Habari Njema: Tiba Lishe Ya NIMRI Yaanza Kufanya Maajabu Katika Kuwaponya Wagonjwa wa Covid 19

Habari Njema: Tiba Lishe Ya NIMRI Yaanza Kufanya Maajabu Katika Kuwaponya Wagonjwa wa Covid 19

Naona sasa hivi nchi za Afrika zinaanza kulazimika kuwekeza katika sayansi, tafiti na technologia. Mungu zidisha majanga kama haya ili tuamke zaidi!

Imagine walikuwa wanafanya utafiti muda mrefu. Yawezekana hata fund hawakuwa nayo.

Lakini baada ya serikali kuwapa changamoto kidogo haya ndiyo matokeo yake.

Kuna muda huwa nasema Tanzania ni miongoni mwa nchi nzuri sana duniani iliyobarikiwa na kila kitu, sijuiutunakwamaga wapi.
 
Kabisa......corona ni facts, siyo sehemu ya kutafuta kiki za kiwango cha akina gigymone. Ni maji marefu; dunia ya kwanza inatumia detailed science lkn bilabila leo lijitu litokee kwa mtogole/ilala boma huko ati sijui mchanganyiko gani unaponya virus? No. Not that extent. Mtupe breake sasa!

Dunia ni nini na Kwamtogole ni wapi? Detailed science inatumia malighafi gani? Ninadhani tunahitaji la mindset transformation.
 
Dunia ni nini na Kwamtogole ni wapi? Detailed science inatumia malighafi gani? Ninadhani tunahitaji la mindset transformation.

Kuna watanzania wana mawazo ya kipumbavu sana. Yaani dawa au tiba lishe kugunduliwa Tanzania kwao ni shida sana sana sana.

Sijui tatizo ni nini.
 
Hongera NIMRI mi naamini Corona ni mdudu dhaifu sana, hana ubavu kwa binadamu anayeishi kwa kula vyakula asili vyenye virutubisho kwa muda mrefu, Ulaya wameathirika sana kwa kuwa Hawana vyakula vya asili vya kutisha kama Afrika hasa Afrika kusini mwa jangwa la Sahara ukiondoa Afrika ya kusini, Naamini Dawa ya Corona itapatikana Afrika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Michuzi blog hawajawahi toa taarifa nikaikubali, tena taarifa nyeti namna hii. Ni sawa na nilivyoamua kutoiamini CNN tokea uchaguzi mkuu alipochaguliwa Trump, wao walikuwa wanatoa taarifa za kumdogosha. Tangu kipindi kile nikaamini wale jamaa makanjanja. Mwaka huu nikajaribu niwaamini kwenye issue ya Kim lakini nikajishtukia, na ni kweli walikuwa waongo.
Yani mimi ukishanidanganya waziwazi, ni vigumu sana nitumie tena taarifa zako.
 
Ukisoma hadi mwisho wanasema watu wanapona na mahitaji yameongezeka.
Na hiyo pia nimesoma lakini haiko kisayansi kabisa.

Kisayansi unatoa idadi ya uliowapa dawa kwa kuelezea Umri wao, jinsi yao na ni wangapi wamepona na wangapi hawapona na kama umewafuatilia kwa muda gani. Pia kwa kuwa ugonjwa huu unawaathiri zaidi wenye kinga dhaifu ni vema pia ukasema nao pia wamesaidiwaje na hizo sawa. Watu wenye Kisukari, UKIMWI, TB na mengineo matokeo yalikuwaje walipopewa hiyo dawa.

Maana kwa wenzetu wanaopona pia wanafuatiliwa kwa sababu imeonekana inawezekana mgonjwa wa COVID - 19 kurudiwa tena na ugonjwa.
 
Kwa nchi za kiafrika hii kauli hapo chino siyo hoja sana mdau.
Angalia waziri wa afya ile nafasi yake (kulingana na professional) ni sahihi?, tunaangalia utendaji na mafanikio yako na ndiyo maana hakuna chuo cha kusomea URAIS.
Professor wa aquatic science now to Corona! Dunia inaenda kasi sana.
 
Nami pia nimesema ni tiba lishe. Ila pia yawezekana hujasoma yote na uliamua kutafuta 'makosa' tu.

Ukisoma hadi mwisho wanasema watu wanapona na mahitaji yameongezeka.

Mwenye kuelewa aelewe na anayebisha abishe.
Aliekuelewa amekuelewa asietaka mwache
 
Hatimaye watafiti wetu wa tiba mbadala wameanza kupata matokeo chanya katika kuwatibu wagonjwa wa Korona.

Kumbe walikuwa katika utafiti kwa muda mrefu tu wakitafiti dawa ya HIV. Na sasa lilipokuja hili la korona wamefanya maboresho wanayoyajua wao. Hatimaye matokeo mazuri yamepatikana.

Pengine sio wao tu, wote tumesikia yule mbunge wa Lushoto akieleza pia kuhusu dawa yake, pia yule profesa wa NIMRI naye bila shaka itakuwa ni independent project yake (Labda).

Jambo la msingi ni kuwa, yawezekana siku chache zijazo mataifa ya dunia watakuja Tanzania kupata dawa ya korona ambayo matokeo yake ni ndani ya masaa tu kadhaa mtu amepona.

Nisiseme maneno mengi, soma mwenyewe.

Credit: Michuzi Blog.

Dawa ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) yatoa mwanga wa matumaini kwa wagonjwa wa corona
Wagonjwa wapi si wameshapona wote ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom