Tetesi: Habari zaanza kuvuja kuhusu zilikoenda Trilioni 1.5 "zilizopotea"

Kama hoja ni kulinda amani ya nchi,zitumike tu hata trilioni tatu. Amani ukitoweka gharama zake hazielezeki kwa maneno
 
Ttz la bavicha mkishakaririshwa kitu kuja kuwatoka kichwani hadi aliyewakaririsha awaambie hapana sio hivo.
Hili ndio tatizo lenu kuu mtuu yeyote aliye ana mawazo tofauti na nyie ni mpinzani kaa hivyo hivyo
 
Habari kutoka vyanzo vinavyoaminika zimekuwa zikititirika juu ya ukweli kuhusu zilikoenda zile Trilion 1.5 ambazo zilionekana kama zimeyeyuka hewani, na kutolewa maelezo yasiyoridhisha na serikali.

Habari zilizopo ni kwamba sehemu kubwa ya fedha hizo zilipelekwa katika matumizi ambayo mamlaka toka juu iliamua yasiwekwe wazi, na kikubwa cha matumizi hayo yakiwa ni mambo ya ki intelijensia/usalama. Habari zimezidi kuanisha kwamba kwa mara ya kwanza toka nchi hii ipate uhuru, kumekuwa na matumizi ya kutisha katika idara zote zote za serikali zinazohusiana na mambo ya usalama zaidi sana ya fedha wanazokuwa wakitengewa.

Pia kumekuwa na ajira nyingi zisizofuata utaratibu na kuanzishwa kwa vitengo ndani ya vitengo ambavyo vingi sio rasmi na hivyo matumizi ya fedha za vitengo hivyo hayawezi kuwekwa wazi. Watu wengi wemeajiriwa katika idara hizi zisizo rasmi katika mazingira ya kibinafsi na maagizo kutoka juu badala ya kufuata taratibu rasmi za serikali, na wamekuwa wakitengewa fedha kwa ajili ya "kazi" zao.

Habari zimezidi kudai kwamba hata wakati wa awamu ya Nyerere ambapo kulikuwa na kiwango cha juu cha mambo ya intelijensia na usalama kutokana na Tanzania kuwa kitovu cha mambo ya ukombozi wa nchi za Afrika hatukufikia matumizi ya kiasi hiki. Mbaya zaidi mengi ni matumizi ambayo hayajainishwa na kufuata tarataibu za matumizi ya fedha za serikali, na hayawezi kuhojiwa na mtu yeyote wala kukaguliwa hata na CAG. Habari zimesema kuwa ni kama kwa sasa kuna "obsession" ya mambo ya usalama na intelijensia, na watu wanaotumikia katika sehemu hizi ambazo nyingine sio rasmi wamepewa uhuru wa kutumia fedha wanavyopenda.

Sasa mbona hiyo ni habari nzuri sana kama zimeenda kwenye mambo ya usalama wa nchi?tunahitaji majeshi yetu yawe na vifaa vya kisasa kutulinda,tunahitaji TISS wafanye kazi yao bila ukwasi,tunahitaji jeshi la polisi,magereza,zimamoto na vyombo vyote vya ulinzi na usalama kufanya kazi bila njaa,so kwangu nampongeza sana Rais kwa hilo,
 
  • Kuna genge ndani ya TISS linamdanganya rahisi kwamba kuna njama za kumua zinapangwa na mafisadi hivyo aongezewe ulinzi. Hapo sasa kunawekwa mlolongo wa vifaa na mahitaji mengine ili watu wapige hela. Rais hasafiri nje ya nchi wale mashushu wake watapata wapi hela ya kuhonga ndio wamebuni mbinu hiyo mpya.
  • Msafara wa rais wa wanyonge wa awamu ya Tano una magari mengi tena ya kifahara kuliko msafara wa rais yeyote tokea Tanzania ipate uhuru.
 
Sasa mbona hiyo ni habari nzuri sana kama zimeenda kwenye mambo ya usalama wa nchi?tunahitaji majeshi yetu yawe na vifaa vya kisasa kutulinda,tunahitaji TISS wafanye kazi yao bila ukwasi,tunahitaji jeshi la polisi,magereza,zimamoto na vyombo vyote vya ulinzi na usalama kufanya kazi bila njaa,so kwangu nampongeza sana Rais kwa hilo,
Polisi Magereza na Uhamiaji kuna wapiganaji wamepanda vyeo tokea 2016 hadi sasa mishahara haijapanda...mwambieni mzee huko majeshini hali mbaya
 
nadhani huko watu wanapanda kwendana na level yao ya elimu na cheo,sasa sijaelewa argument yako imebase kwenye kitu gani mkuu
 
Ukizingatia hoja ya mleta mada lazima the same amount itumike next budgetary year..tusubiri na kuona namna hoja hii inavyokosa mashiko..
 
