Hadi Juni 2021 (mwaka huu) DAR itakuwa Ulaya ndogo

Dar kama ulaya by June 2021. Haya tusubiri time will tell.
 
Hiyo ulaya mpaka uende barabarani ila ukienda kwenye makazi ya watu ni vilevile hakuna tofauti.
Uchafu na nyumba zilizojengwa hovyo.

Ningekubali kama wangeanza kudeal na makazi ya wananchi na kupanga nyumba vizuri pia nyumba ziwe za kuanzia viwango fulani tu ili kuboresha usafi wa mazingira.
Pia wangeanza kuweka urban parks ili watu wapate kupumzika na kupunga hewa ya asili pia kuondoa mavumbi.
Like new york central park.

Au itakuwa ukitoka mtaani kwako ukifika barabarani utajihisi upo New York then jioni unarudi Mbagala kuoga vumbi.
 
Wadau Habari za kazi. Nimetafakari Sana Miradi ya Kimaendeleo iliyoko Dar na hatua iliyofikia, inatia Moyo kiasi kwamba ndani ya mwezi 6 tangu sasa kwa MIUNDOMBINU Dar itakuwa Kama Ulaya. Check Ubungo interchange, Flyover ya TAZARA, Flyover zinazojengwa Uhasibu na Ile ya makutano ya barabara ya Keko, barabara nzuri ya Ocean road, ya Victoria na Mwenge zinazoendelea kukamilishwa, barabara nzuri Sana ya kuelekea Morogoro, Daraja LA Slender, mibarabara ya Mwendokasi hadi Mbagala, Treni ya Mwendokasi yaani SIPATI PICHA. nawasihi Sana tuendelee kuwaombea viongozi wetu wakamilishe Miradi hiyo. NAWASILISHA

Rais wetu alikua anasisitiza sana ila nahisi hawa watendaji wake hawamuelewi.

Wamachinga wameharibu uzuri wowote wa Dar ambao mtu angeufurahia kasoro tu eneo la jeshi lugalo ndio mtu ukipita unafurahia.

Flyover Ubungo ukigeuka tu pembeni ukiona mabanda ya machinga utam wote kwisha. Mlimani City ndio kabisaa ni takataka. Ukienda city centre maeneo ya kuanzia DIT mabanda kila kona hadi machizi wanalala humohumo.

Haya saizi Bagamoyo Road kuanzia Mwenge hadi Morocco pameanza kupendeza ila nawaambia soon uzuri wote unaisha machinga wanahamia. Hivi hizi mamlaka haziendi hata hapo nairobi tu zikajifunze vitu vidogo kama hivi? Ndio ulaya tutaifikia kweli?

Hatusemi biashara zisifanyike, ila tafuteni utaratibu sehem za uso wa barabara kuu zibaki zinavyopendeza. Au basi mtangaze maeneo yote ya mbele ya barabara kuu ni ya jeshi ili machinga waondoke wenyewe pabaki pazuri kama Lugalo.
 
Iringa itakuwa kama Amsterdam( siyo yule wakili mkorofi)
Mibarabara na uwanja wa ndege wa kisasa.

Iila mtu asemee mkoa wake.
 
Wadau Habari za kazi. Nimetafakari Sana Miradi ya Kimaendeleo iliyoko Dar na hatua iliyofikia, inatia Moyo kiasi kwamba ndani ya mwezi 6 tangu sasa kwa MIUNDOMBINU Dar itakuwa Kama Ulaya. Check Ubungo interchange, Flyover ya TAZARA, Flyover zinazojengwa Uhasibu na Ile ya makutano ya barabara ya Keko, barabara nzuri ya Ocean road, ya Victoria na Mwenge zinazoendelea kukamilishwa, barabara nzuri Sana ya kuelekea Morogoro, Daraja LA Slender, mibarabara ya Mwendokasi hadi Mbagala, Treni ya Mwendokasi yaani SIPATI PICHA. nawasihi Sana tuendelee kuwaombea viongozi wetu wakamilishe Miradi hiyo. NAWASILISHA
Magufuli atakumbukwa kuliko rais yeyote yule tanzania maana aliyo yafanya kwa kipindi chake ataacha historia kubwa sana sana sana
 
Kabisaa hasa ukipita Jangwani flyover ikinyesha mvua, ukienda sokoni Mabibo, Stereo, Buguruni, Ilala, ukipita UN Road, Bibi Titi CBE, na Mfugale flyover wakati wa mvua ni kama ulaya wakati wa snow!

