Hadi leo najiuliza, ilikuwaje tukajenga SGR kwenda Burundi na kuacha kuboresha TAZARA kuwa SGR ambapo tungefika Congo kirahisi sana

Hadi leo najiuliza, ilikuwaje tukajenga SGR kwenda Burundi na kuacha kuboresha TAZARA kuwa SGR ambapo tungefika Congo kirahisi sana

hela hata sio nyingi ya kuliko kujenga, tungeweka tu line za nyaya za umeme na kuagiza train za umeme tuwe tunapiga dsm - mbeya kwa masaa manne, hadi zambia masaa 6, unaenda zambia na kurudi. kama kweli sisi tunaimiliki hiyo reli, kwanini hatuiboreshi?
Wabongo kwa kurahisisha mambo mko vizuri.
Reli ile haikusanifiwa kwa matumizi ya train ya mwendokasi mkubwa kama za umeme zitakazotumika kwenye SGR mpya.

Ile ina kona kubwa au niite kali hivyo mwendo ukiwa wa kasi train inaweza kupata ajali. Ubakumbuka mamambo ya banking system kwenye fizikia?
 
NI
Nijuavyo Mimi Reli ya Tazara Ni Standard Gauge Railway (SGR) ndio maana hata Train za South Africa huwa zinakuja kwa kutumia SGR ya Tazara kasoro ya Tazara sio Electrified Railway
Ni Cape gauge mkuu
 
Mimi hata sielewi mnachoongea kuhusu SGR kwenda Mwanza na Kigoma eti haina umuhimu> Ndugu zangu ulaya yote imeunganishwa kwa reli tena kama ningeukwaa urais wa nchi hii kitu cha kwanza ningeunganisha nchi nzima na railway network. Ningejenga reli ya kutoka Mbamba bay hadi Songea, Mtwara, Lindi, Kilwa hadi D'salaam. Ningejenga ile ya Tanga , Arusha , Musoma hadi Bukoba. Mwanza hadi Isaka na mikoa yote ya Tanganyika kungekuwa na vituo vya reli. Baada ya hapo ningeshughulikia shule na hospitali kila mkoa kuwa na hospitali ya rufaa na kila mkoa uwe na chuo kikuu japo kimoja. Baada ya hapo ni kuanzisha huduma za wastaafu wote hata mkulima kulipwa pensheni na kila mkoa kujenga nyumba za kuwalea wazee, vikongwe na maskini kwa gharama za serikali. Kila Mtanganyika akifikisha miaka 25 kama hajapata ajira ya kulipwa mshahara kima cha chini basi atalipwa posho ya kujikimu mpaka atakapopata kazi yaani 80% ya kima cha chini. Nipeni kura zenu
 
Kwa jinsi Malori yalivyajaa Tanzania sahau kuhusu reli kupewa kipaumbele.
Hizo ni hadaa za wanasiasa, za miaka nenda rudi, nenda UK, kunausafiri bora sana wa treni na malori ni mengi mno, ya kusafirisha mizigo.Mfano kwa hapa Tz, huo mfumo wa reli umesambaa kwa kiasi gani hadi malori yashindwe kufanya kazi?!!
 
Nijuavyo Mimi Reli ya Tazara Ni Standard Gauge Railway (SGR) ndio maana hata Train za South Africa huwa zinakuja kwa kutumia SGR ya Tazara kasoro ya Tazara sio Electrified Railway
Mkuu tazara sio stardand gauge haikidhi vigezo hivyo pia sio electified kama ulivyosema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afrika mtu akiwa cheti anafanya kazi na kujituma sana.

Akipata Diploma anaongeza juhudi na ubunifu na kufanya kazi Kwa uaminifu .

Akipata digrii Moja anafanya kazi Kwa majivuno.

Akipata mastars anafanya kazi Kwa majivuno na dharau. Akipata PhD anafanya kazi Kwa mikataba,vikao na kuangalia maslahi tuu.

