Hadi bajeti ya Tanzania, Uganda na Rwanda ziunganishwe ndio zifikie ya Kenya

Bagamoyo ni ndoto tu.huku lamu port ikianza mwendo..😀
 
Mie uzalendo kwangu ni kukosoa ili wahusika wafanye kweli.Hiyo mambo ya kusema sijui gesi mara bomba "ita" wakati hata ujenzi haujaanza sio realistic points,tunaoshindana nao wanaweka on going projects na sio itarajiwayo
 
Ukanena vyema kaka, ila wacha nikukosoe kwa masuala mawili au matatu. Mradi wa LAPSSET hata kabla haujabuniwa, taifa la Uhabeshi lilikua latumia djibuti kwa usafiri wake wote na mradi huu ulikua uwezeshe Uhabeshi kutotegemea djibuti kwa usafiri wake wote ilivyo sasa hivi. Mataifa ya kongo, Uganda na Rwanda hata hayakua katika mipangilio ya LAPSSET kwa hivyo kuwepo au kutokuwepo kwao si pigo kubwa kwa mradi huu. Taifa ambalo likijiuzulu huenda mradi huu ukaumia ni Sudan Kusini, na sioni hilo likifanyika kwani hata Tanzania na djibuti ziko mbali sana na pia mali yao itapitia nchi mingi na kuongeza zigo la matumizi ya hela. Labda waitumie Sudan Kaskazini na twajua uhusiano baina yao.

Kisha ukiangalia matumizi ya bajeti kwa kila sekta, miradi yagubia 34.6%, na masomo 20.4%, zaidi ya nusu ya bajeti kwa hizi mbili huku usalama ukipewa 7.4% tu. Alshabab wenyewe nguvu ishawaishia kwani sijasikia wakishambulia kenya kwa karibu mwaka mzima hivi
 
Tatizo S/Sudan haisomeki ni kama DRC na Somalia,miaka nenda rudi wanagombanaga tu sasa sijui watatulia lini ili wajenge uchumi yao ili na sie wenye sea access tufaidi.But hatari kubwa inaikabiri LAPSSET endapo S/Sudan wata opt kuunga bomba na Uganda via TZN au wakaunga na Ethiopia via Djibout
 
Tanzania ya viwanda kwa hela za mikopo [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Livale Unasahau kwenye Jumuiya za kiuchumi umbali sio kitu wala tatizo! Uganda wana miundombinu bora kuelekea Sudan Kusini kuliko Kenya na kingine ni uhakika wa kuwa na mtambo wa kuchuja mafuta Uganda na bomba kuelekea Pwani ya Afrika Mashariki ukilinganisha na Kenya. Ukiangalia jinsi ramani ilivyo umbali toka Juba mpaka Hoima si zaidi ya km 400 na mdogo kuliko umbali toka Juba au Unit state (kwenye visima vya mafuta) mpaka Lokichar kunapopangwa kujengwa mtambo wa kuchuja mafuta ghafi. Halafu kutoka Lokichar kwenda Lamu huko kote kutokana na bonde la Ufa kuna mabonde na miinuko ukiacha kutowepo miundombinu, umeme na maji.

Kingine ni kuwa Kampuni ya Total wanamilika zaidi ya km za mraba 120,000 za vitalu vya mafuta na viko kwenye njia ambapo bomba la kwenda Kenya litapita (kama litajengwa) yaani upande wa kusini mwa Sudan Kusini! Mbali na hilo, Total wanamiliki vitalu vya mafuta Ziwa Albert upande wa Kongo Kinshasa (vyenye mafuta yaliyohakikiwa) na pia Ziwa Tanganyika Tanzania upande wa Kigoma (uchunguzi ukiendelea). Hii ina maana punguzo kubwa sana kama wakigawana gharama pamoja hizi nchi tatu na pia hata na Rwanda kama ikigundulika uwepo wa mafuta.

Ukiacha hayo yote kuna suala la siasa Rais Museveni ana ushawishi kwa Kiir zaidi ya Rais Uhuru. Kumbuka wanajeshi yaani JWUG walizuia jaribio la Mapinduzi la Serikali ya Sudan Kusini na wapo mpaka sasa Juba kuzuia fujo zozote. Sidhani kama Museveni huyohuyo atashindwa kumshawishi Kiir kusafishia mafuta yake Hoima na kuyasafirisha Bandari ya Tanga. Ukiachilia mbali uwepo wa Sudan ya Kusini katika Shirikisho unaipa nafasi ya punguzo la tozo kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Zaidi ya hayo Ushawishi wa CCM unakua siku hadi siku kuanzia usuluhisho, muafaka na uundaji wa serikali ya muungano ya Kiir na Marchar yote yalichorwa Arusha kwa kupitia CCM kama Chama tena kwa baraka za Museveni. Ubalozi wa Sudan upo Dar sasa na mara nyingi mshauri wa Kiir anaonekana Ikulu!

