Binafsi kama mpenzi wa soka nilikuwa nahamasika kulipa kiingilio kwenda kuangalia mechi za timu yangu ya Simba nikiamini mapato hayo ni sehemu muhimu ya kuinufaisha club.
Hata hivyo nilikatishwa tamaa sana na tangazo la bodi ya ligi kuhusu mapato ya mlangoni ya Simba. Kibaya zaidi hakuna kiongozi aliyelalamika wala kushtushwa na mapato hayo kiduchu. Sisi wengine tuliona kuna wizi mkubwa sana unafanyika na hatujui anayefaidika ni nani.
Kutokana na hali hiyo, imetukatisha tamaa sana watu kuingia kuisapoti timu huku mapato yakihujumiwa na hakuna anayelalamika. Hadi tutakapoambiwa ukweli kuhusu mapato ya watu wanaoujaza uwanja huwa yanavujia wapi, ndipo tutakuwa na ari tena ya kuisapoti timu yetu kwa kuingia viwanjani.