Sitaki kuongelea mitaa mingine! Kigogo Mburahati, sijui Mpalange n.k

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Wadau Habari za kazi. Nimetafakari Sana Miradi ya Kimaendeleo iliyoko Dar na hatua iliyofikia, inatia Moyo kiasi kwamba ndani ya mwezi 6 tangu sasa kwa MIUNDOMBINU Dar itakuwa Kama Ulaya. Check Ubungo interchange, Flyover ya TAZARA, Flyover zinazojengwa Uhasibu na Ile ya makutano ya barabara ya Keko, barabara nzuri ya Ocean road, ya Victoria na Mwenge zinazoendelea kukamilishwa, barabara nzuri Sana ya kuelekea Morogoro, Daraja LA Slender, mibarabara ya Mwendokasi hadi Mbagala, Treni ya Mwendokasi yaani SIPATI PICHA. nawasihi Sana tuendelee kuwaombea viongozi wetu wakamilishe Miradi hiyo. NAWASILISHA
Dar es salaam eneo kubwa limejaa nyumba za waswahili. Ziko hovyo, hazina mpangilio, Dar inakaliwa na wamaskini na mafukara wa kutupwa, Dar watu hula milo 2 tu kwa siku.
Dar es salaam uaimwone mtu kavaa suti , wengi hali zao ngumu sana.
Kwahiyo hizi interchange ndizo zinakupagawisha mpaka unasahau tafsiri sahihi ya maendeleo?
 
Hata huko Mwanza baada ya miezi 12 itakuwa kama ulaya au uchina kabisa. Yaani daraja la Kigongo - Busisi ambalo ni kubwa na zuri kuliko yote barani Africa litakuwa limekamilika. Fly overs za Mabatini na Furahisha zilishakamilika. Meli za kisasa zaidi ya 5 zimeshakamilika. Soko kuu la kisasa, stendi kubwa ya kisasa ya mabasi, reli ya umeme ya SGR inayotumia masaa 7 tu uko DSM, terminal II ya kisasa kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza International Airport, soko la kimataifa la Nile perch aka sangala, barabara za lami mitaa yote na kadhalika.
Alafu ndo panakuwa ulaya, tunadanganyikaa ulaya mfanano wake nchiii ipambane miaka 50 mingine at least tunaweza anza fananisha na vijinchi vidogo vya uko unapopasema
 
Wadau Habari za kazi. Nimetafakari Sana Miradi ya Kimaendeleo iliyoko Dar na hatua iliyofikia, inatia Moyo kiasi kwamba ndani ya mwezi 6 tangu sasa kwa MIUNDOMBINU Dar itakuwa Kama Ulaya. Check Ubungo interchange, Flyover ya TAZARA, Flyover zinazojengwa Uhasibu na Ile ya makutano ya barabara ya Keko, barabara nzuri ya Ocean road, ya Victoria na Mwenge zinazoendelea kukamilishwa, barabara nzuri Sana ya kuelekea Morogoro, Daraja LA Slender, mibarabara ya Mwendokasi hadi Mbagala, Treni ya Mwendokasi yaani SIPATI PICHA. nawasihi Sana tuendelee kuwaombea viongozi wetu wakamilishe Miradi hiyo. NAWASILISHA
Ww hata nairobi utakuwa haujafika. Eti ulaya ndogo. Kwanza mshughulikie mambo ya mafuriko. Maji taka. Uchafu wa jiji. Ufukwe ovyo. Umeme. Shule. Afya. Ajira kwa vijana. Kichwa chako kibovu kweli ww. Hayo ndio mambo ulaya imekuzidi tena mbali sana.
 
Back
Top Bottom