Tetesi: Hadhi (status) ya VODACOM imeshuka hapa nchini. Wanahama kutoka Mlimani City kwenda Kinondoni

Niko Voda tangu zamani......tangu waingie nchini na sijajutia. Labda wewe mtoa mada unalipwa na kampuni pinzani uwazodoe Voda. Kwenye Mpesa Voda wako vizuri kuliko wengine wote. Mikoani Voda wametamalaki. Mitandao mingine ina vifurushi vya bei ndogo zaidi lakini mawasiliano yanakatika kila wakati
 
Kaka kama huelewi si ukae kimya tu hadhi gani unayozungumzia kwa mtu ambaye yupo kwenye industry ya telecom,barabara ya Bagamoyo ndio hub ya industry ya telecom kwa Tanzania ,makampuni yote ya simu yapo kwenye maeneo ya barabara ya Bagamoyo,hii sio kwa bahati tu hapana hii inatokana na miundo mbinu rafiki,kama vile mkonga wa Taifa n.k pia kumbuka hili eneo ndio kuna Maxmalipo,Costech,jiulize Tigo,Halotel na Zantel wapo wapi.Hakuna eneo Tanzania nzima ambalo limerundikana kamapuni za mawasiliano kama barabara ya Bagamoyo maeneo kuanzia Morocco hadi Mwenge ndio Silicon Valley ya Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…