Wazo lako zuri lakini zingatia haya ili uwe na ushawishi kwa kampuni/mwekezaji wa mradi wako
1. Eneo la hostel
Nimepitia majibu yako unasema unataka iwe Sinza. Sababu zipi zimefanya uamue Sinza na si sehemu nyingine kama Mwenge, Kijitonyama nk?
2. Huduma
Katika eneo hilo utakalo kujenga unatarajia kuweka huduma zipi zilizo rahisi kwa wateja/wanafunzi ambazo ni bora na za kipekee kiasi cha kufanya kila awazae hostel basi aje kwako
3. Urahisi wa usafiri
Asili ya wapangaji wengi hupenda kutumia basi moja kutoka anapokaa hadi mahala pa kazi/masomo. Je hili kwa eneo lako linawezekana au una ushawishi gani wenye mabasi kuja kuqnzisha huduma ya mabasi ya kwenda chuo/ mjini kutokea kwako
4. Kodi ya pango
Maeneo yanayozunguka Sinza na karibu na Sinza na Sinza yenyewe kumejaa utitiri wa hostel na nyumba za kupanga. Je kodi yako ushaifanyia upembuzi yakinifu kuwa ipo chini na itaweza kukidhi kugharamia huduma zote za kijamii na za ziada
5. Utulivu
Mtu anaesoma anapenda mazingira yaliyotulivu na hakuna kelele. Sinza kwa hili bado ni changamoto. Umeliona hili?
6. Mtaji za uwekezaji
Mradi huu naamini unaweza kuwa rahisi kwako kutekelezeka kama nawe ungekuwa na mtaji. Mtaji huu unajumuisha pesa kiasi au hata kiwanja kikubwa na kipo katika eneo 'potential' ss angalia hili
7. Mwisho
Mawazo yako mazuri yaandike na uanze kutengeneza mipango na shirikisha wadau wewe uwe na shea kiasi tu
Nawasilisha
Sent using
Jamii Forums mobile app