Habari za Mauza uza ya porini niulize mimi

Habari za Mauza uza ya porini niulize mimi

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
2,489
Reaction score
5,764
Mwaka flani nikiwa sekondari likizo nlienda kwa babu.babu yangu ni mwindaji miaka mingi sana.anafahamika kijijini. Na zaidi zaidi ni mpenzi wa nyama ile mbaya. Huwa hatumii maharage hata kwa shida. Yeye ni nyama na anajua namna ya kuitunza hata mwezi akaila.

Nlikuwa form four mzee alinambia nisirudi home nikae na babu huko kijijini. Basi siku moja babu akanambia twende porini kuwinda.sababu nami nlikuwa napenda akachukua bunduki yake akanipa kamkoba flani kana risasi na vitu vitu vingine.

Siku hiyo ilikuwa asubuhi. Tulitembea sana kuingia kwenye pori kubwa sana...baada ya kuacha gari sehemu flani tukaingia porini huko mwendo wa masaa mawili.

Tukafika sehemu flani nikaona nyumba nikamwambia babu nimechoka aniache pale nipumzike. Babu alinitizama kwa macho makali akanambia nisioneshee kidole hiyo nyumba nimtizame yeye.sikumwelewa.tukaendelea mbele kufika sehemu moja ina mto.akanambia tulale chini tusubiri pale kweli.kama dk 40 hivi tukaona dikdik wanne wanakunywa maji.

Babu akalenga na kuachia mashine....risasi ikatoka kwa mlio mkubwa pamoja na kuwa alikuwa amenambia nizibe masikio nlipatwa ganzi masikioni.

Tulisikia kilioa cha yule dikdik akarushwa pemben akajinyoosha.babu akatulia kidogo.then akainuka kueleka alipo yule dikdik...nikamwona akiwa amesimama kama dk 10 hiv amejishika kiuno.niliamua kumfuata. Pale tulikuta pasafi hamna damu wala alama ya mnyama kuwepo.

Babu alisonya na kusema tuondoke.tukaondoka mpaka sehemu nyingine hapo babu aliona alama za swala kwa maelezo yake.akanambia nimfuate taratibu....tulienda mbele sana nikawaona swala wawili.nikambonyeza babu kuwa kule mbele kuna swala.akawa hawaoni.nlijaribu mwonesha hawaoni kabisa.baadaye akanambia nimefahamu shida nini turudi.

Tulihangaika sana kurudi home...tulipotea kama mara kumi hivi mpaka saa 8 usiku tupo porini. Babu akashauri tulale kwenye mti mmoja wapo. Akachora kuzunguka ule mti akamwagia unga wa baruti kama sikosei na unga mwingine.tukapanda akanielekeza namna ya kulala.

Nlishtuka mida ya saa tisa hivi nasikia harufu nzuri ya viazi nikadhani naota.mara nikasikia sauti za watu wanacheka sana.babu alikuwa macho ila kanyamaza anajifanya kalala.sikuweza pata usingizi.kesho yake asubuhi babu aliamka tukashuka mtini na hapo haraka akaanza tafuta mti flani.akaupata. akachukua majani akafikicha na kuchanganya na kinyesi cha sijui mnyama gani alizoa njiani.akawasha moto.yakaungua yote akanambia nikanyage.naye akakanyaga... Mengine tukapaka usoni akaniambia nimfuate.

Kweli kama mwendo wa dk 20 tukajikuta pale tulipoacha gari. Tukarudi home. Tulipofika tu babu alitaka nioge naye akaoga akaniita nimfuate baada ya kula tukaenda kwa mzee mmoja.babu alikuwa amebeba panga amelizungushia kitambaa cheusi

Tulifika kwa mzee mmoja pale kijijini.alipotuona akataka kukimbia...babu alimwahi na kumpiga na ubapa wa panga mgongoni yule mzee akaanguka kwa kishindo sana.mimi kuona hivyo nikaanza piga kelele.babu akanitolea macho "nyamaza" akamshika shingoni yule mzee na kumwambia.

"Ukicheza tena na mimi ntakukata kata vipande huyu ni mjukuu wangu ole wako asumbuke au ulete michezo yako tena"

Sikuwa naelewa hasa shida nini.tukarudi home.baada ya siku mbili babu akasema tena twende kuwinda.nlitaka kusita ila nikaona aibu mjukuu wa kiume shababi kuwa mwoga.tukaenda na babu kule kule porini.nakumbuka sehemu flani nlimwona yule mzee tulieenda mpiga biti kwenye kijumba flani kule porini akiwa analima.alipoinua kutuangalia yeye na nyumba sikuviona tena.nlishtuka sana.

Babu hakusema kitu.siku hiyo tulipata swala. Babu alichukua damu ya yule swala na kupaka kwenye bunduki.tukarudi home.

Baada ya week akataka tena twende porini.babu alidhamiria kunifundisha uwindaji.siku hiyo porini nlikutana mauza uza ya hovyo sana.tulikutana na bint mmoja mrembo anavutia sana.amekaa pembeni ya kuni.kiukweli nlishtuka sana...babu akanishika mkono na kunambia nisiseme lolote.kweli tukapita kugeuka sikumwona yule bint.nikashangaa kule porini anatafuta nini.

Basi tukaenda sehemu moja tukakuta ndege kanga.babu alifanikiwa kuua watano.alichukua wanne mmoja akamwacha.nlimwuliza babu why unamwacha huyu.akajibu hawa wanne wanatosha twende.

Kijijini alikuwepo bint mmoja mkali sana huyo nlikuwa nmemweka sawa nikamtafune.alikuwa mzuri sana ...siku hiyo kulikuwa na ngoma usiku nami nlienda na dada wengine nliokuwa nao kijijini na akina bamdogo.mpaka saa mbili tupo ngomani nikawa nmechepuka kwenye kichaka nikamla yule bint.

Usiku ulipoenda tukarudi kulala.sababu ya hali ya ubaridi kiasi flani hata sikuoga.siku hiyo nliota namla demu mmoja wa kitambi naenjoy sana mzigo.kuamka asubuhi nmechoka kinyama.

Kesho yake nikamtafuta tena bint nikamla.nmerudi home around saa kumi babu ananambia twende mtoni.tukaingia kwenye gari take land rover 110 hao kasi mpaka sehemu moja porini kuna mto. Tukaacha gari barabarani tukaanza kuuingia ndani kidogo nikamwona tena yule bint mrembo this time amekasirika sana ananitizama kwa hasira sana.babu akanitizama na kunishika mkono kunivuta pembeni.

Akaniuliza umefanya nini leo au jana.mimi sikuwa naelewa lolote.akanihoji mwishowe akaniuliza hujamlala mwanamke?" Hapo nikajibu ndiyo. Akanitizama akanambia turudi.

Basi tujarudi garini ndo kunambia kama nikimla demu niwe naosha uume maana nmekuja porini nanukua papuchi hadi nmemuudhi yule mtoto wa mfalme.daah nlishindwa kujizuia nikacheka, babu aliniwasha kibao.ndo mara ya kwanza na ya mwisho babu kuniwasha kibao.nikajua ipo serious.

Kumbe yule demu wa porin mrembo ni jini alipenda niwe namgegeda so alichukia sana kuwa nmemgegeda mtu huko kijijini halafu nakuja mringishia harufu ya papuchi.so ali mind kinyama.

Sasa hapo demu yule wa porini akaanza kunifuatilia.


Ntaendelea....
 
Mhhh hyo harufu kali hivyo ya papuchi gani hyo? siku nzima unanukia😬
 
Mkuu huyo binti mrembo naomba namba yake ya simu tafazali
 
Back
Top Bottom