Haya yote tukiacha hali legelege ya usalama kaskazini mwa Kenya. Kutoka kwa tishio hai la Al Shaabab na pia fujo za kikabila zitokanazo na migogoro ya Ardhi na wizi wa mifugo.

Ukiacha hayo kuna Mgogoro unafukuta Umoja wa Kimataifa kuhusu eneo la pembe tatu la Ilemi ambalo linagombaniwa kati ya Kenya na Sudan ya Kusini. Kiukweli, sioni nafasi ya Kenya katika kufaidi rasilimali za Juba naongelea haya kama mtu ninayejua kinachoendelea, tukiachia mbali uwezo wa Kenya kupata ufadhili wa Bomba na ujenzi wa Bandari Lamu.

Zaidi kiutaalam, Kina cha Lamu ni kifupi na chenye mikoko na viumbe haba na vile vyenye hatari kutoweka majini, kinahitaji kuongezwa kupokea meli za mafuta na gharama ni zaidi ya dola milioni 800, ukiachilia mbali uharibifu wa mazingira. Zaidi ya hayo uendeshaji wa Lamu unaathiriwa na Pepo za Monsoon zinazodumu kwa mwezi mzima kila mwaka tatizo ambalo halipo Tanga inayokingwa na visiwa vya Pemba. Kelele za Kenya zisikutishe utaona katika uzinduzi wa bomba na wa upanuzi wa bandari ya Tanga tena na jinsi viongozi wa Jubilee Wakikuyu wanavyomchafua Kiir. Nina uhakika Sudan Kusini watakuja Tanga.


nomasana, sam999, NairobiWalker, hbuyosh, msemakweli, simplemind, Kimweri, Bulldog, MK254, Kafrican, Ngongo, Ab_Titchaz, mtanganyika mpya, JokaKuu, Ngongo, Askari Kanzu, Dhuks, Yule-Msee, waltham, Mzee, mombasite gabriel, Juakali1980, Boda254, mwaswast, MwendaOmo, Mwanakijiji, Iconoclastes, oneflash, Kambalanick, 1 Africa, saadeque, burukenge, nyangau mkenya, Teen-Upperhill Nairobi, kadoda11
 
Nchi zingine zimeamka na bado Kenya ipo macho bado hivyo basi sioni mabadiliko yeyote, Kenya bado inaongoza ukanda huu na mambo hayatabadilika hivi karibuni na yakibadilika labda Kenya iongoze Africa nzima.
influence ya kenya inazidi kupungua katika ukanda huu na hilo halihitaji elimu ya PHD kulijua...

Siombi na wala sintoiombea kenya kushuka kwa sababu hili halitokuwa vyema kwa nchi za ukanda wetu maana yatupasa kunyanyuana na kutumiana
 
influence ya kenya inazidi kupungua katika ukanda huu na hilo halihitaji elimu ya PHD kulijua...

Siombi na wala sintoiombea kenya kushuka kwa sababu hili halitokuwa vyema kwa nchi za ukanda wetu maana yatupasa kunyanyuana na kutumiana
After 2017 there will be no Catching up with Kenya!
 

Geza sidhani kama Sudan wataincur gharama kujenga bomba na vile uchumi wao ulivo sasa hivi baada ya vita, na wanayapitisha N Sudan mind you, na N Sudan wamewapunguzia hadi bei ya kusafirisha nilisoma mahala.
 

All well and good kaka, ila kwenye analysis yako umehold all scenarios constant for Kenya bila kufanya the same for Tanzania. There are always two sides to a coin. Hapo kwenye red kuna mambo mengi sana ambayo huenda yakabadilika depending on so many unpredictable events. E.g. Any of these scenarios changes the landscape.

1. Kenya kupata mafuta zaidi kwenye prospecting zones zao.
2. Regime change in Nairobi/Juba/Uganda/Ethiopia.
3. Kenya kupata ufadhili wa LAPPSET e.t.c.

The opposite is also true,
1. UG wakipata mafuta zaidi na ku-fast track ujenzi wa pipeline.
2. Uchaguzi wa Kenya kuwa na vurugu/machafuko
3. Vitalu vya mafuta kuchange hands. Kwa mfano from Total to CNOOC n.k.

