Habari za za Simba kupewa nafasi badala ya Mbeya City

yahoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
3,526
Reaction score
1,409
Kuna habari nimekutana nazo facebook kwamba simba wamepewa nafasi ya kushiriki kagame cup badala ya mbeya city kwa kigezo kwamba wao ni wazoefu...habari hizi sijaziona wala kuzisikia kwenye blog wala redioni.

Mwenye source ya kuaminika naomba atusaidia kudhibitisha
 
TIMU za Yanga, Simba na Azam zilipewa nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Kagame yalipofanyika kwa mara ya mwisho hapa nchini mwaka 2012 kwasababu zilishika nafasi tatu za juu.
Lakini mwaka huu Tanzania ikitarajiwa kuwe mwenyeji, CECAFA wametoa nafasi tatu kwa timu za Tanzania na kwa namna ligi ilivyoisha msimu uliopita, Azam, Yanga na Mbeya City zinatakiwa kushiriki, lakini Mbeya City fc licha ya kushika nafasi ya tatu msimu uliopita imepigwa chini na nafasi yake wamechukua Simba walioshika nafasi ya nne.
Katibu mkuu wa Shirikisho la soka nchini, TFF, Selestine Mwesigwa amesema timu yenye uhalali wa moja kwa moja ni Azam fc, lakini unapokuwa mwenyeji unapewa nafasi mbili nyingine, kwahiyo mshindi wa pili na watatu wanatakiwa kuingia, lakini Mbeya City hawatakuwepo.
"Mbeya City walistahili, lakini niseme ukweli, tumeamua kumchukua Simba, kwanini? kwasababu ya rekodi yake. Amekuwa bingwa mara nyingi wa mashindano haya, kwahiyo ana nafasi yake sio katika Tanzania tu bali ukanda mzima, na huwezi kumuondoa". Amesema Mwesigwa na kuongeza: "Mwaka jana baada ya Azam kujitoa kushiriki mashindano mapya ya kagame, tuliwapa Mbeya City nafasi".
Hata hivyo ukiangalia kwa jicho la ndani, TFF na CECAFA hawawezi kuwanyima Simba kwasababu za kimaslahi.
Yanga na Simba zinaposhiriki michuano yoyote nchini watu wengi wanajitokeza kutazama mpira, hivyo kuziwek

Yanga na Simba zinaposhiriki michuano yoyote nchini watu wengi wanajitokeza kutazama mpira, hivyo kuziweke timu hizi ni kutengeneza namna bora ya kupata mapato.
Bahati nzuri pia hakuna kanuni inayobana kwamba lazima timu tatu za juu zishiriki, nchi mwenyeji inaweza kuchagua timu yoyote kwa vigezo itavyojiwekea
e timu hizi ni kutengeneza namna bora ya kupata mapato.
Bahati nzuri pia hakuna kanuni inayobana kwamba lazima timu tatu za juu zishiriki, nchi mwenyeji inaweza kuchagua timu yoyote kwa vigezo itavyojiwekea

CHANZO> MPENJA BLOG
 
inawezekana ikawa kweli maana tff wanaangalia MAPATO KWANZA halafu mambo mengine baadae...
 
Mtoto halali na Pesa.. analala na Ma...vi

au Mwajuma ndala ndefu mnatuogopa!??
 
sasa hao mbeya city watapata wapi uzoefu wa kimataifa bila kupewa nafasi ya kushiriki kama hizi??
 
Hii ndio shida ya kufanya mambo bila kanuni wala utaratibu. Watu wanaangalia matumbo yao kwanza. CECAFA na TFF lazima wawe na kanuni zinazoeleweka kama CAF.
 
Mm nashauri wazishindanieshe hizi timu Kati ya Mbeya city Vs Simba mshindi aende kucheza Kagame cup
 
Afu tuone kama simba anatoka, pia recod zao Sio hivi wamekutana Mara nne simba kafungwa Mara mbili na sære mbili afu simba hiyohiyo mbovu mnasema ikacheze Kagame how?
 
ni kweli katibu wa tff alivyotamka juzi tukiwambia kombe la bonanza la mosonye maana halina hata kanuni nasikia yanga wamewapa masharti ili washiriki walipwe milioni 30 ndio washiriki
 
Soka la east Africa ni pasua kichwa Yaani kila kitu siasa na usishangae hao simba na yanga wakakutana finally
 
Mikia wanavyoigopa MCC hawawezi kukubali hata kwa mtutu wa bunduki
 
Afu tuone kama simba anatoka, pia recod zao Sio hivi wamekutana Mara nne simba kafungwa Mara mbili na sære mbili afu simba hiyohiyo mbovu mnasema ikacheze Kagame how?
huu ni uonevu wa wazi wazi. duniani kote waliofanya vizuri ndiyo hupewa nafasi. mbeya city inabidi wakate rufaa. simba inabebwa sana na tff, kwanza wamechezesha mchezaji mwenye red na leo wanafanya haya.
 
Haya ni maamuzi muhimu sana kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania kwa maana hata wale waliokuwa hawajajua ni jinsi gani yanafanyika maamuzi ya kijinga kijinga sasa kwa uamuzi huu watajua.
Kama maamuzi yenyewe ni haya basi hakuna haja ya kucheza ligi maana washiriki mnaosema wana uzoefu ndio hawa hawa waliodumaza mpira wa Tanzania!
 
Halafu Tanzania isiposhiriki AFCON,CHAN,WORLD CUP,Tunaanza kutafuta mchawi wakati wachawi wanajulikana.Ni uongozi wa TFF
 
Afu tuone kama simba anatoka, pia recod zao Sio hivi wamekutana Mara nne simba kafungwa Mara mbili na sære mbili afu simba hiyohiyo mbovu mnasema ikacheze Kagame how?

Maslahi tu hapo hamna kingine
Mpira wetu hautafika mbali kwa mambo haya 😡
 
Yani hawa jamaa huwa wanashindwa tu kubadili matokeo ya uwanjani mfano yanga anapofungwa na mgambo Jkt au Simba kufungwa na Mbeya city
 
Mi ni simba Damu ila siungi mkono hii kitu hata kidogo,anayestaili ndo aende! Mbeya City ni nafasi yao na sisi HATISTAHILI, na kubebwa bebwa sababu ya kutumika tuu ajili ya mapato sio kitu kizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…