Habib Mchage chini ya genge la Nchimbi wameanza siasa za makundi ndani ya CCM mapema sana

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
12,213
Reaction score
28,916
DK. NCHIMBI NA DHANA YA “VICE-PRESIDENTIAL DILEMMA”

Tafakuri ya Habibu Mchange

Katika sayansi ya siasa kuna dhana inayojulikana kama “Vice-Presidential Dilemma” yaani mtego unaoweza kumkabili Makamu wa Rais anapotaka kujenga utambulisho na mustakabali wake binafsi wa kisiasa, huku akiwa sehemu ya Serikali ambayo anawajibika kubeba mafanikio na changamoto zake.

Swali huwa ni kuwa Makamu wa Rais anawezaje kujijenga kuwa Rais wa kesho bila kuonekana anaikimbia Serikali ambayo leo yeye ni mtu wake namba mbili?

Miongoni mwa walioichambua dhana hii ni mwanazuoni wa Marekani, Dk. Vance R. Kincade Jr., mtaalamu wa historia ya urais wa Marekani aliyefundisha katika vyuo vya Arcadia University, Rowan University na Philadelphia University.

Katika kitabu chake Heirs Apparent: Solving the Vice Presidential Dilemma, Kincade anaonyesha kwamba nafasi ya Makamu wa Rais inaweza kuwa daraja kuelekea urais, lakini pia inaweza kuwa mtego kwa anayetaka kujenga utambulisho wake bila kubeba kikamilifu rekodi ya Serikali aliyomo.

HISTORIA INA MIFANO MINGI

John C. Breckinridge wa Marekani, aliyekuwa Makamu wa Rais wa James Buchanan, aligombea urais mwaka 1860 na kushindwa.

Richard Nixon, baada ya miaka minane akiwa Makamu wa Rais wa Dwight Eisenhower, aligombea urais mwaka 1960 na kushindwa na John F. Kennedy.

Hubert Humphrey, Makamu wa Rais wa Lyndon B. Johnson, alikabiliwa na mazingira magumu zaidi mwaka 1968, wakati Vita vya Vietnam vikiwa mzigo mkubwa wa kisiasa kwa Serikali yao.

Alipotafuta urais, Humphrey alihitaji kujitofautisha na baadhi ya sera za Johnson bila kukwepa ukweli kwamba alikuwa sehemu ya Serikali iliyozitekeleza na hatimaye alishindwa na Richard Nixon.

Aidha, Walter Mondale, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jimmy Carter, aligombea urais mwaka 1984 na kushindwa dhidi ya Ronald Reagan.

Al Gore naye, baada ya miaka minane akiwa Makamu wa Rais wa Bill Clinton, alijenga umbali fulani na Clinton katika kampeni ya mwaka 2000, huku akitaka kuendelea kunufaika na mafanikio ya Serikali yao.

Gore alipata kura nyingi zaidi kitaifa, lakini akashindwa katika Electoral College, mifano ni mingi sana

Kadharika, Historia hiyo hiyo ina mifano ya waliofanikiwa.

Martin Van Buren, Makamu wa Rais wa Andrew Jackson, alichaguliwa kuwa Rais mwaka 1836.

kama ambavyo George H. W. Bush, baada ya miaka minane akiwa Makamu wa Rais wa Ronald Reagan, hakujenga kampeni yake kwa kuikimbia Serikali ya Reagan.

Kwa kiasi kikubwa aliubeba urithi wa Serikali yao, akajenga hoja ya mwendelezo na mwaka 1988 akachaguliwa kuwa Rais.

Somo muhimu hapa hapa si kwamba kuwa karibu na Rais kunahakikisha ushindi, wala kujitenga naye kunahakikisha kushindwa bali kuwa mtu namba mbili hakukupi moja kwa moja tiketi ya kuwa mtu namba moja.

Namna unavyoibeba Serikali unayoitumikia inaweza kuwa sehemu ya hukumu yako ya kisiasa baadaye.

YAMETOKEA AFRIKA PIA

Atiku Abubakar wa Nigeria alikuwa Makamu wa Rais wa Olusegun Obasanjo kuanzia mwaka 1999 hadi 2007.

Kadiri suala la nani angemrithi Obasanjo lilivyozidi kuwa kubwa, tofauti zao za kisiasa zilipanuka, mgogoro wao ulifikia hatua ambayo Rais na Makamu wake wakawa wapinzani wa kisiasa huku wakiwa viongozi wawili wakuu wa Serikali moja.

Atiku akaondoka chama chao cha PDP, akajiunga na chama cha Action Congress na kugombea urais mwaka 2007 hata hivyo HAKUFANIKIWA KUWA RAIS.