Bila posho hafanyi kazi. Yaani PhD yake ni ya kupata mshahara mkubwa na marupurupu basi na anafanya kazi Kwa muda kidogo huku akisema kuwa afadhali Sasa napata mshahara mkubwa Kwa kazi kidogo,Tena ya kufanyiwa na walioko chini yake.

Akiwa Professor anaingia Jalalani na kuanza upya kama ombaomba mitaani ,tofauti yake ni kuwa ombaomba Kwa wakuu wenye kuweza kumtoa Jalalani na kumpa neema ya maisha Bora.

Mchezo unaishia hapo anakua ni mtu wa kusifu na kuabudu wanadamu wenzake Tena wenye Elimu ndogo kuliko yeye.

Usitegemee wasomi na watawala wa afrika wafanye jambo lenye maslahi mapana Kwa Taifa zaidi ya kuangalia matumbo yao. Miradi mikubwa Ina pesa nyingi sana za wizi.

Kila mtawala anawaza miradi mipya na kutelekeza miradi iliyoko tayari na inayozalisha. Mfano Mradi wa gesi.

Wapya walikuja wakautelekeza mradi wa gesi na kuturudisha wanakotaka wao kisa walituaminisha kuwa mradi wa gesi una ifisadi lakini hawawachukulii hatua hao waliofanya ifisadi.

Reli ya TAZARA ni standard G Railwas imekosa umeme tu kuendesha train ya umeme.
Reli ya tazara sio stardand gauge ni cape gauge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijuavyo Mimi Reli ya Tazara Ni Standard Gauge Railway (SGR) ndio maana hata Train za South Africa huwa zinakuja kwa kutumia SGR ya Tazara kasoro ya Tazara sio Electrified Railway
Sawa upo sahihi lakini ya TAZARA ni 3ft 6 in gauge ambayo inaelekea kupitwa na wakati sasa na kwa jina maarufu ikijulikana kama Cape Gauge Railway. Na hii ya reli ya kati ndio the modes one 4ft 8.5 gauge almaarufu kama Standard Gauge Railway.
Swali la mtoa mada ni kwanini serikali isingeiboresha reli ya TAZARA kuwa the modest SGR?
 
Hapa kwenye Tazara naitetea serikali,wakati wa awamu ya rais magufuli walikubaliana kila nchi kuchanga 10Bilion ili kufufua injini zilizokuwa zimekufa ambazo kwa Tanzania nyingi ziko Mbeya pale Iyunga.Serikali ya Tanzania ilitoa hela na zikafufuliwa Engine 7 lakini Zambia hawakutoa.Na mkumbuke kila kinachowekezwa kinakuwa mali ya nchi mbili.Sasa mnataka serikali itoe tuu hela ya walipa kodi wakati Zambia hawajihangaishi kugharamia hii reli? Mkataba unaipa nguvu Zambia sana kuliko sisi kwanza Mkurugenzi mkuu lazima atoke Zambia hili marehemu alipambana baadhi ya vipengele vibadilishwe ikiwemo hata la mkurugenzi awe mtu yeyote yule mwenye uwezo.Jambo lingine ni kila nchi iweze kuendeleza kipande chake au kwa maana nyingine Tanzania inaweza kununua Engine au Mabehewa yakawa yake yenyewe.Kwa jinsi ilivyo sasa kila ukinunua kitu ni mali ya nchi 2.Hata hivyo serikali inajitahidi sana ndio maana hata ile migomo ya wafanyakazi imekwisha tazara.
Tunachotaka kama zambia wamesusa TZ ije na mkakati mpya wa kuiendesha TAZARA bila kuishirikisha zambia na dg awe mtz na siyo mzambia. Na pia ijengwe reli kutoka tunduma kwenda bandari ya kasanga. Mizigo ya drc ipitie bandari ya kasanga ikiwezekana kama kuipitishia zambia ni shida.
 
