Hadhi ya kuitwa ‘Balozi’ huwa ina faida gani kwa mtu asiyetumikia tena ubalozini?

Mama inapaswa atambue kuwa hadhi na vyeo vya kibinadamu ni ubatili mtupu sababu hapa duniani sisi wana wa Adamu tu wapitaji tu...

Hata uitwe Rais wa marais au wana wa Adamu wote, ipo siku utaitwa jina moja sawasawa na kapuku aliyekuwa hajulikani juu ya jamii ya watu...

Balozi ana shtakiwa vizuri tu kama akifanya jinai na ishawahi tokea nyuma na hata kwa Slaa mwenyewe kabla hajavuliwa hiyo hadhi...
 
Tanzania tuna sifa za kijinga sana,na hii ni Kwa sababu ya uelewa wetu mdogo watz.watu wanapenda kuitwa wastaafu
Sisi wa tz shida sana, tunapenda titles hadi inakera. Tulipokuwa wadogo title tulio ijua ni dr anaetibu. Baadae tukajifunza kuna dr wa mifugo duniani (siyo uk), halafu dr wa kusoma phd. Balaa lika anzia hapo, huko afya kila mtu akaanza kuitwa dr. Hujui dr wa kweli ni yupi bola liende. Ghafla bin vuu viongozi wetu wakawa wanatunukiwa degree za heshima (honoris causa)- Mwalimu akazikusanya za kutosha lakini hakupenda kuitwa dr. Nyerere. Wakafuata wengine kwa staili hiyo hiyo Mwinyi na Mkapa, alipoingia Kikwete yeye akakubali kuvumisha u dr wake. Magufuli alikuwa na phd(udsm), sasa awamu hii mama hakutaka kuachwa mbali na tuna Dr. Suluhu na hiyo title anaipenda sana. Magufuli kama sikosei (au ni kikwete) ndio akatuletea mabalozi wa nchi kavu (sauti ya Mpango) yaani ubalozi ukawa ni title na cheo hata kama hujatumwa nje kumuwakilisha raisi. Kijazi nae aliporudi kuwa katibu mkuu kiongozi ikazalisha style ya kuwaita hawa waheshimiwa mabalozi ndio tukampata balozi dr. Bashiru na sasa balozi dr kusiluka. Huko foreign wako wengi ambao ni mabalozi wa "nchi kavu". Ubalozi ndio huo. Kwenye professions nyingine nako hakuja lala badala ya mr. Hamza ambae ni engineer sasa tuna Eng. Hamza, mhasibu mwenye Cpa sasa ni CPA Hamza. Hayo ndiyo maisha yetu watanzania. Tutaona mengi.
 
Mabalozi wa Nchi kavu ! 🙄😱
Sijawahi kusikia hii kitu 🙄😂😂
 
Mbona kuna.watu humu ndani wanalia sana! Huyu si alisema wachukue hicho cheo hata wakitaka leo!
 
Cheo cha ubalozi ilikuwa zamani
Mabalozi wengi walikuwa wanajielewa
Sahvi unaweza kusikia mwijak kapewa ubalozi

Ova
 
Mwalimu Nyerere,alikuwa hawachekei wanaotaka kuburuga amani,hata kama militafuta uhuru pamoja,chamoto atakuonyesha tu,huyu alimuogopa Mwalimu Nyerere,Kambona alikuwa waziri,lakini alikimbia nchi na uwaziri wake,alipotaka kuuruga amani.
 
Mwalimu Nyerere,alikuwa hawachekei wanaotaka kuvuruga amani,hata kama walitafuta uhuru pamoja.Kambona alikimbia nchi,akiwa waziri,na wengine wengi chamoto walikiona.
 
Mwalimu Nyerere,alikuwa hawachekei wanaotaka kuburuga amani,hata kama militafuta uhuru pamoja,chamoto atakuonyesha tu,huyu alimuogopa Mwalimu Nyerere,Kambona alikuwa waziri,lakini alikimbia nchi na uwaziri wake,alipotaka kuuruga amani.
Unaota nadhani! Mzee Tibandebage au mtu mwingine???? Mzee Tibandebage ampinge Nyerere!!!!!! We acha hizo. Kama hujui kitu nyamaza
 
Sawa ila niweke sawa ni BABA Mkubwa na Cardinal
Niweke sawa zaidi ni baba mkubwa wa Cardinal.
Ukisema baba mkubwa na Cardinal unamaanisha watu wawili yaani kuna baba mkubwa na kuna cardinal, au mtu mmoja mwenye sifa hizo mbili. Unamaanisha huyo ni baba mkubwa na pia huyo huyo ni Cardinal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…