Hivi haya mabanda ya Machinga kila kona Dar wameshindwa kuyadhibiti?

Hivi haya mabanda ya Machinga kila kona Dar wameshindwa kuyadhibiti?

Kwa kweli hawa ndugu zetu ni kweli wanakitaftia kipato kwa ajili ya kuendesha familia lakini hawajawekewa utatatibu mzuri. Cha kushangaza wanaziba hadi njia za watembea kwa miguu ambao ndio wateja.
Kwa kweli serikali inatakiwa kuweka utaratibu mzuri ili kila kitu kiende kwa utaratibu mzuri.
Mkubwa kasema baadhi ya mitaa ifungwe kabisa Watu wapige hela Sasa wachumi wa jiji wameona Bora wasifunge Ila tupite hivyohivyo kwa kubanana Ila Watu wapare ridhiki.
 
Ndugu ni nchi nzima....Ni aibu...miji yote ni michafu....

Arusha ni balaa tupu...ni aibu....
Aibu kwa Nani ? Unayemuonea aibu ni Nani? Wakati huko dunia ya kwanza Homeless/ machokoraa wamejaa kibao hawajui hata watakula Nini watalala wapi Sasa aibu unamuonea Nani? Acha Watu wapige hela.
 
Kwa kweli taswira ya jiji imeharibika sana. Sokoine drive mbele ya Mahakama ya Rufaa, Kempiski hotel mpaka feri kuna mabanda machafu sana. Watu wanapanga mafungu ya bamia na matembele kwenye njia ya waenda kwa miguu.

Hata kama ni haki ya Wajasiriamali kufanya biashara. Si busara kuchafua kila mahali kwa mabanda na hasa mji mkongwe(maeneo ya posta) bora kuwe na sehemu yao maalum.

Mama lishe pia wanapika kwa kuni kila sehemu mjini kati. Lazima kuwe na udhibiti.
 
Hìi sio solution. Watu kuweka mabanda mabaya barabarani sehemu ya wapita njia haiwasaidii lolote. Tena wengi wao watakuwa wanafanya shughuli haramu ili kukidhi mahitaji yao, huwezi kuishi kwa kuuza dodoki barabarani.
Bora watengewe maeneo ya masoko kwasababu kama ni sokoni watu wataenda tu kwa wingi na faida watakayopata itakuwa kubwa zaidi.
Exactly na ndio tunachosema kama wanaruhusiwa mabanda basi isiwe kila mahali natena yawe same standard kama vile vibanda vya askari vya Asas hata ukiweka kinapendeza. Au waruhusiwe maeneo baadhi kama buguruni,manzese etc othewise wajenge masoko
 
Kwa kweli taswira ya jiji imeharibika sana. Sokoine drive mbele ya Mahakama ya Rufaa, Kempiski hotel mpaka feri kuna mabanda machafu sana. Watu wanapanga mafungu ya bamia na matembele kwenye njia ya waenda kwa miguu.

Hata kama ni haki ya Wajasiriamali kufanya biashara. Si busara kuchafua kila mahali kwa mabanda na hasa mji mkongwe(maeneo ya posta) bora kuwe na sehemu yao maalum.

Mama lishe pia wanapika kwa kuni kila sehemu mjini kati. Lazima kuwe na udhibiti.
Yaani mkuu inatia kinyaa aisee ukiangalia miundombinu inavyopendeza mfano pale mahakama ya rufaa hadi feri lakini mauchafu ya yale mabanda mpaka mtu unajiuliza kama hawa viongozi wanatembeaga hata nchi za jirani tu kujifunza.
 
