Hadi leo najiuliza, ilikuwaje tukajenga SGR kwenda Burundi na kuacha kuboresha TAZARA kuwa SGR ambapo tungefika Congo kirahisi sana

Ulitaka Tanzania tukajenge tazara huko kampirimposhi Zambia,je,kama wazambia hawajakubali?
Hili tu la malori yanayopita Zambia Kwenda DRC Kila siku Kuna figisu Toka Kwa wazambia!
Wanataka malori yalifika mpakani madereva wao wapewe Kazi.
 
Kwani Rwanda na Burundi Hakuna matatizo ya Malori yetu kuzuiwa?
 
Mradi wa sgr umetutia madeni. Halafu mradi ukikamilika utatutia madeni zaidi. Pia ramani ya mradi imekosewa. Reli ya sgr inatakiwa iende sehemu ya mizigo mingi. Na mizigo mingi ni shaba ya Zambia, na madini ya cobalt na shaba yaliyopo Lubumbashi/kolwezi/katanga DR Congo.

Sasa hii reli naona imepotea uelekeo wa mizigo mingi mno kwa hiyo haitarudisha hela. Kwa hiyo ni madeni juu ya madeni halafu riba. Mizigo mingi ipo kusini kwa Congo na Zambia. Halafu reli inaelekea mashariki mwa Congo

Hao Rwanda na Burundi hawana mzigo wa maana kuzidi Zambia na Cobalt na Copper ya Drc congo. Ilitakiwa SGR iende kwenye mizigo ya maana huko kwenye migodi ya zambia na Congo.

Hii sgr inayojengwa imekosewa kabisa. SGR ilitakiwa iwe Dar-Kapirimposhi-Lubumbashi(ikiwezekana ipite kwenye migodi ya Copper na Cobalt iliyopo Kolwezi, Mutanda huko Drc ndanindani
 
Siku Saba zilizopita shirika la habari la Ujerumani DW wametoa makala nzuri sana kuelezea upekee wa Reli ya Tazara inayotoka Tanzania hadi Ndola nchini Zambia.

Wameelezea upekee wa reli hii na namna inavyopita kwenye mbuga maarufu za Selous na Mikumi na inavyopita mwenye milima ya Iringa hadi kuingia Zambia.

Waandaaji wa Makala hii wamehoji sana uchakavu wa reli hii na namna ambavyo serikali za nchi zetu zimeipuuza na kiufanya ichakae sana na kutoleta matunda yaliyokusudiwa!

Baada ya kuiona Makala hii nimegundua kuwa Reli ya Tazara inafika hadi Zambia ambapo Kuna urefu wa kilomita chache sana Kwenda Congo ambazo Pia zimeunganishwa na reli nyingine Kwenda Congo, Mji wa Lubumbashi ambao ni mji Mkuu wa kibiashara.

Kwa ninavyojua reli ya kati kwa Kiwango cha SGR mpaka mwanza na Kigoma itagharimu kiasi cha Trilioni si chini ya 25 kwa ujumla wa vipande vyote.

Jambo lililonishangaza ni kuwa tayari Reli ya Tazara inafika hadi Ndola Zambia na kuna Reli nyingine inafika hadi Lubumbashi , Congo kutoka Zambia.

Je haikuwa sahihi kwetu kuboresha Reli ya Tazara kwa Kiwango cha SGR na kuiwekea umeme na kuongea na Zambia kidiplomasia tukawakopesha hela za kuboresha reli kutoka Zambia hadi Lubumbashi Congo kwa Kiwango cha SGR?

Kwa mtazamo wangu naona gharama za kuboresha Reli ya Tazara kwenda Congo kwa Kiwango cha SGR ingekuwa ndogo sana kuliko kuijenga upya hadi Burundi na kuanza kuongea na Burundi ili waifikishe Congo jambo ambalo sidhani kama litakamilika hivi karibuni kutokana na hali ya kiuchumi ya Burundi! Na uhohehae wao kutokana na vita!

Nauliza swali hili kwenu wadau! Je kulikuwa na haja Kweli ya kujenga Reli ya SGR kwenda Kigoma na Mwanza? Au Tungeboresha tu TAZARA kuwa Kiwango cha SGR ambapo tungetumia gharama ndogo na kufika Congo kirahisi sana?

Hii ndo ramani ya Zambia inavyoonesha ukaribu wa Zambia na Lubumbashi Congo na urahisi wa kufika Congo kupitia reli ya TAZARA

Naunga mkono hoja. Kwa mwaka 2017/18, jumla ya tani 5.6 million zilipitia Tanzania (bandari ya Dar es Salaam pekee) kwenda au kutoka nchi za jirani, ikilinganishwa na tani 4.8 million mwaka 2016/17. Hili ni ongezeko la asilimia 17.1 na ni habari njema kabisa kwa TPA na nchi yetu kwa ujumla.

