Livale unasahau kwenye jumuiya za kiuchumi umbali sio kitu! Uganda wana miundombinu bora kuelekea Sudan Kusini kuliko Kenya na kingine ni uhakika wa kuwa na mtambo wa kuchuja mafuta Uganda na bomba kuelekea Pwani ya Afrika Mashariki ukilinganisha na Kenya. Ukiangalia jinsi ramani ilivyo umbali toka Juba mpaka Hoima si zaidi ya km 400 na mdogo kuliko umbali toka Juba au Unit state (kwenye visima vya mafuta) mpaka Lokichar kunapopangwa mtambo wa kuchuja mafuta ghafi. Halafu kutoka Lokichar kwenda Lamu huku kote kuna mabonde na miinuko ukiacha kutowepo miundombinu, umeme na maji.
Kingine ni kuwa Total wanamilika zaidi ya km za mraba 120,000 za vitalu vya mafuta na viko kwenye njia bomba la kwenda Kenya litapita yaani upande wa kusini mwa Sudan Kusini! Mbali na hilo, Total wanamiliki vitalu vya mafuta ziwa Albert upande wa Kongo Kinshasa (vyenye mafuta) na pia Ziwa Tanganyika Tanzania upande wa Kigoma (uchunguzi ukiendelea). Hii ina maana punguzo kubwa sana kama wakigawana gharama pamoja hizi nchi tatu na pia hata na Rwanda kama kuna mafuta.
Ukiacha hayo yote kuna suala la siasa Museveni ana ushawishi kwa Kiir zaidi ya Uhuru. Kumbuka wanajeshi yaani JWUG walizuia jaribio la Mapinduzi na wapo mpaka sasa Juba kuzuia fujo. Sidhani kama Museveni huyohuyo atashindwa kushawishi Kiir kusafishia mafuta yake Hoima na kuyasafirisha Tanga. Ukiachilia mbali uwepo wa Sudan ya Kusini katika Shirikisho unaipa nafasi ya punguzo la tozo kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Zaidi ya hayo Ushawishi wa CCM unakua siku hadi siku kuanzia usuluhisho, muafaka na uundaji wa serikali ya muungano ya Kiir na Marchar yote yalichorwa Arusha kwa kupitia CCM kama Chama tena kwa baraka za Museveni. Ubalozi wa Sudan upo Dar sasa na mara nyingi mshauri wa Kiir anaonekana Ikulu!
Haya yotee tukiacha hali legelege ya usalama kaskazini mwa Kenya. Kutoka kwa tishio hai la Al Shaabab na pia fujo za kikabila zitokanazo na migogoro ya Ardhi na wizi wa mifugo.
Ukiacha hayo kuna Mgogoro unafukuta Umoja wa Kimataifa kuhusu eneo la pembe tatu la Ilemi ambalo linagombaniwa kati ya Kenya na Sudan ya Kusini. Kiukweli, sioni nafasi ya Kenya katika kufaidi rasilimali za Juba naongelea haya kama mtu ninayejua kinachoendelea, tukiachia mbali uwezo wa Kenya kupata ufadhili wa Bomba na ujenzi wa Bandari Lamu.
Zaidi kiutaalam, Kina cha Lamu ni kifupi na chenye mikoko na viumbe haba wa majini, kinahitaji kuongezwa kupokea meli za mafuta na gharama ni zaidi ya dola milioni 800, ukiachilia mbali uharibifu wa mazingira. Zaidi ya hayo uendeshaji wa Lamu unaathiriwa na Pepo za Monsoon zinazodumu kwa mwezi mzima kila mwaka tatizo ambalo halipo Tanga inayokingwa na visiwa vya Pemba. Kelele za Kenya zisikutishe utaona katika uzinduzi wa bomba na wa upanuzi wa bandari ya Tanga tena na jinsi viongozi wa Jubilee Wakikuyu wanavyomchafua Kiir. Nina uhakika Sudan Kusini watakuja Tanga.