Dk. Saulos Chilima wa Malawi naye alikuwa Makamu wa Rais wa Peter Mutharika baadaye alijitenga kisiasa na Mutharika na DPP, akaongoza United Transformation Movement na mwaka 2019 akagombea urais dhidi ya Rais ambaye bado alikuwa Makamu wake. HAKUFANIKIWA KUWA RAIS

Baadaye Chilima alibadili mkakati, akaungana na Lazarus Chakwera katika uchaguzi wa marudio wa mwaka 2020 na kuwa tena Makamu wa Rais baada ya muungano wao kushinda.

Daniel arap Moi wa Kenya anatoa mfano tofauti ambapo akiwa Makamu wa Rais wa Jomo Kenyatta tangu mwaka 1967, alikabiliwa na mapambano makubwa ya kisiasa kuhusu urithi wa madaraka.

Baadhi ya wanasiasa walitaka hata utaratibu wa kikatiba ubadilishwe ili kumzuia kurithi mamlaka.

Hata hivyo, Moi hakujenga nguvu yake kwa kujitenga hadharani na Kenyatta japo alibaki ndani ya mfumo, na Kenyatta alipofariki mwaka 1978, Moi akarithi urais kwa mujibu wa utaratibu wa kikatiba na baadaye akaimarisha nafasi yake.

Mifano hii haimaanishi kwamba anayebaki karibu na Rais lazima ashinde au anayejitenga lazima ashindwe bali mazingira ya kisiasa, nguvu za vyama, uchumi, wagombea na wakati vina nafasi kubwa katika matokeo.

ZAIDI mifano hiyo inaonyesha ugumu wa kujenga kesho yako ya kisiasa huku ukijaribu kujitenga na gharama za Serikali unayoitumikia leo.

TUMTAZAME DK. NCHIMBI

Sina ushahidi wa kusema kwamba Dk. Emmanuel Nchimbi anajiandaa kugombea urais baada ya Rais anayemtumikia, na yeye mwenyewe hajaitangaza nia hiyo.

Lakini siasa hazichambuliwi kwa matamko pekee bali mienendo, lugha na political positioning ya kiongozi nazo hutoa picha.

Kwa msingi huo, dhana ya Vice-Presidential Dilemma inaweza kutumika kama lenzi ya kuchunguza mwenendo wa Dk. Nchimbi.

Je, anajenga political independence yake ndani ya Serikali, au anajenga political distance kati yake na Serikali ambayo yeye mwenyewe ni sehemu yake?

Kauli yake kwenye hoja ya Katiba mpya ni mfano mzuri kuutumia kujifunza kitu.

Tunafahamu kwamba Serikali yake imetangaza umuhimu wa Katiba mpya na kueleza mwelekeo wa kuendelea na mchakato huo baada ya kukamilika kwa maridhiano.

Tunajua pia kuwa Chama chake nacho kimeeleza umuhimu wa Katiba mpya.

Na hata Dk. Nchimbi mwenyewe naye anataka Katiba mpya.

Hakuna mgongano kabisa katika hilo la uhitaji wa katiba mpya.

Lakini anapowaambia wananchi “pambaneni mpate Katiba mpya”, huku akisema Katiba iliyopo inampa Rais “madaraka yasiyo na maana,” jambo linalohitaji maelezo ya ziada

Wananchi wapambane na nani?

Kama Serikali yake inataka Katiba mpya na chama chake kinataka Katiba mpya, mapambano hayo yanaelekezwa dhidi ya nani?

DK. NCHIMBI SI MTU WA NJE

Kwa mujibu wa Katiba, Makamu wa Rais ni msaidizi mkuu wa Rais.

Dk. Nchimbi kwa hiyo si mwananchi anayegonga mlango wa Serikali akidai majawabu bali yeye yupo ndani ya chumba ambamo majawabu yanapaswa kutengenezwa.

Kama Katiba ina mapungufu, ana nafasi ya kushiriki kuyatafutia ufumbuzi.

Kama Rais ana madaraka anayoyaona kuwa “hayana maana”, ana nafasi ya kumshauri Rais na kueleza ni madaraka gani hasa anayokusudia.

Kama mchakato wa Katiba mpya una kasoro au unachelewa, yeye ni sehemu ya uongozi unaowajibika kueleza tatizo na kusaidia kulitatua.

Kwa nafasi yake, wananchi tuna haki ya kutarajia zaidi ya kauli ya “pambaneni.”

Tunataka kujua Dk. Nchimbi mwenyewe amefanya nini?

