John Fedha
JF-Expert Member
- Jul 2, 2018
- 624
- 717
Napenda sana Chadema mnavyojipa moyo.
Kwa taarifa yako kampeni ya mkoa mmoja aliyofanya magufuri ni sawa na mikutano yenu yote Chadema iliyofanya katika kanda zote mpaka sasa. CCM ni chama kubwa nadhani leo umeiona vizuri mwanza. CCM KIRUMBA hakukuwa na sehemu ya kutema mate ndani na nje acha kule gola milimani.
Si nyie ndiyo mlisema Chadema imekufa sijui nini upuuzi puuzi mwingi tu humu ndani.
Kuna kitu lazima muelewe kuwa ,mawazo mbadala hamuwezi yazuia kwa kununua wabunge,
Upinzani upo tu na utaendelea kuwepo mioyoni mwa watu wengi tu ,ambao hawaridhishwi na hali ya mambo inavyokwenda ndani ya nchii hii.
Kuna makosa mengi tu ya kimkakati ambayo serikali ya ccm imefanya,
Kuzuia Bunge Live lilikuwa kosa kubwa sana,
Kupiga marufuku Siasa wakati wao miaka 5 wao walikuwa wanafanya,
Angalia sasa nguvu kubwa mnayotumia katika kampeni zenu ni kama hamkufanya chochote ndani ya miaka 5.
Hivi weww na ccm yako mlishawahi jiuliza Watanzania hawa wanataka nini.?
Mnaleta habari za ndege sijui madaraja kweli kwa Mtanzania huyu wa leo ambaye anaishi chini ya dola 1,kupata milo 2 ni shida unamletea habari za madaraja eti ndiyo sera.
Alafu bado kwenye kampeni unamtisha kwa maneno ya hovyo hovyo yasiyo na tafsida.