Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Habib Halahala alichaguliwa kuwa mwandishi wa habari na mpiga picha wa Rais Nyerere mwishoni mwa utawala wa Rais Nyerere kwenye miaka ya 1980.
Ilipofika mwaka 1985, Mwl Nyerere aling'atuka ofisini kama Rais wa kwanza wa Tanzania mara baada ya takribani miongo miwili na robo madarakani.
Habib Halahala aliendelea na majukumu yake ya uandishi wa habari katika awamu ya pili ya Rais Ali Hassan Mwinyi. Moja ya sifa ya yeye kuendelea ni uchapaji wake kazi mzuri uliomvutia Rais Mwinyi.
Mwanzoni mwa miaka 1990, Nchi ikakumbwa na mafuriko makubwa sana na kusababishaathari kubwa sana kwa wananchi hasa kusini mwa Tanzania.
Ikabidi Rais Mwinyi afanye ziara kuangalia athari hizo huku akitumia ziara hiyo kama sehemu ya kuwafariji wananchi waliokumbwa na kadhia ya mafuriko.
Siku ya ziara ilipofika, Rais Mwinyi alitumia usafiri wa helikopta, kuelekea kusini mwa Tanzania, katika msafara huo alikuwepo pia ndugu Habib Halahala. Walipofika eneo la tukio, Helikopta ilipotua tu, miongoni mwa watu wa mwanzo kushuka ni Habib Halahala, aliwahi kushuka ili kupiga picha ya Rais akishuka kwenye helikopta hiyo.
Bahati mbaya wakati anashuka panga za helikopta bado zilikuwa zinazunguka kwa kasi, bila kujua Habib Halahala hakuinamisha kichwa lile panga la helikopta likapita nae kwenye shingo. Akafariki kifo kibaya cha maumivu makubwa sana.
Nimeona niilete leo jukwaani kwa faida ya kizazi hiki ambao wengi wao hawamfahamu wala hawakuwahi kusikia tukio hilo...wasalaaam
Pia soma - Nini chanzo cha kifo cha Habibu Halahala aliyekuwa mpiga picha wa Hayati Mwalimu Nyerere?