Kasanga port huwa mnaizungumzia kwa faida ipi hasa? Mnaelewa hata jiografia ya eneo kweli?
kasanga port ni kwa ajili ya southern drc, jimbo kubwa la katanga-lubumbashi na majimbo mengine yaliyo kusini mwa jimbo la Tanganyika nchini drc. Inaonekana japo unadai hatujui jiografia wewe ndiyo bure kabisa hujui lolote
 
  • Thanks
Reactions: Cyb

Narudia tena kukuuliza unajua jiografia vizuri? Yaani uache kupitia Tunduma kwenda Lubumbashi uke kupitia Kasanga?

Jimbo la Katanga na kasanga port wapi na wapi? Kwa taarifa yako sasa bandari ya Kasanga na barabara vimekamilika toka 2020 na hakuna kinachofanyika cha maana.
 
nami bado ninakuuliza, unaijua jiografia ya drc? usielekeze akili yako kwa mji wa lubumbashi tu. DRC ni zaidi ya Lubumbashi. Elekeza akili yako drc kupitia tazara lakini ukweli ni kuwa iko drc nyingine ambayo inahudumiwa na bandari ndogo ndogo kama ya kasanga, kipili na kalema.

Acha ligi ya kipu.mbavu. tafuta atlas ujiongezee maarifa
 
Zote ni SGR utofauti upo kwenye ukubwa wa mataluma na electrification tu. Iliitwa Cape Gauge kwasababu ilianzia huko British Empire chini ya Cape government.
Acha kupotosha watu mkuu, kwanza kabisa cape gauge haijaanzia british empire, bali Norway.

Pia rail track hazipewi majina kwa kua zimeanzia sehemu flani bali ni upana wa njia yake ( track gauge).

1,435 mm (4 ft 8+1⁄2 in) standard gauge,
1,000 mm (3 ft 3+3⁄8 in) metre gauge.( Reli ya kati)
Cape gauge (3 ft 6 inches). Tazara.

Pia reli haitaji kua electified ili kuitwa stardand gauge ila ni track gauge pekee ndio hutofautisha reli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabongo kwa kurahisisha mambo mko vizuri.
Reli ile haikusanifiwa kwa matumizi ya train ya mwendokasi mkubwa kama za umeme zitakazotumika kwenye SGR mpya.

Ile ina kona kubwa au niite kali hivyo mwendo ukiwa wa kasi train inaweza kupata ajali. Ubakumbuka mamambo ya banking system kwenye fizikia?
kama ulishawahi kupanda tazara utaelewa nini tumemaanisha kwamba hela sio nyingi. hii ni kwasababu hapatakuwa na kazi ya kutoboa milima tena na yale mahandaki ambayo huwa tunaingia na train, yalishatobolewa. itakuwa kazi ni kutandaza tu reli mpya na nyaya za umeme. gharama itapungua, hakuan kuchoronga milima. ulishawahi kupanda tazara?
 
Siku Saba zilizopita shirika la habari la Ujerumani DW wametoa makala nzuri sana kuelezea upekee wa Reli ya Tazara inayotoka Tanzania hadi Ndola nchini Zambia.

Wameelezea upekee wa reli hii na namna inavyopita kwenye mbuga maarufu za Selous na Mikumi na inavyopita mwenye milima ya Iringa hadi kuingia Zambia.

Waandaaji wa Makala hii wamehoji sana uchakavu wa reli hii na namna ambavyo serikali za nchi zetu zimeipuuza na kiufanya ichakae sana na kutoleta matunda yaliyokusudiwa!

Baada ya kuiona Makala hii nimegundua kuwa Reli ya Tazara inafika hadi Zambia ambapo Kuna urefu wa kilomita chache sana Kwenda Congo ambazo Pia zimeunganishwa na reli nyingine Kwenda Congo, Mji wa Lubumbashi ambao ni mji Mkuu wa kibiashara.

Kwa ninavyojua reli ya kati kwa Kiwango cha SGR mpaka mwanza na Kigoma itagharimu kiasi cha Trilioni si chini ya 25 kwa ujumla wa vipande vyote.

