ya kujengeana hofu.
fu*k fear
 
Kwa hiyo aliharamisha kwa sababu ya HUENDA TUTAPATA KIFAFA...???

Tukilumbana na Waislam hakuna kuelewana ..Ila sisi Tunagonga tu.....
Sigara ni Makruh Na sura Tulbakra inasema..Lakini watu wanagonga..
Ila Mambo yetu Halali Tuachieni wenyewe...

[h=3]Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia unajisi; kwa sababu hakimuingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote. (Marko 7:18)[/h][h=3]Pia[/h][h=3]Matendo 10:9-16 “Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana, akaumwa na njaa sana, akataka kula lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia, akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi, ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watatambaao, na ndege wa angani, Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule. Lakini Petro akasema, Hasha Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi. Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi, Jambo hili likatendeka mara tatu, kisha kile chomo kikapokewa tena mbinguni“[/h]
 
kutokana na takwimu ulimwenguni nyama ya kitimoto ndio nyama inayoongoza kuliwa ulimwenguni kuliko aina nyingine ya nyama yaani kuliko kuku,samaki, dagaaa,bata, mbuzi,kondoo, ngombe,sungura, nyani, mbwa, n.k. kitimoto inaongoza kwa kuliwa na watu wengi sana ulilmwenguni, china, ulaya mshariki, ulaya magharibi, marekani, latino, afrika, gosh,
nchi ya misri naongoza kwa export ya kitmoto afrika nzima,sasa kama watu wote hawa hawajadhurika kuna haja gani ya kujengeana hofu.
fu*k fear

Egypt is the main expoter of pork? You are not serious, bossman!
Source?
 
Egypt is the main expoter of pork? You are not serious, bossman!
Source?
100% correct
Most Egyptian pig farmers are Coptic Christians, a group that makes up about 10 percent of the 80 million people in the mostly Muslim nation. Coptic Christians do not observe the Muslim ban on eating pork, and historically they have coexisted peacefully with the Muslim majority in Egypt. The farmers also work in the garbage industry and use their daily collections to feed their herds, which number about 300,000 animals in the country.
 
Mimi sishauri watu wasile kitimoto, mwenyewe nakula. Ila mazingira ya kukiandaa ndo yawe vizuri hasa hapa bongo ambapo ufugaji wake wa wengi haufuati kanuni. Mfano kutibu minyoo angalau kila baada ya miezi 3 na ufugaji wa ndani kutaja kasoro chache.
 
Acha kutisha watu Mzizimkavu hii haijagunduliwa leo hii ni kampeni ya waislam ili wakristo tusile nyama tamu. Haya si mapya yalikuwepo tangu karne za zamani sana. Mimi nimesoma medicine nimeyakuta hivyo, kwa taarifa jamii ya minyoo hiyo pia inapatikana kwa ngombe pia ingawa seriousness yake ni tofauti. Cha kushauri hapa watu waache kula nyama za kuchoma ila zichemke kwa nguvu kabisa. Kula nyama choma ya mifugo wote inakuweka rehani kupata magonjwa ya waliyonayo wanyama husika kama brucelosis, cystesocosis, hydatidosis, toxoplasmosis nk
 
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Nyama ya nguruwe.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao
nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.

Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za
baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu.

Kwa mujibu wa Profesa Lekule,
baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao.

Lekule

Kwenye red tafiti inaonyesha conditions zinazopelekea hatari ya ugonjwa, otherwise hiyo kitu ni very safe, nutritious and delicious
 
100% correct
Most Egyptian pig farmers are Coptic Christians, a group that makes up about 10 percent of the 80 million people in the mostly Muslim nation. Coptic Christians do not observe the Muslim ban on eating pork, and historically they have coexisted peacefully with the Muslim majority in Egypt. The farmers also work in the garbage industry and use their daily collections to feed their herds, which number about 300,000 animals in the country.

Source please!
 
Bahati nzuri hawajataja Arusha - moshi. Co vibaya wa2 wakitumia mdudu wa kanda ya kaskazini.
 
Kwa wale watu wabishi kuleni tu nyama ya nguruwe mukiumwa ugonjwa wa kifafa mimi nipo na nina dawa

ya kutibu hayo maradhi ya kifafa kwa pesa za ki-tanzania ni shillingi millioni 2 kuleni nyama mukiumwa

munitafute mimi kwa gharama za hizo pesa nitawatibuni.
 
