Hadhi ya kuitwa ‘Balozi’ huwa ina faida gani kwa mtu asiyetumikia tena ubalozini?

Hadhi ya kuitwa ‘Balozi’ huwa ina faida gani kwa mtu asiyetumikia tena ubalozini?

Dr.slaa ameshitakiwa akiwa bado anahadhi ya ubalozi na alilala rupango na ubalozi wake

Kwahyo hiyo point ni dhaifu
 
Mwalimu Nyerere,alikuwa hawachekei wanaotaka kuvuruga amani,hata kama walitafuta uhuru pamoja.Kambona alikimbia nchi,akiwa waziri,na wengine wengi chamoto walikiona.

Huyo aliyekuwa hawachekei watu sasa hivi yu wapi?

Juhudi zote alizofanya kuna msingi wowote wa uadilifu uliojengeka hadi leo kwamba watu wanaufuata?
 
Hizo ni hasira tu baada ya madalali wa mauzo kusagiwa kunguni
 
Huenda kuna kitu sikijui au kimenipita. Hivi mtu ambaye aliwahi kuwa balozi, na sasa hatumikii tena kazi hiyo, kuendelea kuitwa balozi huwa kunaongeza nini kimaisha yake ukiondoa sifa za kujidai kijamii au kumbukumbu za zamani?

Je, kuna posho huwa wanalipwa kwa kuwa na hiyo hadhi ya kuitwa balozi?

Je, huwa wanaendelea kubakia na diplomatic status previlege maisha yao yote wakiwa na hiyo hadhi ya kuitwa balozi?

Hapa ni baadhi ya watu ya watu waliowahi kuwa mabalozi na hatukuwahi kuwasikia wakiitwa au kujiita mabalozi mara baada ya kuondoka kwenye kazi za ubalozi.

1. John Samweli Malecella
2. Salim Mohamed Salim
Wala sishangai, sikuwahi kuutambua huo ubalozi, alipewa ubalozi "KIHUNI" kavuliwa ubalozi "KIHUNI"
 
Niweke sawa zaidi ni baba mkubwa wa Cardinal.
Ukisema baba mkubwa na Cardinal unamaanisha watu wawili yaani kuna baba mkubwa na kuna cardinal, au mtu mmoja mwenye sifa hizo mbili. Unamaanisha huyo ni baba mkubwa na pia huyo huyo ni Cardinal.
Mother tongue ina akisi sentenso tunazotunga katika Kiswahili hasa sisi wachanga! Niwie radhi bwashee
 
Niweke sawa zaidi ni baba mkubwa wa Cardinal.
Ukisema baba mkubwa na Cardinal unamaanisha watu wawili yaani kuna baba mkubwa na kuna cardinal, au mtu mmoja mwenye sifa hizo mbili. Unamaanisha huyo ni baba mkubwa na pia huyo huyo ni Cardinal.
Kiswahili hicho. Wengi husema ni ndugu na fulani badala ya ndugu yake fulani.
 
Sisi wa tz shida sana, tunapenda titles hadi inakera. Tulipokuwa wadogo title tulio ijua ni dr anaetibu. Baadae tukajifunza kuna dr wa mifugo duniani (siyo uk), halafu dr wa kusoma phd. Balaa lika anzia hapo, huko afya kila mtu akaanza kuitwa dr. Hujui dr wa kweli ni yupi bola liende. Ghafla bin vuu viongozi wetu wakawa wanatunukiwa degree za heshima (honoris causa)- Mwalimu akazikusanya za kutosha lakini hakupenda kuitwa dr. Nyerere. Wakafuata wengine kwa staili hiyo hiyo Mwinyi na Mkapa, alipoingia Kikwete yeye akakubali kuvumisha u dr wake. Magufuli alikuwa na phd(udsm), sasa awamu hii mama hakutaka kuachwa mbali na tuna Dr. Suluhu na hiyo title anaipenda sana. Magufuli kama sikosei (au ni kikwete) ndio akatuletea mabalozi wa nchi kavu (sauti ya Mpango) yaani ubalozi ukawa ni title na cheo hata kama hujatumwa nje kumuwakilisha raisi. Kijazi nae aliporudi kuwa katibu mkuu kiongozi ikazalisha style ya kuwaita hawa waheshimiwa mabalozi ndio tukampata balozi dr. Bashiru na sasa balozi dr kusiluka. Huko foreign wako wengi ambao ni mabalozi wa "nchi kavu". Ubalozi ndio huo. Kwenye professions nyingine nako hakuja lala badala ya mr. Hamza ambae ni engineer sasa tuna Eng. Hamza, mhasibu mwenye Cpa sasa ni CPA Hamza. Hayo ndiyo maisha yetu watanzania. Tutaona mengi.
'mabalozi wa nchi kavu' ndio wapoje ?...Au ni wale hawajaripoti/hawajapangiwa vituo vya kazi ?
 
'mabalozi wa nchi kavu' ndio wapoje ?...Au ni wale hawajaripoti/hawajapangiwa vituo vya kazi ?
Hawa ni wale wanaopewa hadhi ya ubalozi bila kupangiwa kituo mfano bashiru. Wako pia wizarani ambao wana hiyo hadhi au cheo lakini hawana vituo vya kibalozi nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom