Eng. Japhet Matarra ni kada kindakindaki wa CHADEMA ambaye kwa sasa yuko gerezani Karanga Moshi kwa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuhukumiwa kwa kufanya makosa ya mtandaoni. Ilikuwa aende jela au alipe faini ya Tsh 7m ila kwa bahati mbaya huyu kijana hakuwa na hizo pesa ikambidi aende jela. Ninapoandika uzi huu ndo wanaharakati wa kisiasa huko X wanachangishana Tsh 7m ili kulipa faini na kumtoa kijana jela.
Kupitia post ya Twaha Mwaipaya, kijana Matara amedai kwa mwaka mzima aliokuwa gerezani hakuna mtu aliyewahi kumtembelea wakiwemo wanaCHADEMA wenzake. Nimeshangaa pia hata mkewe hakwenda baada ya kusoma bio yake inayoonyesha kuwa Matara alishaoa kabla ya kwenda jela.
Suala la CHADEMA kumpuuzia mwanachama wake aliyehitaji Tsh 7m tu linafikirisha sana. Kama wanaweza kuhamasishana kuchanga ili kununua gari la kifahari la Lissu inakuwaje wanashindwa kumkumbuka kijana wao anayesota gerezani hadi wanaharakati wa X wajitokeze?
CHADEMA ijitathmini. Pia liwe fundisho kwa vijana wengine wanaofikiri CHADEMA itawasaidia wakati wa shida.
View attachment 3030483
View attachment 3030484