Mwisho wa siku haya yote yanabakia kuwa predictions tu, with a varying degree of probability. Siasa (especially za Africa) haitabiriki na mfano mzuri ni TZ. kama kuna yeyote alipanga yake kule RW/Kenya/UG/DRC e.t.c akitarajia Membe atakuwa Rais sasa hivi atakuwa amelazwa ICU na pressure kwa sababu ilikula kwake. 🙂
 
Mafuta ya Uganda yanatosha wana zaidi ya 6 bln barrels (1.6 bln recovable) kwa kuanzia na Total wame-commit tayari ufadhili! Hiyo fasttrack unayoongelea ni ipi au unathani itakuwa kama ile yenu iliyochukua miaka mitatu? we upo Dunia gani? Au maumivu ya kukosa mradi yanakufanya kufikiri negative! As a matter of fact kuanzia July safari za uzinduzi zitaanza. Hayo mafuta ya Kenya si rahisi kuwa mengi karibuni maana makampuni mengi yanajitoa baada ya kuingia hasara ya kuchimba visima bila mafuta! Hata Tullow oil yenyewe ipo kwenye hatihati za kufilisika! hizi habari zote zipo online kama unajisumbua kutafuta!

Kuanza kufikiria uwezekano wa mradi kukwama kutokana na regime change ni kutokuwa realistic! Sioni uwezekano wa kubadilika kwa uongozi kwa Ethiopia, Uganda na Juba labda Kenya! Otherwise kama unamaanisha kupitia coup na sponsor wakiwa Kenya! Kenya hawana ujanja huo maana kufanya hivyo ina maana kutoa greenlight kwa wengine kufanya the same kwenu! Msimjaribu Museveni maana kufanya hivyo ni kutuchokoza Tanzania pia! Na kwa jinsi hali ya kisiasa ilivyo tete Kenya msithubutu kujaribu! Bakieni hukohuko Somalia na Al Shaabab wenu...
 
Woi... Stop talking about your dreams.. More than half of Tzs least ve below the poverty line... Your GDP per capita speaks for itself.
Ndiyo maana tunawaambia elimu yenu hiyo ya kukariri. GDP, per capita income doesn't give the real distribution of the National cake. This is why your GDP sounds great, but the poverty is widely spread. Only kikuyu & Co are the ones who enjoy the Kenya's chow.
 
Geza umefanya uchanganuzi mzuri na wa kina wa hoja zako but umesahau kuweka "at ceteris paribus" especially geopolitics ya eneo letu hili
 
Geza umefanya uchanganuzi mzuri na wa kina wa hoja zako but umesahau kuweka "at ceteris paribus" especially geopolitics ya eneo letu hili
geopolitics imefanya nn? Kenya ana ubavu wa ku-sabotage Mfaransa? Uganda? Rwanda? Tanzania? Alogwe ajaribu na jinsi walivyo divided kiubali waisthubutu!
 

SMH. You see that fast disappearing thin line in the horizon? That was the point on my comment and you missed it by miles. Forgive my intrusion, please carry on...
 
Kwa analysis yako kuna ukweli hapa na pale lakini pia hoja zipo. Ni kweli Hoima ikaribu na unity state kuiliko Lokichar lakini tofauti si kubwa vile, takriban 900km kwa zote (punguza kiasi kwa hoima ukiongeza kiasi kwa Lokichar) kwa hivyo hela za kujengea bomba hazijatofautiana kwa umbali sana. Kisha kuhusu Alshabaab, hawajawahi shambulia eneo lolote kilomita kama 500 hivi kutoka Lokichar. Na pia shambulizi lao la mwisho Kenya ni karibu mwaka mzima uliopita kumaanisha nguvu zawaishia hao. Mizozo ya na vita vya kikabila kuhusu lishe na maji eneo hilo na punje dogo ukilinganisha na mizozo Sudan Kusini, na mizozo hii ni mda pia tangu niiskie na nikidhani ni juu ya serikali ya majimbo k

Uliyonena kuhusu upepo na wimbi ni kweli, lakini vivyo hivyo ndivyo Mombasa ilivyo ila imenawiri katika biashara ya usafirishaji bandarini na pia ipo mtambo wa kuchuja mafuta ghafi usioathiriwa na mawimbi. Lakini hapo Tanga ina bahati kibiashara.

Lipo jambo pia watu wengi husahau, LAPSSET sio kuhusu mafuta tuu, hata mwanzoni ilibuniwa ili iwezeshe kaskazini mwa Kenya kunawiri kiuchumi kwa kuiunganisha na bandari. Karibu 700km za barabara zishajengwa na zimeleta mabadiliko makubwa kwa wakaazi wa huko ingawa bado kazi kubwa ipo. Ndio, mafuta ni ya maana sana kwa mradi huu lakini kama ingekua kuhusu mafuta tu basi bomba la kusafirisha mafuta na mtambo ma kughuja mafuta pekee zingetosha. Barabara, reli, majiji, viwanja vya ndege na kadhalika havingehitajika hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…