MTEGO WA “CREDIT” BILA “COST”

Vice-Presidential Dilemma inakuwa muhimu zaidi inapounganishwa na dhana ya collective responsibility.

Kiongozi wa juu wa Serikali hawezi kuchukua credit ya mafanikio yake halafu political cost ya changamoto zake awaachie wengine.

Miradi ikifanikiwa—tumefanya.

Uchumi ukifanya vizuri—tumefanya.

Serikali ikipongezwa—tumefanya.

Lakini changamoto ikitokea—“pambaneni.”

Kimantiki, hiyo haikai sawa.

Collective responsibility haimaanishi kwamba viongozi wote lazima wafikiri sawa tofauti za mawazo zinaweza kuwepo, ushauri unaweza kuwa mkali na mjadala wa ndani unaweza kuwa mkubwa.

Lakini kiongozi aliye katika kilele cha Serikali kama Dk. Nchinbi hawezi kujitenga na wajibu wa changamoto za Serikali hiyo huku akiendelea kuwa sehemu ya mafanikio yake.

“MWENZETU SI MWENZETU”

Ninapotumia kauli ya “mwenzetu si mwenzetu”, simaanishi kwamba Dk. Nchimbi yupo nje ya Serikali au chama chake.

Kinyume chake hoja yangu inatokana na ukweli kwamba yupo ndani kabisa ya Serikali na chama.

Ninazungumzia mwenendo unaoweza kujenga taswira ya mwanasiasa anayetaka yeye binafsi aonekane mwema kwa gharama ya Serikali na chama ambavyo yeye mwenyewe ni sehemu ya uongozi wake.

Serikali inapokabiliwa na jambo lisilopendwa, lugha yake inaweza kumweka upande wa wanaoikosoa.

Chama kinapobeba lawama anaweza kuonekana akijenga umbali na lawama hizo lakini Serikali au chama kinapofanikiwa, yeye anabaki kuwa sehemu ya mafanikio hayo.

Hiyo ndiyo maana ya “mwenzetu si mwenzetu” katika tafakuri hii kuwa mwenzetu katika mamlaka na mafanikio, lakini kuonekana si mwenzetu wakati gharama za kisiasa za maamuzi ya Serikali au chama zinapotakiwa kubebwa.

Kwa lugha nyingine, ni hatari ya mwanasiasa kutaka kuwa “the good guy” kwa gharama ya timu yake mwenyewe.

Kama Serikali imekosea, Dk. Nchimbi akiwa msaidizi mkuu wa Rais alikuwa wapi?

Kama chama chake kimekosea, akiwa mmoja wa viongozi wake wakuu alifanya nini?

Kiongozi hawezi kuwa ndani ya nyumba, akafaidika nyumba ikiwa nzuri, lakini paa likivuja akasimama nje na kuwauliza waliomo kwa nini hawajalitengeneza.

INDEPENDENCE SI DISTANCING

Ifahamike kwamba Makamu wa Rais kuwa na utambulisho wake wa kisiasa si kosa, wala hapaswi kuwa kivuli kisicho na mawazo.

Lakini political independence na political distancing ni vitu viwili tofauti.

Independence ni kuwa na mawazo na utambulisho wako huku ukibeba wajibu unaotokana na nafasi yako.

Distancing ni kujenga taswira kwamba mafanikio ya Serikali yanakuhusu, lakini matatizo yake yanawahusu wengine.

Kiongozi makini anaweza kujenga jina lake bila kuifanya Serikali yake ionekane mbaya ili yeye aonekane mzuri.

Anaweza kujenga umaarufu bila kukifanya chama chake kuwa gharama ya umaarufu huo.

Na anaweza kutofautiana katika hoja bila kujenga picha kwamba “mimi nilijua, wao hawakujua.... mimi niko sahihi, wao ndiyo tatizo,” wakati yeye mwenyewe ni sehemu ya uongozi huo.

HISTORIA INATOA SOMO

Atiku wa Nigeria alijitenga na Obasanjo na hakufanikiwa kuwa Rais mwaka 2007.

Chilima wa Malawi alijitenga na Mutharika na hakufanikiwa kuwa Rais mwaka 2019.

Humphrey na Gore wa Marekani walikabiliwa na changamoto zao za kujitofautisha na Serikali walizokuwa sehemu yake, na wote hawakufanikiwa kuingia Ikulu.

Van Buren na George H. W. Bush walifanikiwa kutoka nafasi ya Makamu wa Rais hadi urais.

Moi wa Kenya alibaki ndani ya mfumo wa Kenyatta na hatimaye akarithi urais.

Historia zao hazifanani na sababu za matokeo yao ni nyingi. Lakini zinafundisha jambo moja muhimu:

Mtu namba mbili hawezi kuukimbia kabisa urithi wa Serikali anayohudumu ndani yake.

