Hivi haya mabanda ya Machinga kila kona Dar wameshindwa kuyadhibiti?

Hivi haya mabanda ya Machinga kila kona Dar wameshindwa kuyadhibiti?

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,345
Reaction score
15,851
Nataka Dar iwe kama Ulaya.

Rais wetu alikua anasisitiza sana ila nahisi hawa watendaji wake hawamuelewi.

Wamachinga wameharibu uzuri wowote wa Dar ambao mtu angeufurahia kasoro tu eneo la jeshi lugalo ndio mtu ukipita unafurahia.

Flyover Ubungo ukigeuka tu pembeni ukiona mabanda ya machinga utam wote kwisha. Mlimani City ndio kabisaa ni takataka. Ukienda city centre maeneo ya kuanzia DIT mabanda kila kona hadi machizi wanalala humohumo.

Haya saizi Bagamoyo Road kuanzia Mwenge hadi Morocco pameanza kupendeza ila nawaambia soon uzuri wote unaisha machinga wanahamia. Hivi hizi mamlaka haziendi hata hapo nairobi tu zikajifunze vitu vidogo kama hivi? Ndio ulaya tutaifikia kweli?

Hatusemi biashara zisifanyike, ila tafuteni utaratibu sehem za uso wa barabara kuu zibaki zinavyopendeza. Au basi mtangaze maeneo yote ya mbele ya barabara kuu ni ya jeshi ili machinga waondoke wenyewe pabaki pazuri kama Lugalo.
 
Bila mabanda vijana wasio na ajira watafanya nini? Kuna nguvu kazi kubwa kuriko uchumi unavyoweza kuwatumia, nguvu kazi kubwa lakini uwezo wake unatumia kwa asilimia 5 tu,kila kijana anayeingia kwenye soko la kazi, lazima atatafuta Cha kufanya, apake rangi za kucha, auze leso mbili, atauza nyanya fungu mbili, atauza mahindi

Lakini ni shughuri ambazo hazikizi mahitaji yake muhimu, badala ya kuzalisha 100, uchumi unampa nafasi ya kuzalisha 10 tu, ndio hayo mabanda
 
Bila mabanda vijana wasio na ajira watafanya nini?Kuna nguvu kazi kubwa kuriko uchumi unavyoweza kuwatumia,nguvu kazi kubwa lakini uwezo wake unatumia kwa asilimia 5 tu,kila kijana anayeingia kwenye soko la kazi,lazima atatafuta Cha kufanya,apake rangi za kucha,auze leso mbili,atauza nyanya fungu mbili,atauza mahindi,
Lakini ni shughuri ambazo hazikizi mahitaji yake muhimu,badala ya kuzalisha 100,uchumi unampa nafasi ya kuzalisha 10,tu,ndio hayo mabanda
Serikali zote Duniani ndo zinavyo fanya? Kuwa hamasisha wafanya raia wao wafanye Uchuuzi?
 
Bila mabanda vijana wasio na ajira watafanya nini?Kuna nguvu kazi kubwa kuriko uchumi unavyoweza kuwatumia,nguvu kazi kubwa lakini uwezo wake unatumia kwa asilimia 5 tu,kila kijana anayeingia kwenye soko la kazi,lazima atatafuta Cha kufanya,apake rangi za kucha,auze leso mbili,atauza nyanya fungu mbili,atauza mahindi,
Lakini ni shughuri ambazo hazikizi mahitaji yake muhimu,badala ya kuzalisha 100,uchumi unampa nafasi ya kuzalisha 10,tu,ndio hayo mabanda
Hìi sio solution. Watu kuweka mabanda mabaya barabarani sehemu ya wapita njia haiwasaidii lolote. Tena wengi wao watakuwa wanafanya shughuli haramu ili kukidhi mahitaji yao, huwezi kuishi kwa kuuza dodoki barabarani.

Bora watengewe maeneo ya masoko kwasababu kama ni sokoni watu wataenda tu kwa wingi na faida watakayopata itakuwa kubwa zaidi.
 
Kariakoo wametapakaa hadi sehemu za wapita njia, watembea kwa miguu sasa inabidi tubanane kwenye barabara kuu. Makonda alianza kuwatoa barabarani baadae akapigwa stop.
Barabara ya Uhuru toka Ilala boma mpaka stesheni hakuna njia za waenda kwa miguu.sehemu zao zote wameweka vimeza vyao.harafu wanajua kujenga hivyo vimeza vinatosha kabisa.Kilichofanyika sasa waenda kwa miguu wanapita barabarani wanahatarisha maisha mbaya sana.

Halafu vile vibajaji mataa ya msimbazi na uruhu ni kero nyingine kabisa. Ukipita town mamlaka za majiji zimeishia kushika wrong parking za wastaarabu wenye magari tu.
 
Ukiwa unakula bure au amemaliza tu chuo na kupata ajira huwa mnaona Maisha rahisi Sana na unakuja na viushauri vya kipuuzi na unasahau kuwa Kuna wenzako toka wamalize chuo hawajapata hata laki tano na imeshapita miaka kumi.

Huku tunakotafuta ridhiki Kuna Mambo mengi Sana nakushauri inakusaidia nini kupendeza usoni wakati huna uhakika wa Kula. Pakishapendeza hapo Morocco panawasaidia nini walala hoi .Acha ujinga Watu wanaishi maisha duni Sana na wanatafuta wateja popote walipo wamuuzie angalau hata pipi na karanga ili apate faida ya kupata kununua unga ale na wanae.

Siku ukimuona mama kabeba mtoto mgongoni na kajitisha beseni anauza mihogo au dizi ujue huyo anatafuta hela ya Kula tu siyo kufanikiwa. Acha dharau kwakuwa hujawahi lala njaa waliwahi kusota ndiyo waliowaruhusu hao Watu wafanye biashara maana wanajua nini maana ya njaa.
 
Walishaambiwa wasisumbuliwe wafanye popote na hivi karibuni watapewa vitumbulisho kuhalalisha kabisa....hakuna mkuu WA mkoa atakayewatoa..... Badae wakitaka kuwatoa itakuwa ngumu sana...Naona wameanza kujivuta flyover ubungo pale chini. ..... Samaki mkunje angali mbichi..
 
Hatari hawa wanaopika vyakula bila kuzingatia Afya .Nearly wasiwasi Raia wengi kuambukizwa ugonjwa wa ini yani Hepatitis.
Acha upuuzi wako tumekula Hivyo vyakula toka miaka hiyo na hakuna ugonjwa wa inni .ebu fika pale cbe,Ifm, kila kichochoro wamejaa mama lishe na mazingira hayohayo lakini tumepata wachumi safi na wahasibu na hakuna Cha inni wala kipindupindu.

Yaani Leo umepata ajira umesahau kuwa ilikuwa unasotea Mihongo au ugali maharage wa buku pale kando ya barabara na hukuumwa inni wala nini. Ushauri wako upuuzi mtupu.Wakati huu wa Magufuli hakuna hata usafi wowote ulioglfanyika jijini lakini hakuna ugonjwa wa kipindupindu kwanini hajajiuliza Jambo Kama Hilo unajifanya utaumwa inni.

Amka wewe Karne na Karne wazee wameishi Hivyo na wakiendelea kuzaliana tu.
 
Walishaambiwa wasisumbuliwe wafanye popote na hivi karibuni watapewa vitumbulisho kuhalalisha kabisa....hakuna mkuu WA mkoa atakayewatoa..... Badae wakitaka kuwatoa itakuwa ngumu sana...Naona wameanza kujivuta flyover ubungo pale chini. ..... Samaki mkunje angali mbichi..
Kwakuwa unakula bure unaona Kama maisha rahisi Sana !!!!. Mpuuzi wewe utamkunja samaki ambaye ameshaoza unafikiri atakunjika hapo atamwagika tu.
 
Kwa kweli hawa ndugu zetu ni kweli wanakitaftia kipato kwa ajili ya kuendesha familia lakini hawajawekewa utatatibu mzuri. Cha kushangaza wanaziba hadi njia za watembea kwa miguu ambao ndio wateja.

Kwa kweli serikali inatakiwa kuweka utaratibu mzuri ili kila kitu kiende kwa utaratibu mzuri.
 
Barabara ya Uhuru toka Ilala boma mpaka stesheni hakuna njia za waenda kwa miguu.sehemu zao zote wameweka vimeza vyao.harafu wanajua kujenga hivyo vimeza vinatosha kabisa.Kilichofanyika sasa waenda kwa miguu wanapita barabarani wanahatarisha maisha mbaya sana.Halafu vile vibajaji mataa ya msimbazi na uruhu ni kero nyingine kabisa.ukipita town mamlaka za majiji zimeishia kushika wrong parking za wastaarabu wenye magari tuu
Pamoja na yote hayo hakuna aliyegongwa na gari na maisha yanasonga tu Watu wanapiga hela na Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Uchumi Kama hapa Tz IFM na CBE kutoka Mozambiq na Angola wanakuja kujifunza huo mfumo wa Uchumi na kuupeleka kwao wewe bado unabwabwaja tu huna unalolijua .
 
Back
Top Bottom