Mh.Jiwe na mwanaye Maliyamungu wana matumizi mengi zaidi ya hao!
Umesahau gharama za kupandikiza mimba ya mke wa Maliyamungu!
Ila uzuri Mzee Jiwe hawezi kupeleka hiyo "change ya 1.5 trliion nje ya Afrika Mashariki zimehamishiwa kwa Wahutu wenzake hapo Kigali!Msalika Robert RAS Tabora anajua zilipo!
 
nadhani huko watu wanapanda kwendana na level yao ya elimu na cheo,sasa sijaelewa argument yako imebase kwenye kitu gani mkuu
Konstebo X mwaka 2016 alikwwenda kozi ya kuwa koplo akamaliza baada ya miezi mitatu na kutunukiwa ukoplo lakini tokea mwaka huo hadi leo anapokea mshahara wa konstebo.. Huo ni mfano wa cheo kimoja na wapo wengi katika majeshi yetu..mwambieni mzee awakumbuke wanapigika. Jeshine elimu haichukui nafasi kubwa kama unavyodhani wewe mwana ccm raia
 
Nikiangalia idadi ya pesa na utumbo wako haviingiliani kabisa,ni mbingu na ardhi,porojo hizi wataelewa mashabiki wako tu,sio ma GT.
Majibu ya naibu waziri wa fedha yalijitosheleza kabisa
Kuna kina mwanahabari huru na zito jr wataipamba hii habari maana sina hakika nini kimetokea katija hichwa vyao
 
Habari kutoka vyanzo vinavyoaminika zimekuwa zikititirika juu ya ukweli kuhusu zilikoenda zile Trilion 1.5 ambazo zilionekana kama zimeyeyuka hewani, na kutolewa maelezo yasiyoridhisha na serikali.

Habari zilizopo ni kwamba sehemu kubwa ya fedha hizo zilipelekwa katika matumizi ambayo mamlaka toka juu iliamua yasiwekwe wazi, na kikubwa cha matumizi hayo yakiwa ni mambo ya ki intelijensia/usalama. Habari zimezidi kuanisha kwamba kwa mara ya kwanza toka nchi hii ipate uhuru, kumekuwa na matumizi ya kutisha katika idara zote zote za serikali zinazohusiana na mambo ya usalama zaidi sana ya fedha wanazokuwa wakitengewa.

Pia kumekuwa na ajira nyingi zisizofuata utaratibu na kuanzishwa kwa vitengo ndani ya vitengo ambavyo vingi sio rasmi na hivyo matumizi ya fedha za vitengo hivyo hayawezi kuwekwa wazi. Watu wengi wemeajiriwa katika idara hizi zisizo rasmi katika mazingira ya kibinafsi na maagizo kutoka juu badala ya kufuata taratibu rasmi za serikali, na wamekuwa wakitengewa fedha kwa ajili ya "kazi" zao.

Habari zimezidi kudai kwamba hata wakati wa awamu ya Nyerere ambapo kulikuwa na kiwango cha juu cha mambo ya intelijensia na usalama kutokana na Tanzania kuwa kitovu cha mambo ya ukombozi wa nchi za Afrika hatukufikia matumizi ya kiasi hiki. Mbaya zaidi mengi ni matumizi ambayo hayajainishwa na kufuata tarataibu za matumizi ya fedha za serikali, na hayawezi kuhojiwa na mtu yeyote wala kukaguliwa hata na CAG. Habari zimesema kuwa ni kama kwa sasa kuna "obsession" ya mambo ya usalama na intelijensia, na watu wanaotumikia katika sehemu hizi ambazo nyingine sio rasmi wamepewa uhuru wa kutumia fedha wanavyopenda.
Kwanini usiseme habari ulizozipata kutoka GOGO VIVU KARIAKOO? The way ulivyoiandika hii habari yako ni kama umezipata habari kijiweni manzese ama Gogo Vivu la mabaharia Kariakoo
 
Back
Top Bottom