Ukiwa unakula bure au amemaliza tu chuo na kupata ajira huwa mnaona Maisha rahisi Sana na unakuja na viushauri vya kipuuzi na unasahau kuwa Kuna wenzako toka wamalize chuo hawajapata hata laki tano na imeshapita miaka kumi. Huku tunakotafuta ridhiki Kuna Mambo mengi Sana nakushauri inakusaidia nini kupendeza usoni wakati huna uhakika wa Kula. Pakishapendeza hapo Morocco panawasaidia nini walala hoi .Acha ujinga Watu wanaishi maisha duni Sana na wanatafuta wateja popote walipo wamuuzie angalau hata pipi na karanga ili apate faida ya kupata kununua unga ale na wanae. Siku ukimuona mama kabeba mtoto mgongoni na kajitisha beseni anauza mihogo au dizi ujue huyo anatafuta hela ya Kula tu siyo kufanikiwa. Acha dharau kwakuwa hujawahi lala njaa waliwahi kusota ndiyo waliowaruhusu hao Watu wafanye biashara maana wanajua nini maana ya njaa.
Mkuu unaakili ndogo sana....na umekurupuka hata hujaelewa mada...na inaonekana ww hata nchi ya jiran yoyote hujaenda....hebu vuka boda kidogo afu utajua watu wanavyofanya vitu kwa utaratibu. Usiwe na akili za bashite
 
Kwakweli hili linasikitisha sana jiji lote limekuwa slum sababu ya wamachinga, wafanyabiashara wanaolipa kodi kariakoo wanashindwa fanya biashara sababu ya hao wachuuzi. Mbaya zaidi kiuchumi hawana impact sababu sio wazalishaji ni ongezeko la wachuuzi tu ambao ni middle men, kodi hawalipi.

Kwakweli sekali inapaswa kulisimamia hili haiwezekani kuwa na mji hauna utaratibu yaani ukifika posta pale jengo la benjamin mkapa, jengo la mabilion watu wanakaanga mihogo barazani vibanda kila upande. Hivi watalii watakuja kweli kutalii slum city?
 
Walishaambiwa wasisumbuliwe wafanye popote na hivi karibuni watapewa vitumbulisho kuhalalisha kabisa....hakuna mkuu WA mkoa atakayewatoa..... Badae wakitaka kuwatoa itakuwa ngumu sana...Naona wameanza kujivuta flyover ubungo pale chini. ..... Samaki mkunje angali mbichi..

Basi serikali itumie hayo maeneo ya chini ya hayo madaraja Ubungo na Tazara kuweka maeneo sahihi ya matumizi ya wananchi wa kawaida, inawezekana sana!

IMG_3783.jpg

IMG_3782.jpg

IMG_3781.jpg
 
Nataka Dar iwe kama ulaya.
Rais wetu alikua anasisitiza sana ila nahisi hawa watendaji wake hawamuelewi.
Wamachinga wameharibu uzuri wowote wa Dar ambao mtu angeufurahia kasoro tu eneo la jeshi lugalo ndio mtu ukipita unafurahia. Flyover ubungo ukigeuka tu pembeni ukiona mabanda ya machinga utam wote kwisha. Mlimani city ndio kabisaa ni takataka. Ukienda city centre maeneo ya kuanzia DIT mabanda kila kona hadi machizi wanalala humohumo. Haya saizi bagamoyo road kuanzia mwenge hadi morocco pameanza kupendeza ila nawaambia soon uzuri wote unaisha machinga wanahamia. Hivi hizi mamlaka haziendi hata hapo nairobi tu zikajifunze vitu vidogo kama hivi? Ndio ulaya tutaifikia kweli? Hatusemi biashara zisifanyike, ila tafuteni utaratibu sehem za uso wa barabara kuu zibaki zinavyopendeza. Au basi mtangaze maeneo yote ya mbele ya barabara kuu ni ya jeshi ili machinga waondoke wenyewe pabaki pazuri kama lugalo.
Sasa jiwe mwenyewe ndio anataka iwe hivyo,tutafanyaje?
 
Mitano tenaa
 
Miji yote imekuwa takatakaa. Kila mahali mabanda kama kibera slums.

Aiseee ni pachafuuu! Miji inakuwa kama ya machokoraa!
Siasa hovyo sana kisa vitambulisho vya machinga wanaweka mabanda kila mahali aisee miji inachukiza kwakweli wawadhibiti wawe na maeneo baadhi tu ndo waruhusiwe kama manzese etc
 
Back
Top Bottom