Habari Njema: Tiba Lishe Ya NIMRI Yaanza Kufanya Maajabu Katika Kuwaponya Wagonjwa wa Covid 19

Habari Njema: Tiba Lishe Ya NIMRI Yaanza Kufanya Maajabu Katika Kuwaponya Wagonjwa wa Covid 19

bizplan

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2013
Posts
592
Reaction score
574
Hatimaye watafiti wetu wa tiba mbadala wameanza kupata matokeo chanya katika kuwatibu wagonjwa wa Korona.

Kumbe walikuwa katika utafiti kwa muda mrefu tu wakitafiti dawa ya HIV. Na sasa lilipokuja hili la korona wamefanya maboresho wanayoyajua wao. Hatimaye matokeo mazuri yamepatikana.

Pengine sio wao tu, wote tumesikia yule mbunge wa Lushoto akieleza pia kuhusu dawa yake, pia yule profesa wa NIMRI naye bila shaka itakuwa ni independent project yake (Labda).

Jambo la msingi ni kuwa, yawezekana siku chache zijazo mataifa ya dunia watakuja Tanzania kupata dawa ya korona ambayo matokeo yake ni ndani ya masaa tu kadhaa mtu amepona.

Nisiseme maneno mengi, soma mwenyewe.

Credit: Michuzi Blog.

Dawa ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) yatoa mwanga wa matumaini kwa wagonjwa wa corona
 
Hajahahahahah.........unadhani pilipili kali ya NIMRI inaweza kufunika Madagascar?! Achana na story za vijiweni za akina Profesa Mgaya; Professor wa aquatic science now to Corona! Dunia inaenda kasi sana.
 
Zikfanya kazi tuanze ku export kuuza Marekani ambako ndugu zetu wana athirika sana.
 
Ata kama unalipwa kusifu na kuimba mapambio, siyo kwa kupitia Covid 19 utahadhirika
Kabisa......corona ni facts, siyo sehemu ya kutafuta kiki za kiwango cha akina gigymone. Ni maji marefu; dunia ya kwanza inatumia detailed science lkn bilabila leo lijitu litokee kwa mtogole/ilala boma huko ati sijui mchanganyiko gani unaponya virus? No. Not that extent. Mtupe breake sasa!
 
watu kama nyie mnaotumika na mabeberu mnakera sana ,adhabu yenu ni kupigwa risasi au kutekwa?kwani kuna corona Tanzania? imegundulika watu wa maabara walikuwa wanatumika na mabebeu ndiyo maana ikafungwa,hata hivyo vifo 16 ni magonjwa mengine labda wqapeleke nchi nyingine zilizoshindwa kudhibiti corona hadi kwa uoga na uzembe wao wakaweka lockdown,sisi tuko poa kabisa, PIGA KAZI MWANAUME ALIYEKAMILIKA HAOGOPI CORONA
hata kwa hatua ndogo kama hii kuna watu watachukia.kuna watu wanatoho mbaya sana hi tanzania yetu,alafu hawafagi haraka sijui kwa nini ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaobisha waendelee kubisha ila hii dawa ni genuine hata kama huna covid vifua mafua clearity ya mapafu inafanya vizuri kwa kweli, hata ukigoogle item moja moja utagundua ni nzuri! Mwenye sikio na afahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona sasa hivi nchi za Afrika zinaanza kulazimika kuwekeza katika sayansi, tafiti na technologia. Mungu zidisha majanga kama haya ili tuamke zaidi!
 
Hii habari uliyosema tukasome ndiyo imeandikwa hivyo!!

Nami pia nimesema ni tiba lishe. Ila pia yawezekana hujasoma yote na uliamua kutafuta 'makosa' tu.

Ukisoma hadi mwisho wanasema watu wanapona na mahitaji yameongezeka.

Mwenye kuelewa aelewe na anayebisha abishe.
 
Back
Top Bottom