Ukiangalia mchanganuo wa shehena zinazoenda au kutoka nchi za jirani, asilima 61.1% ni za Zambia (36.6%) na J.D. Kongo (24.4%). Hii ni zaidi ya tani 3.4 million ambazo kwa asilimia kubwa zinawafikia jirani zetu kupitia barabara zetu hapa Tanzania. Ukipitia takwimu za 2017/18, TAZARA imefanikiwa kusafirisha mizigo ya tani 187,558 tu (3.4% ya 5.6 million) kwa njia ya reli.

Shehena za Rwanda ni asilimia 16.5% pekee (au tani 922,134) kwa mwaka wa 2017/18. Ukilinganisha na 2016/17, kuna upungufu wa 9.0% - kitu ambacho kinaashiria kuwa mizigo ya Rwanda inawezekana kuwa inapitia Kenya na Uganda.

Kwa kutumia akili za kawaida (common sense), kuna haja ya kuwekeza reli ya SGR kuunganisha Tanzania na Zambia na J.D. Kongo kwa sababu business case (volume of cargo) ni kubwa mno (kwa mara 3.7) kuliko Rwanda. Pia, tukiweza kuondoa hata tani 2 million barabani, TANROADS watapumua kidogo na matengenezo ya kila mara yanayotokana na uharibifu wa baraba zetu. Hii ni kwa mujibu ya data za NBS na TPA wenyewe.
 
Umeniongezea madini sana kichwani kwangu. Asante sana
 
Umemaliza kila kitu Mkuu. Asante sana
 
Acha kupotosha watu mkuu, kwanza kabisa cape gauge haijaanzia british empire, bali Norway.

Pia rail track hazipewi majina kwa kua zimeanzia sehemu flani bali ni upana wa njia yake ( track gauge).

1,435 mm (4 ft 8+1⁄2 in) standard gauge,
1,000 mm (3 ft 3+3⁄8 in) metre gauge.( Reli ya kati)
Cape gauge (3 ft 6 inches). Tazara.

Pia reli haitaji kua electified ili kuitwa stardand gauge ila ni track gauge pekee ndio hutofautisha reli.

Sent using Jamii Forums mobile app

..asante sana kwa soma hili zuri.

..Watz tangu wasikie kuhusu Standard Gauge Rail hawataka kusikia chochote kuhusu reli za gauge nyingine.

..Binafsi siamini kama Tazara haifanyi vizuri kwasababu ni Cape Gauge rail. Na kwamba ikibadilishwa na kuwa Standard Gauge matatizo yaliyopo yatatoweka.

..Pia sioni mantiki ya kupeleka reli ya SGR katika nchi ambazo reli zake ni Cape Gauge. Nchi zote za kusini mwa Afrika zinatumia Cape Gauge na hiyo ndiyo sababu ya Tazara kuwa Cape Gauge.

..Mwisho, miaka ya karibuni Angola waliijenga upya reli yao na wanatumia Cape Gauge.
 
Siku Saba zilizopita shirika la habari la Ujerumani DW wametoa makala nzuri sana kuelezea upekee wa Reli ya Tazara inayotoka Tanzania hadi Ndola nchini Zambia.

Wameelezea upekee wa reli hii na namna inavyopita kwenye mbuga maarufu za Selous na Mikumi na inavyopita mwenye milima ya Iringa hadi kuingia Zambia.

Waandaaji wa Makala hii wamehoji sana uchakavu wa reli hii na namna ambavyo serikali za nchi zetu zimeipuuza na kiufanya ichakae sana na kutoleta matunda yaliyokusudiwa!

Baada ya kuiona Makala hii nimegundua kuwa Reli ya Tazara inafika hadi Zambia ambapo Kuna urefu wa kilomita chache sana Kwenda Congo ambazo Pia zimeunganishwa na reli nyingine Kwenda Congo, Mji wa Lubumbashi ambao ni mji Mkuu wa kibiashara.

Kwa ninavyojua reli ya kati kwa Kiwango cha SGR mpaka mwanza na Kigoma itagharimu kiasi cha Trilioni si chini ya 25 kwa ujumla wa vipande vyote.

Jambo lililonishangaza ni kuwa tayari Reli ya Tazara inafika hadi Ndola Zambia na kuna Reli nyingine inafika hadi Lubumbashi , Congo kutoka Zambia.

Je haikuwa sahihi kwetu kuboresha Reli ya Tazara kwa Kiwango cha SGR na kuiwekea umeme na kuongea na Zambia kidiplomasia tukawakopesha hela za kuboresha reli kutoka Zambia hadi Lubumbashi Congo kwa Kiwango cha SGR?

Kwa mtazamo wangu naona gharama za kuboresha Reli ya Tazara kwenda Congo kwa Kiwango cha SGR ingekuwa ndogo sana kuliko kuijenga upya hadi Burundi na kuanza kuongea na Burundi ili waifikishe Congo jambo ambalo sidhani kama litakamilika hivi karibuni kutokana na hali ya kiuchumi ya Burundi! Na uhohehae wao kutokana na vita!

