Habari mbaya: Uwanja wa Uhuru Dar, Watu 45 wapoteza maisha kutoka na msongamano

Habari mbaya: Uwanja wa Uhuru Dar, Watu 45 wapoteza maisha kutoka na msongamano

Watu 45 ni wengi sana, da! inasikitisha sana na kuumiza. Hivi mtu na akili zako watoto mnawapeleka kuaga ili iweje?
na baada ya muda mfupi tutashuhudia tena maambukiza na vifo vingi vya 'kushindwa kupumua'
 
Polisi temeke ipi wame report?
Taarifa inazunguka mitandaoni.
Hata hivyo, nje ya taarifa za polisi, watu waliofiwa na ndugu zao wamewataja kwa majina na mipango ya mazishi inajadiliwa kwenye groups mbalimbali. Hakuna siri.
 
Nitakufa kwa sababu nyingine ila siyo hii ya kizembe ya kwenda kumshangaa marehemu au ile ya Mwamposa ya kukanyaga "maji/mafuta" ya upako!!

Pole kwa wafiwa. Ila uwezi jua, labda siku zao na wenyewe zilishafika. Ngoja tusubirie vifo vingine leo huko Dodoma, baadae Zanzibar, Mwanza na Chato! Serikali si inafurahia kuionesha dunia ya kwamba marehemu alikuwa ni kipenzi cha wanyonge?
 
Tusiposhuhudia itakuwaje?

Mlisema hivyo kwa Maalim kiko wapi?
 
Hapo Dodoma, watu kibao wanafanya kazi ya askari jeshi iwe ngumu zaidi, si wakae tu pembezoni mwa barabara ya nini kufuata msafara nyuma? Huku kwetu iwe ivyo basi fimbo zitacheza sana kwa raia, sio fresh ivyo ata heshima apewe anga
 
Waliokuwa wanahusika na zoezi zima la usimamizi na taratibu za kuaga mwili yapaswa washitakiwe kwa maafa yaliyotokea.
Na mtu mwenye akili na utashi ushaona hali ni tete uwezekano wa kutekeleza kilichokupeleka pale haupo, kwanini ung'ang'ane kuscrumble utoke mijasho kwa lipi hasa?
 
Nyumbu kwa Sasa wanageuza mada ili kuuaminisha umma JPM hakufanya chochote na kinachoendelea eti Ni maigizo,Hivi nyote nyinyi mnaishi ubelgiji Kama lisuu kiasi mnaletewa taarifa?hamuoni?
 
Naona umeandika huku unacheka mpaka mdomo umefunguka mpaka sikioni...
Mpe taarifa hizi binti wa sarungi pia...
Wewe mataga hebu jitahidi muhuzunike kwa staha.

Ndiyo huzuni gani huu mpaka mnavunja uzio airport mnakimbiza ndege hadi kwenye run away ??
 
Aliyeyasababisha yote haya na yeye Karma imejibu huko Dodoma

GracefulDirectIzuthrush-max-14mb.gif
 
Watu 45 ni wengi sana, da! inasikitisha sana na kuumiza. Hivi mtu na akili zako watoto mnawapeleka kuaga ili iweje?
na baada ya muda mfupi tutashuhudia tena maambukiza na vifo vingi vya 'kushindwa kupumua'
[3/21, 19:04] Rco Temeke.: AFANDE DCI,N/DCI,ZCO ,RPC,OP.OFFICER.

Hali ya uhalifu mkoa wa temeke kwa saa 12, zilizopita leo tarehe 21.03.2021 . Tukio kubwa lililoripotiwa ni taarifa ya vifo vikivyotokea uhuru stadium-cha/rb/2267/2021 na kusababisha majeruhi kadhaa.


Aidha maombolezo ya hayati dr.John pombe magufuli na shughuli za kuaga mwili zimekamilika katika uwanja wa uhuru . Mwili uliondolewa na kuelekea uwanja wa ndege wa julias nyerere ta yari kwa safari ya kuelekea dodoma .Watu ni wengi lakini pamoja na ulinzi na usalama kuiimarishwa kila kona ,na vyombo vyote vya ulinzi na usalama,bado kumejitokeza vifo vilivyosababishwa na msongamano na kukanyagana .

Wamekufa watu 45, kati yao wanaume 11,ambapo miongoni mwao kuna watu wazima 6 na watoto 5 .Aidha wanawake ni 34 ambapo kati yao watoto 2 na watu wazima 32 .Majeruhi kwa kukanyagana na kukandamizana na wanaendelea na matibabu ni 32 ambapo 6 wamepelekwa hospitali ya muhimbili kwa matibabu zaidi .Taarifa kwa kirefu mbioni na uchunguzi zaidi unaendelea.

Naomba kuwasilisha .

[3/21, 19:04] rco temeke.: afande wenzetu wa dodoma,zanzibar, mwanza na geita wachukue hadhari mapema wenye mapenzi kwa hayati ni weengiiii sana na wanalazimisha kuuaga mwili wote .Wajadiliane mbinu bora ya kudhibiti umati kwenye msiba huu mzito kwa nchi .Toka rco temeke.
 
Uwanja wa uhuru ulivyo mdogo lazima hayo yatokee
 
Yameshatokea.
Ila sisi watu wa mitandaoni ndo chanzo.
Yote hii imetokea sababu ya yale maneno.
MAREHEMU HAKUWA NA WATU KWENYE MSIBA WAKE.
mwisho wa siku serikali ikaamua kuachia watu kiasi hicho.
Inafaa jeshi la polisi waweke mikakati dhabiti kuzuia watu kufanya yao. Hio ndio kazi yao, mpeeni heshima huyo mzee jamani
 
Back
Top Bottom