Mafanikio yake yatamfuata, na changamoto zake pia zitamfuata.

DK. NCHIMBI, “PAMBANENI” NA NANI?

Ieleweke wazi kwamba, kama ilivyo kwangu mimi na Watanzania wengine, Dk. Nchimbi naye ana haki ya kutaka Katiba mpya.

Anayo haki ya kuona mapungufu katika Katiba iliyopo.

Anayo pia haki ya kuwa na maoni kuhusu ukubwa wa madaraka ya Rais.

Lakini akiwa msaidizi mkuu wa Rais wajibu wake hauishii katika kuyaona au kuyataja matatizo.

Anaposema Katiba ina tatizo, amefanya nini kulitatua?

Anaposema Rais ana madaraka yasiyo na maana, amemshauri nini Rais?

Na Serikali yake inaposema yenyewe inataka Katiba mpya, halafu yeye akawaambia wananchi “pambaneni”, wananchi hao wapambane na nani?

Hili ndilo somo la Vice-Presidential Dilemma kwa Dk. Nchimbi.

Mtu namba mbili anaweza kujenga utambulisho wake, anaweza kuwa na mawazo tofauti, anaweza kujenga political capital yake.

Lakini akijenga sifa zake kwa kuifanya Serikali au chama chake ionekane ndiyo tatizo, anaweza kupata sifa ya leo na kutengeneza tatizo kubwa zaidi la kesho.

Kwa sababu ikiwa siku moja ataomba kuaminiwa zaidi, wananchi hatutamuuliza tu “Uliona matatizo gani?”

Tutakuwa na haki pia ya kumuuliza “Ukiwa msaidizi mkuu wa Rais na sehemu ya Serikali yenye mamlaka ya kuyatatua, wewe ulifanya nini?”

Na ikiwa taswira iliyojengwa ni ya yeye kuonekana mwema wakati Serikali na chama chake vikibeba tutamuulizs zaidi “Kama wewe ulikuwa sahihi na wao ndiyo walikuwa tatizo, kwa nini uliendelea kuwa sehemu ya uongozi na maamuzi yao?”

Historia haitoi jibu kwa niaba ya Dk. Nchimbi. bali inatoa tahadhari Muhimu kuwa;

Mtu namba mbili anaweza kujenga jina lake akiwa ndani ya Serikali, lakini akijenga jina hilo kwa kuifanya Serikali na c
IMG-20260818-WA0014.jpg
hama chake kuwa gharama ya yeye kuonekana mwema, anaweza kuishia kudhoofisha msingi uleule anaoweza kuhitaji kuurithi kesho.

Hii ndiyo tafakuri yangu.

Habibu Mchange
0762178678
[email protected]
MAJIBU MCHANGE NI MFITINI ASIYEBADILIKA TANGU CHADEMA, ACT MPAKA CCM

Mtu akiwa kijana, kuna muda unaamini kadri anavyozidi kuwa mtu mzima basi busara, hekima na utulivu utaongezeka lakini hali haipo hivyo kwa Habibu Mchange.

Tabia zake bado ni zilezile. Mchochea majungu, mpenda fitna na mwenye tamaa ya kufanya lolote bila kujali utu ilimradi litamuingizia kipato.

Habibu Mchange alipoanza siasa zake ndani ya CHADEMA mwaka 2009 alipendwa, akafundishwa uongozi na hata kuaminiwa kuwa Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA), Kigamboni. 2010 akaaminiwa kuwa mgombea Ubunge wa Chadema jimbo la Kibaha Mjini.

Viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakamnadi, wananchi wakaamuunga mkono na kumpigania awe Mbunge lakini baadae “akawekwa sawa” na mpinzani wake Sylvester Koka wa CCM na akakubali kushindwa ubunge.

Mchange akaingia katika mradi mpya wa kuwachonganisha Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA enzi hizo Zitto Kabwe dhidi ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe. Baada ya ugomvi kuwa mkubwa akatangaza kugombea Uenyekiti wa BAVICHA Taifa 2011.

Akakusanya fedha kwa wadau akiwemo Zitto Kabwe na marafiki zake ili ahonge wajumbe wa uchaguzi huo. Kamati ya Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa ikabaini kuwa namba yake ya Vodacom ilikua ikituma 50,000 mpaka 100,000 kwa wajumbe mbalimbali hivyo akaenguliwa kugombea uenyekiti wa Bavicha kwa makosa ya Rushwa.

