Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Habari kutoka vyanzo vinavyoaminika zimekuwa zikititirika juu ya ukweli kuhusu zilikoenda zile Trilion 1.5 ambazo zilionekana kama zimeyeyuka hewani, na kutolewa maelezo yasiyoridhisha na serikali.
Habari zilizopo ni kwamba sehemu kubwa ya fedha hizo zilipelekwa katika matumizi ambayo mamlaka toka juu iliamua yasiwekwe wazi, na kikubwa cha matumizi hayo yakiwa ni mambo ya ki intelijensia/usalama. Habari zimezidi kuanisha kwamba kwa mara ya kwanza toka nchi hii ipate uhuru, kumekuwa na matumizi ya kutisha katika idara zote zote za serikali zinazohusiana na mambo ya usalama zaidi sana ya fedha wanazokuwa wakitengewa.
Pia kumekuwa na ajira nyingi zisizofuata utaratibu na kuanzishwa kwa vitengo ndani ya vitengo ambavyo vingi sio rasmi na hivyo matumizi ya fedha za vitengo hivyo hayawezi kuwekwa wazi. Watu wengi wemeajiriwa katika idara hizi zisizo rasmi katika mazingira ya kibinafsi na maagizo kutoka juu badala ya kufuata taratibu rasmi za serikali, na wamekuwa wakitengewa fedha kwa ajili ya "kazi" zao.
Habari zimezidi kudai kwamba hata wakati wa awamu ya Nyerere ambapo kulikuwa na kiwango cha juu cha mambo ya intelijensia na usalama kutokana na Tanzania kuwa kitovu cha mambo ya ukombozi wa nchi za Afrika hatukufikia matumizi ya kiasi hiki. Mbaya zaidi mengi ni matumizi ambayo hayajainishwa na kufuata tarataibu za matumizi ya fedha za serikali, na hayawezi kuhojiwa na mtu yeyote wala kukaguliwa hata na CAG. Habari zimesema kuwa ni kama kwa sasa kuna "obsession" ya mambo ya usalama na intelijensia, na watu wanaotumikia katika sehemu hizi ambazo nyingine sio rasmi wamepewa uhuru wa kutumia fedha wanavyopenda.