Habari Ndiyo Hii; Hata Viongozi wa Dini Hampo Salama.

Habari Ndiyo Hii; Hata Viongozi wa Dini Hampo Salama.

TODAYS

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
14,747
Reaction score
24,250
Amani kwako mdau.

Viongozi wa madhehebu mmekaa kimya kama waumini/ kondoo wa mazizi yenu wamekamilika.

Hali siyo nzuri, mnapaswa kupiga mwangwi kupitia madhabau, hii hali ya utekaji inayoota mizizi nchini kisa tu mwananchi anaongea/ kuandika kuhusu serikali.

Mtume Issa bin Mariam, Yesu Kristo hakutaka kumpoteza hata mmoja, sasa leo mmekuwa wapole na wanyenyekevu huku mnaona hali hairidhishi.

Sheikh, Mufti, Kasisi, Mchungaji, Baba Askofu na nyie mnajiita eti manabii, nini jukumu lenu hapa duniani?

Wakati nyie mnatuhubilia kwamba siku ya mwisho tutahukumiwa kwa kutenda maovu, nanyi mjiandae na moto wa milele kwa kuwaacha kondoo wa mazizi yenu wakiuliwa na kuchinjwa pasipo kupiga mwangwi.
 
Naunga mkono hoja.Mahubiri yasiishie kwenye kusaka sadaka tuu bali kupata sauti kwa yanayolitesa taifa.
 
Wachungaji CCM ktk vitu km hv wao wapo busy makanisan kumsifia mama Ili wasifukuzu nchi ...
 
Viongozi wengi wa dini ni wanafiki wanachojali ni sadaka na masilahi yao.
 
Back
Top Bottom