Nauliza swali hili kwenu wadau! Je kulikuwa na haja Kweli ya kujenga Reli ya SGR kwenda Kigoma na Mwanza? Au Tungeboresha tu TAZARA kuwa Kiwango cha SGR ambapo tungetumia gharama ndogo na kufika Congo kirahisi sana?

Hii ndo ramani ya Zambia inavyoonesha ukaribu wa Zambia na Lubumbashi Congo na urahisi wa kufika Congo kupitia reli ya TAZARA

Sasa mtafahamu kwa nini SGR imeanzia Kanda ya ziwa badala ya Kigoma (Uganda/Rwanda/Burundi) Vs DRC.
Screenshot_20220722-203601.jpg
 
Waulize Sukuma gang
 
Naoona mama kaamua kuanza na barabara ya Igawa-Tunduma.
Tumeona tender note ya TANROADS magazetini.
Ila kwa TAZARA , mama Samia sijui itakuwa mfupa uliowashinda wengI?
 
SGR haiendi Uganda!
Inaishia Mwanza!

Kama target ni Congo , kulikuwa na haja gani kuipeleka Burundi na Rwanda tena kwa gharama kubwa sana?

Kwa nini tusingeboresha TAZARA na kufika Congo kirahisi sana?
Target congo ya Kati na kaskazini kupitia Burundi na ziwa tanganyika.historia inaonyesha usumbufu Ni mwingi kwa mizigo inayopitia Zambia hawatabiriki Kama Rwamda.Kongo,Burundi na Tanzania walishakubaliana wameshasaini. makubaliano .Rwanda pia wamo .uimarishaji wa bandari kongo na Tanzania ziwa Tanganyika Lengo mizigo ya ishuke sehemu mbalimbali kongo bila kupitia nchi ya Kati.
TAZARA lazima Zambia wakubali so sio rahisi kufikua malengo yetu
 
Ushauri umefanyiwa kazi

Rais wa JMT amezungumza hili na Rais wa Zambia na wamekubaliana kuanza kuifanyia kazi Reli ya Tazara na kuibadilisha kuwa SGR

Tunashukuru kuona kumbe Rais anapitia sana JF na kusoma mawazo mazuri ya members wa humu na kuyafanyia kazi

Kongole kwenu JF kwa kulifanya jukwaa hili kuwa hivi na sasa linatumika kama Think tank ya Taifa
 
Reli ya TAZARA sio kiunganishi cha EAC kama ilivyo reli ya TRC
 
TRC imeishia Kigoma na Mwanza ziwa Victoria. Haijafika hata Burundi, Rwanda na Uganda. Sasa inaunganishaje East Africa?

Pili kama mpango ni kufika DRC kupitia Burundi kiukweli kwa hali ya kiuchumi na kiusalama Burundi, sioni Reli ya SGR TRC tunayojenga ikifika Congo this soon! May be after 30 years
 
Reli ya kati ilijengwa kwa lengo hilo hapo awali, haikuweza kugusa mipaka tu ya majirani lakini vilibakia vipande kidogo...

Kigoma ilikuwa iunge Burundi na DRC kupitia ziwa Tqnganyika...Arusha ilikuwa iunge Kenya...Mwanza iunge na Uganda kupitia ziwa Victoria...

Baada ya kuibuka kwa EAC kwa upya, mpango makakati wa TZ umekuwa ni kuiboresha hiyo reli kwa kujenga SGR, ili tena kuziunga hizo nchi na bandari ya Dar

TAZARA ingeziunga chi za Zambia, pengine na Malawi ambazo hazipo EAC...
 
TRC imeishia Kigoma na Mwanza ziwa Victoria. Haijafika hata Burundi, Rwanda na Uganda. Sasa inaunganishaje East Africa?

Pili kama mpango ni kufika DRC kupitia Burundi kiukweli kwa hali ya kiuchumi na kiusalama Burundi, sioni Reli ya SGR TRC tunayojenga ikifika Congo this soon! May be after 30 years
Reli ya TRC inafika Uganda kupitia meli zenye Reli, ni rahisi kukuta locomotive za TRC Uganda au Kenya na usishangae. Kenya wana Mv. Uhuru, Tanzania Mv. Umoja na Uganda wanazo Mv. Pamba na Kahawa. Hizo meli ndio zinazounganisha East Africa railway kupitia ziwa Victoria.

Kenya sasa wanaongeza meli nyingine Mv. Uhuru II. Na Tanzania wanampango wa kuongeza meli ya aina hiyo hiyo yenye Reli ndani. Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika. Hiyo ya ziwa Tanganyika itaunganisha Reli ya Tanzania na Reli ya DRC kupitia ziwa Tanganyika.
 
Very bold

Siasa inapeleka sgr kwenda Rwanda na burundi nchi ambazo hazina zinacho exoprt
Sgr.

Hata ikifika huko itakuwa inarudi na mabehewa empy kama maroli ya rwanda, burundi ,shinyanga na mwanza yanavyorudi Dar.
We kaa tuu chalinze pale au morogoro, maroli tote yanaotoka rwanda yapo empty nyuma kule ni asala tupu
 
Back
Top Bottom