Jambo lililonishangaza ni kuwa tayari Reli ya Tazara inafika hadi Ndola Zambia na kuna Reli nyingine inafika hadi Lubumbashi , Congo kutoka Zambia.

Je haikuwa sahihi kwetu kuboresha Reli ya Tazara kwa Kiwango cha SGR na kuiwekea umeme na kuongea na Zambia kidiplomasia tukawakopesha hela za kuboresha reli kutoka Zambia hadi Lubumbashi Congo kwa Kiwango cha SGR?

Kwa mtazamo wangu naona gharama za kuboresha Reli ya Tazara kwenda Congo kwa Kiwango cha SGR ingekuwa ndogo sana kuliko kuijenga upya hadi Burundi na kuanza kuongea na Burundi ili waifikishe Congo jambo ambalo sidhani kama litakamilika hivi karibuni kutokana na hali ya kiuchumi ya Burundi! Na uhohehae wao kutokana na vita!

Nauliza swali hili kwenu wadau! Je kulikuwa na haja Kweli ya kujenga Reli ya SGR kwenda Kigoma na Mwanza? Au Tungeboresha tu TAZARA kuwa Kiwango cha SGR ambapo tungetumia gharama ndogo na kufika Congo kirahisi sana?

Hii ndo ramani ya Zambia inavyoonesha ukaribu wa Zambia na Lubumbashi Congo na urahisi wa kufika Congo kupitia reli ya TAZARA

Mkuu Magufuli interest yake ilikuwa kwso na kabila lake.
Barabara nyingi zaidi zimejengwa kanda ya ziwa na Central kuliko kwingine kokote.
Daraja la Busisi na Chato International Airport ndio vielelezo vya mawazo hasi ya Magufuli.

TAZARA na mkoa haswa wa Mbeya ulisuswa kwa muda mrefu .
Hatujui kwa sasa Samia ana mpango upi.
 
kama ulishawahi kupanda tazara utaelewa nini tumemaanisha kwamba hela sio nyingi. hii ni kwasababu hapatakuwa na kazi ya kutoboa milima tena na yale mahandaki ambayo huwa tunaingia na train, yalishatobolewa. itakuwa kazi ni kutandaza tu reli mpya na nyaya za umeme. gharama itapungua, hakuan kuchoronga milima. ulishawahi kupanda tazara?
Sahihi kabisa! Kama tungebadirisha TAZARA kuwa SGR kusingekuwa na gharama kubwa za kuchoronga milima au kujenga upya madaraja mengine mapya ambapo ndo gharama zipo
 
Mkuu Magufuli interest yake ilikuwa kwso na kabila lake.
Barabara nyingi zaidi zimejengwa kanda ya ziwa na Central kuliko kwingine kokote.
Daraja la Busisi na Chato International Airport ndio vielelezo vya mawazo hasi ya Magufuli.

TAZARA na mkoa haswa wa Mbeya ulisuswa kwa muda mrefu .
Hatujui kwa sasa Samia ana mpango upi.
Kinachonishangaza hasa ndo icho!
Southern Corridor kuelekea Zambia ni strategic zaidi kuingia Congo tena kwa gharama ndogo sana kuliko kupitia Burundi maana tayari Zambia kuna miundombinu ya Reli kuelekea Congo hasa Lubumbashi ambayo ndo business capital ya Congo.

Kupitia Kalema still tutahitaji Maboresho makubwa ya Bandari ya kalemii upande wa Congo ili nao wawe na Bandari ya Kiwango chetu ili tuweze kupakia mizigo ya maana! Same kupitia Burundi inahitajika investment Kubwa kufanywa na Burundi na Congo kwa upande wao ili hii Reli ya sasa ya SGR kuweza kuingia kwao.

Sina uhakika Kama wataweza kukamilisha huu mradi kwa sasa maana kwa hali ya Uchumi ya nchi za Congo na Burundi sidhani kama zinaweza kujenga Reli tena ya umeme na kuihumuia kwa sasa
 
Back
Top Bottom