Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
- Thread starter
-
- #21
Umesema kabisa ukweli. Kila mtu akiwemo Mimi, nilitamani sana kupata hela but cha ajabu tangu nikiwa shule ya msingi miaka hiyo ya 1990s tena kijijini, niliaminishwa kuwa maisha mazuri yanapatikana kwa kusoma na kwa kuwa nilikuwa naogopa kuishia kuwa mkulima, nilijitahidi kusoma ili ni is hi vizuri hasa nikiangalia askari polisi, madaktari, walimu na viongozi wa tarafa na kata waliokuwa wakifanya kazi kijijini kwetu. Tena cha ajabu nilivutiwa sana na jinsi askari Polisi walivyokuwa wakiishi vizuri wakiwa na wake wazuri sana.Akili bila mali ni sawa na debe tupu :
Kigezo 1 hela
Kigezo 2 hela
Kigezo 3 Pesa
Hata ukiwa mbumbumbu ukiwa na hela utaitwa mh
Of course, leo hii baada ya sekta binafsi kuwa na maslahi mazuri kuliko makundi ya watumishi niliyotaja, yanaweza kukufanya ukanishangaa kuvutiwa made makundi hayo but trust me, zamani hao ndio watu walioishi vizuri wilayani ukitoa watumishi wa Ofisi ya DC huku Halmashauri ndio zinaanza kupata nguvu.
Sasa, ukiniambia mimi mhenga, nitakwambia hela ilipatikana kwa kusoma tu na hadi leo Ndiyo njia pekee ya mkato kwa masikini kutajirika kwani mafanikio mengine ya kuwa na biashara kubwa huwa ni majaaliwa zaidi ama kuwa tayari kutumia wimbo wa 50 Cent "Get rich or die trying." Yaani uutafute kwa njia yoyote - kwa ujambazi, uchawi ama kujihusisha na madawa ya kulevya. Hivyo vyote you're likely to be doomed, but kadri kitu kinavyokuwa kizuri ndio risk yake inavyoongezeka.