Acha kutisha watu Mzizimkavu hii haijagunduliwa leo hii ni kampeni ya waislam ili wakristo tusile nyama tamu. Haya si mapya yalikuwepo tangu karne za zamani sana. Mimi nimesoma medicine nimeyakuta hivyo, kwa taarifa jamii ya minyoo hiyo pia inapatikana kwa ngombe pia ingawa seriousness yake ni tofauti. Cha kushauri hapa watu waache kula nyama za kuchoma ila zichemke kwa nguvu kabisa. Kula nyama choma ya mifugo wote inakuweka rehani kupata magonjwa ya waliyonayo wanyama husika kama brucelosis, cystesocosis, hydatidosis, toxoplasmosis nk
even anthraX
 
kwa ng'ombe yupo mnyoo anaitwa Tinea Sagnata, Nguruwe tinea solium, samaki D. latum, Mbwa na paka toxoplasomisis, ngombe, mbuzi kondoo Brucelosis.
wanyama wengi tu wanaishi na minyoo tofauti tofauti na ambayo inaweza sababisha magonjwa mbalimbali kwa binadamu. Kwa hiyo Mzizimkavu usifikiri kuacha kula nyama ya nguruwe bas utakuwa salama, hata ukila samki unaweza pata minyoo mingi tu. kikubwa tuzingatie taratibu za kiafya.
 
Kwa wale watu wabishi kuleni tu nyama ya nguruwe mukiumwa ugonjwa wa kifafa mimi nipo na nina dawa

ya kutibu hayo maradhi ya kifafa kwa pesa za ki-tanzania ni shillingi millioni 2 kuleni nyama mukiumwa

munitafute mimi kwa gharama za hizo pesa nitawatibuni.

Mkuu very soon hiyo hospital yako itazidiwa na wagonjwa wa hicho kifafa
 
Mkuu very soon hiyo hospital yako itazidiwa na wagonjwa wa hicho kifafa
Siyo tu Hospitali bali hata Hospitali za serikali zitakuwa na wagonjwa wengi wa kifafa möuda sio mrefu kuanzia sasaa


WALAJI WA NGURUWE KUPATA KIFAFA




CHUO Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa.Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini

kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.Akizungumza na gazeti hili

hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo

wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa

wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya

vipimo.“Majibu ya sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii. “Lazima jitihada za makusudi

zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na Serikali,” alisema Profesa Lekule.Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya nguruwe yanatokana na tabia za baadhi

ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha kujitafutia chakula na maji mitaani na kula kinyesi cha binadamu.Kwa mujibu wa Profesa Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia

vichakani na kuwaacha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao.Baada ya kula kinyesi minyoo

humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri, minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.Alisema athari za

kuenea kwa maambuziki hayo inaweza kutokea katika miji mikubwa ikiwamo Dar es Salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo.“Hatua hii inaweza kusababisha

kusambaa kwa ugonjwa huu, hivyo ushirikiano kati ya wafugaji, wafanyabiashara, Serikali na wataalamu wa afya katika kufikia hatua ya kumaliza changamoto hii unahitajika,” alibainisha

Profesa Lekule.
(Kwa hisani ya Venance Gilbert at Thursday, December 26, 20130)

UFUGAJI BORA WA NGURUWE
Nguruwe ni mnyama mwenye faida, ni rafiki kwa mazingira na hahitaji gharama kubwa

“Ufugaji wa Nguruwe ni lazima uwe wa kisasa ili kupata mazao bora. Unaweza kupata kila unachohitaji wewe, familia na hata ndugu zako kutokana na ufugaji wa nguruwe”, anasema Bwana

Lomaiyani Molel kutoka Arusha. Jamii nyingi hapa Tanzania huchukulia nguruwe kama mnyama mchafu na asiyefaa kuwa karibu naye na hata kwa matumizi kama lishe. Zaidi, nyama yake

inapendwa na haina madhara kwa afya na inapendekezwa kuliwa zaidi kuliko nyama nyekundu. Unaweza kuanzisha mradi wa nguruwe kwa gharama ndogo lakini baada ya kipindi cha miezi tisa tu ukaanza kujipatia kipato kutokana na ufugaji huo.

Ufugaji

Kwa kawaida nguruwe wanafugwa na watu wa kada zote, wafugaji wadogo wadogo na hata wakubwa. Aina hii ya ufugaji huweza kumpatia mkulima kipato pamoja na lishe kwa familia, na hauhitaji gharama kubwa.

Banda

Nguruwe wanahitaji kuwa na banda lililojengwa kwa vifaa nafuu. Unaweza kutumia mchanga na simenti kuweka sakafu, ama ukatumia udongo wa mfinyanzi kwa ajili ya kuweka sakafu. Ukubwa wa banda unategemeana na idadi ya nguruwe unaotaka kufuga. Mita 3 kwa mita 2.5 zitawaweka guruwe 8-10 wanaonenepeshwa kwa soko au nguruwe jike mmoja na nguruwe ndume mmoja.

Malisho

Ulishaji wa nguruwe ni rahisi kwa kuwa wanakula aina mbalimbali za vyakula kulingana na mazingira wanayofugwa. Unaweza kuwalisha kwa kutumia majani laini ya aina mbalimbali, na pia hulishwa kwa kutumia masalia ya nafaka (pumba). Unaweza kuwalisha kwa kutumia mashudu au pumba aina ya Wheat Poland. Pia unaweza kuwalisha kwa kutumia mabaki ya jikoni.

Kuzaliana

Nguruwe hubeba mimba kwa kipindi cha siku 114, ambazo hugawanyika kwa miezi 3, wiki 3 na siku 3. Nguruwe mmoja ana uwezo wa kuzaa watoto 6 hadi 14 kwa mara moja. Watoto wa nguruwe (piglets) huanza kula chakula cha kawaida wanapofika umri wa mwezi mmoja na nusu mpaka miezi miwili. Endapo nguruwe watapata matunzo mazuri, baada ya miezi 8 wanakuwa na uzito kati ya kilo 50-70 na wanaweza kuuzwa.

Matunzo

Baada ya nguruwe kuzaa anatakiwa kupatiwa chakula cha kutosha na cha kutia nguvu ili kupata maziwa ya kutosha kwa ajili ya watoto wake. Watoto wa nguruwe wachomwe sindano ya madini ya chuma (Iron injection) baada ya siku moja au mbili toka kuzaliwa. Hii ni muhimu sana vinginevyo wanaweza kufa wote. Kata meno (tooth clipping) baada ya miezi mitatu. Unaweza kuhasi madume (castration) baada ya miezi miwili.

Magonjwa yanayoathiri nguruwe

Kuna aina nyingi za magonjwa yanayoshambulia nguruwe, lakini yapo yale yaliyozoeleka ambapo ni lazima kukabiliana nayo ili kuwa na ufugaji wenye tija.

Ugonjwa wa miguu na midomo

Ugonjwa huu huathiri nguruwe sehemu za miguu na midomo. Ni ugonjwa ambao hushambulia nguruwe mara kwa mara hasa wasipokuwa na matunzo mazuri. Ugonjwa wa miguu na midomo, hudhoofisha nguruwe kwa haraka sana, ikiwa ni pamoja na kupungua uzito.

Chanjo: Chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa midomo na miguu (FMD vaccine) hutolewa kila baada ya mwaka mmoja. Hii inasaidia kuwaweka nguruwe wako katika hali nzuri zaidi bila kushambuliwa na magonjwa hayo.

Tiba: Ugonjwa huu hauna tiba halisi. Inapotokea nguruwe wakawa wameshambuliwa kinachofanyika ni kutibu magonjwa nyemelezi kwa kutumia antibiotics.

Homa ya Nguruwe (Swine fever)


Virusi vinavyosababisha ugonjwa wahoma ya nguruwe huenea kwa harakasana miongoni mwa makundi yanguruwe, na huua kwa haraka sana,lakini hauna madhara kwa binadamuna hauambukizwi kwa binadamu.Nguruwe walioambukizwa waanshikwana vindonda ama mapunyekwenye ngozi. Pia masikio na ngozihuwa mekundu.


Chanjo: Ugonjwa huu hauna chanjo wala tiba. Kinachofanyika mlipuko unapotokea ili kuwa salama ni kuwateketeza nguruwe wote walioathirika na kuanza upya. Unaweza kuteketeza kwa kuwachoma moto.


Muhimu: Baada ya kuwateketeza nguruwe wagonjwa, safisha banda kisha nyunyiza dawa aiana ya Acon au Ectomin, na uache banda wazi kwa kipindi cha wiki moja kabla ya kuweka nguruwe wengine.

Ugonjwa wa mapafu (Pneumonia)

Huu ni ugonjwa unaoshambulia sehemu za koo na mapafu ya nguruwe, ambapo husababisha kukohoa na kupumua kwa shida. Ugonjwa huu husababishwa na bacteria (Secondary bacterial), joto kupita kiasi, vumbi na gesi inayotokana na madawa makali.

Tiba: Homa ya mapafu kwa nguruwe inatibika kwa kutumia antibiotics. Pamoja na kuwaweka wanyama sehemu safi, isiyo na baridi kali au joto la kupitiliza kiwango.

Kimeta (Anthrax)

Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria wanaojulikana kama Bacillus anthracis, wadudu hawa wanabaki kuwa hai kwa muda mrefu na wanaweza kuwa kwenye udongo wakiwa hai kwa kipindi cha miaka mingi.

Chanjo: Chanja nguruwe wako dhidi ya kimeta kama utakavyoelekezwa na wataalamu wa mifugo walio karibu nawe.

Tiba: Unaweza kutibu nguruwe wako kwa kutumia dawa aina ya Penisilin au Oxytetracycline.

Muhimu: Homa ya nguruwe ni lazima iwekewe karatini kwa sababu husambaa kwa haraka sana. Nchini Tanzania mlipuko wa homa ya nguruwe umekuwa ukitokea mara kwa mara maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Malawi na katika mkoa wa Mbeya.

Ushauri: Kwa ushauri zaidi juu ya ufugaji wa Nguruwe na magonjwa ya wanyama, unaweza kuwasiliana na Mtaalamu wa mifugo Bwana Oletikoishi Wawaa, simu 0754 207 987.



Chanzo. MNYALUKOLO: WALAJI WA NGURUWE KUPATA KIFAFA
 
Back
Top Bottom