Hadi leo najiuliza, ilikuwaje tukajenga SGR kwenda Burundi na kuacha kuboresha TAZARA kuwa SGR ambapo tungefika Congo kirahisi sana

Hadi leo najiuliza, ilikuwaje tukajenga SGR kwenda Burundi na kuacha kuboresha TAZARA kuwa SGR ambapo tungefika Congo kirahisi sana

Hakuna nchi ambayo ina mzigo wa kuleta bandari ya dar
Burundi ,Rwanda hazina cha ku export ambacho kitakuwa na significant effect.

Tazara ndo ilikuwa reli ya kuitegemea kwa ajili ya kuiweka busy dar port.

Congo wakiamua kisafirisha magogo tu,. Wanaeza kuiweka busy Tazara railway
Mizuho mingi ya congo yanapitia Katavi na sumbawanga
 
Siku Saba zilizopita shirika la habari la Ujerumani DW wametoa makala nzuri sana kuelezea upekee wa Reli ya Tazara inayotoka Tanzania hadi Ndola nchini Zambia.

Wameelezea upekee wa reli hii na namna inavyopita kwenye mbuga maarufu za Selous na Mikumi na inavyopita mwenye milima ya Iringa hadi kuingia Zambia.

Waandaaji wa Makala hii wamehoji sana uchakavu wa reli hii na namna ambavyo serikali za nchi zetu zimeipuuza na kiufanya ichakae sana na kutoleta matunda yaliyokusudiwa!

Baada ya kuiona Makala hii nimegundua kuwa Reli ya Tazara inafika hadi Zambia ambapo Kuna urefu wa kilomita chache sana Kwenda Congo ambazo Pia zimeunganishwa na reli nyingine Kwenda Congo, Mji wa Lubumbashi ambao ni mji Mkuu wa kibiashara.

Kwa ninavyojua reli ya kati kwa Kiwango cha SGR mpaka mwanza na Kigoma itagharimu kiasi cha Trilioni si chini ya 25 kwa ujumla wa vipande vyote.

Jambo lililonishangaza ni kuwa tayari Reli ya Tazara inafika hadi Ndola Zambia na kuna Reli nyingine inafika hadi Lubumbashi , Congo kutoka Zambia.

Je haikuwa sahihi kwetu kuboresha Reli ya Tazara kwa Kiwango cha SGR na kuiwekea umeme na kuongea na Zambia kidiplomasia tukawakopesha hela za kuboresha reli kutoka Zambia hadi Lubumbashi Congo kwa Kiwango cha SGR?

Kwa mtazamo wangu naona gharama za kuboresha Reli ya Tazara kwenda Congo kwa Kiwango cha SGR ingekuwa ndogo sana kuliko kuijenga upya hadi Burundi na kuanza kuongea na Burundi ili waifikishe Congo jambo ambalo sidhani kama litakamilika hivi karibuni kutokana na hali ya kiuchumi ya Burundi! Na uhohehae wao kutokana na vita!

Nauliza swali hili kwenu wadau! Je kulikuwa na haja Kweli ya kujenga Reli ya SGR kwenda Kigoma na Mwanza? Au Tungeboresha tu TAZARA kuwa Kiwango cha SGR ambapo tungetumia gharama ndogo na kufika Congo kirahisi sana?



Hii ndo ramani ya Zambia inavyoonesha ukaribu wa Zambia na Lubumbashi Congo na urahisi wa kufika Congo kupitia reli ya TAZARA



TAZARA ina siasa nyingi sana na haitakaa kuja kufanya biashara ya faida. Sababu kubwa ni kuwa na partnership ya nchi mbili na sidhani kama kwa leo hii interest zinawiana.
Wao wanaenda kule na sisi huku. Haitakaa kuja kukaa sawa unless mambo ya msingi kabosa yabadilishwe. Tazara inaweza kwenda mpaka Namibia na Angola. Sio DRC peke yake
 
aisee....ujenzi wa kwenda kigoma umeanza lini na umefika hatua gani
Tanzania, Burundi na DRC kujenga reli ya pamoja
Untitled-1.jpg

 
Kupeleka kigoma pia ni kuhudumia watz wengi wa magharibi mwa nchi.

Watu wa magharibi wanafurahia na wanapenda usafiri wa treni kuliko mabasi.

kwa sababu usafiri wa train salama zaidi kuliko mabasi

Tatizo la TAZARA ni ownership. hebu fikiria, zaidi ya 70% ya reli ya tazara iko tanzania lakini dg wa tazara kimkataba anatakiwa atoke zambia.

Hivyo tz inaona kama tazara ni kwa ajili na ni ya zambia.

Upande wa zambia, siasa za ccm hawazielewi na hivyo huona bora wasijikite sana katika kuwekeza tazara badala yake wanatumia hata reli za kushuka kwenda south maana tazara imeungana na reli inayoshuka kwenda south africa mpaka cape town
Mkuu afu ishu nyingine Zambia na wao WANAOGOPA nafikili kurekebisha coz still wanamadeni makubwa sana dhidi ya wachina , pia Tazara inachukua km zaidi ya 2000 ni pesa NDEFU sana tena defu
 
Hatuwezi kuboresha Taraza peke yetu bila kuihusisha Zambia ambayo ni mbia.

Isitoshe Zambia kwa sasa hawaitegemei sana Tazara kama miaka ya nyuma na reli ya SGR tumeijenga kwa manufaa yetu wenyewe kwa kuangalia vipaumbele vyetu kwa wananchi wa huko sio nchi jirani.
Wazambia walishaacha kutumia coz ya wizi ulikuwa mkubwa pamoja ba serikali yeti ilikuwa haina time nayo, watu wanamiliki maroli.
 
Mkuu afu ishu nyingine Zambia na wao WANAOGOPA nafikili kurekebisha coz still wanamadeni makubwa sana dhidi ya wachina , pia Tazara inachukua km zaidi ya 2000 ni pesa NDEFU sana tena defu
Tazara ni white elephant. It is not making any good business. Kuna wakati hata wagons na locomotive walikuwa kama hawana. Na kuna watu pale wanalipwa super salaries.
MD ilikuwa lazima atoke Zambia. Sijui kama utaratibu ulibadilika. Kiufupi ni shirika la umma kama mashirika mengine. Na kuna ugumu sababu ni mali ya nchi mbili tofauti. Unafikiri itakuwaje?
 
Reli ya Kati haifiki Kagera inaenda Mwanza ambapo kufika Uganda lazima upande tena meli na kusafiri si chini ya masaa 24!

Reli ya kati SGR imeenda Mwanza na Kigoma na hapo hakuna tena Reli kwenda Burundi!

Kulikuwa na haja gani kujenga Reli ya kati kwa Kiwango cha SGR?
Reli ya kati inahudumia nchi za Congo, Burundi na Zambia kupitia Bandari ya Kigoma, fatilia vzr utajua namna reli ya kati inavyoliingizia taifa mapato mengi kuliko reli ya Tazara. Kama tunajenga reli kibiashara basi reli ya kati ndiyo sehemu sahihi ya kuwekeza.
 
Back
Top Bottom