John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Sakata la Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda lililopo Mahakamani limekuwa likiwatatiza wengi hasa baada ya awali kuonekana kwa wengi ni kama anaipotezea Mahakama kabla ya kujitokeza hivi karibuni kupitia mwanasheria wake.
Kupitia Kolamu ya Yakub Na Sheria inayoandikwa na Bashir Yakub, leo Jumanne Machi 8, 2022 anafafanua uhalisia wa nini kinachoendelea katika sakata hilo lilipo fika hadi sasa:
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Hadi sasa Makonda hajashitakiwa popote
Kesi iliyo mahakamani dhidi ya Makonda si mashtaka ya jinai. Kilicho mahakamani mpaka sasa ni maombi tu ya Saed Ahmed Kubenea.
Wala Makonda hatafutwi kukamatwa na mahakama yoyote, wala taasisi nyingine ikiwamo Polisi. Nimeona hadi magazeti
yanayoheshimika yakisema Makonda ana jinai za kujibu mahakamani, mara anatafutwa kukamatwa, si kweli.
Ni hivi, Saed Ahmed Kubenea anaomba ridhaa ya kumshitaki Makonda. Kawaida ya sheria ni kuwa DPP (Mwendesha Mashtaka wa Serikali) ndiye mwenye mamlaka ya kushitaki na kuendesha kesi ya mtu yeyote aliyeonewa katika jinai
zote.
Anaendesha kesi za jinai kwa iaba ya raia au mtuu aliyeonewa ama aliyekosewa (aliyeibiwa, aliyeumizwa,
aliyebakwa nk).
Hata hivyo mtu binafsi anaweza pia kushitaki na kuendesha kesi yake ya Jinai mwenyewe bila kupitia kwa DPP.
Lakini ikiwa mtu binafsi atataka kuendesha kesi yake mwenyewe bila kupitia kwa DPP, basi anatakiwa
kuomba ridhaa ya Mahakama kwanza, kupitia maombi (application) maalumu, chini ya vifungu vya 99(13), 128(2), na
392A(1)2) vya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai.
Haya maombi ya ridhaa ndiyo yaliyo mahakamani mpaka sasa na si jinai dhidi ya Makonda. Maana yake Kubenea anaomba ridhaa yeye kama yeye ili aweze kumshitaki Makonda.
Hiki ndicho kilicho mahakamanı. Kwa hiyo Kubenea anaweza akakubaliwa kumshitaki Makonda yeye kama yeye bila DPP ama akakataliwa. Na hiyo ni mpaka hapo hiyo Mahakama ya Kinondoni yalipo hayo maombi 1takapotoa uamuzi kuhusu
hilo.
Katika maombi hayo utamualika DCI, utamualika DPP na utamualika yule unayetaka kumshitaki, ambao nao kila mmoja kwa nafasi yake anaweza kujibu maombi kwa kupinga ama kukubali.
Na kwa haya maombi ya Kubenea, DCI na DPP tayarı wamejitokeza na kupinga asishitaki yeye kama yeye. Makonda hajajitokeza kujibu lakini kwa kuwa haya ni maombi tu (application), basi halazimishwi. Wanaruhusiwa kuendelea tu bila yeye kujibu ama kuwapo (exparte).
Ikiwa Kubenea atakubaliwa kumshitaki Makonda yeye kama yeye bila kupitia kwa DPP, basi hapo ndipo kesi ya jinai dhidi ya Makonda itaanza, na hapo sasa ni lazima Makonda kufika mahakamani atake asitake, na akikosa.
Kwa hiyo tuelewane kuwa mpaka sasa Makonda hana kesi yoyote ya jinai katika mahakama yoyote, wala hatafutwi kukamatwa.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Source: Jamhuri