Akajitetea kuwa yeye mgombea aliwatumia fedha wajumbe kwa kuwa walikua wanamdai baada ya kuwakopa! Mchange hakukubali akaanzisha kampeni inaitwa PINDUA MBOWE. Chadema hawakumvumilia wakamfukuza mwaka 2013, na hivyo 2014 akajiunga chama cha ACT .

Huko ACT Wazalendo akawa akichonganisha viongozi; Mwenyekiti ACT Taifa Kadawi Limbu na Katibu Mkuu Samson Mwigamba. Akaeneza uvumi kuwa Kadawi Limbu ni ‘kibaraka’ wa CHADEMA aliyetumwa kuiua ACT. Watu wakaamini wakamng’oa Kadawi Limbu.

2015 katika uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu za ACT; Mchange akiwa pia mgombea ubunge kupitia ACT jimbo la Kibaha Mjini, alipandishwa jukwaani kuhutubia lakini akaporomosha matusi mpaka viongozi wa ACT wakalazimika kumshusha jukwaanibna wakaomba radhi wananchi.

Uchaguzi ulipoisha na akaona mambo hayaeleweki ndani ya ACT Wazalendo akaamua ajiunge na CCM ambako amekua akishindwa ubunge kila anapogombea. 2020 alishindwa alipogombea Kibaha Mjini akaanza kulalamika kuwa uchaguzi ulijawa na Rushwa.

Baada ya kukosa ubunge amekua akiendesha miradi mbalimbali kupitia gazeti la Jamvi la Habari. Akichafua viongozi na kuwachonganisha kutokana na maslahi ya kifedha anayopata.

Mchange anaweza kumuweka ukurasa wa mbele wa gazeti la Jamvi la Habari mtu mmoja anayelenga kumchafua hata kwa mwezi mzima bila kubadili habari. Kwake hajali kuhusu kuuza nakala za gazeti lake bali anajali kulipwa fedha ili achafue viongozi.

2025 alijaribu kutaka Ubunge jimbo la Kigamboni. Akazunguka kuomba fedha kwa viongozi na wafanyabiashara huku sehemu zingine akitishia asipopewa fedha atawachafua. Alipopewa fedha akaanza kugawa rushwa kwa wajumbe hovyohovyo na baadae akakamatwa na kuhojiwa na TAKUKURU.

Uchaguzi mkuu ulipoisha Mchange akaingia katika mradi mwingine hivi karibuni wa kumtuhumu mfanyabiashara Nillesh kuwa ndio anayewapa mabilioni CHADEMA ili waishambulie serikali. Wabunge mbalimbali na viongozi dini walikemea propaganda hizo lakini hakuacha.

Kwa sasa Mchange yupo kwenye mradi mpya wa kumsakama, kumzushia na kumchonganisha Makamu wa Rais Dk. Emmanuel Nchimbi ili aonekana kwamba anamuhujumu Bosi wake Rais Samia Suluhu Hassan.

Anafululiza kuchapisha uongo na uzushi. Analipa wachora katuni zinazomdhihaki Dk. Nchimbi. Anaunganisha video clips za upotoshaji. Analipa watu wapost uzushi huo ila wengi wamekua wakimkatalia.

Hatujui mradi wa Habibu Mchange utakaofuata baada huu utakuwa ni upi. Utakua ni wa kumchonganisha nani na nani au kumchafua nani. Huyu ndiye Habibu Mchange. Habadiliki, bado anazo tabia zilezile za ufitini na Uchonganishi tangu alipokua CHADEMA, ACT Wazalendo mpaka CCM!!

Mtu namba mbili anaweza kujenga jina lake akiwa ndani ya Serikali, lakini akijenga jina hilo kwa kuifanya Serikali na cView attachment 3652761hama chake kuwa gharama ya yeye kuonekana mwema, anaweza kuishia kudhoofisha msingi uleule anaoweza kuhitaji kuurithi kesho.

TEkaneni mmalizane
 
shida ni kwamba hata kama akiukwaa uraisi kwa katiba hii makamu wake ni lazima atokee zanzibar na zanzibar ~98% muslim, hivyo half way atatwaliwa pia halafu tutarudi square 1 hapa hapa tulipo raisi mzanzibari tena visasi vinaanza upya.
suluhisho la kudumu ni kubadilisha katiba haraka iwezekanavyo, kinyume na hapo wazanzibari hatuwakwepi, the pandora s box has already been opened ...
 
Siku zote ulikuwa kimya wakati Mchange anafanya siasa chafu kwakuwa alikuwa anawafanyia wapinzani, sasa uchafu wake kauleta ccm unajiliza na mabandiko marefu marefu.
 
Chimbi na Lissu unaenda na nani mimi 😂😂😂🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom