Hadi sasa Rais Samia ndiye bora zaidi, anafanya kila kitu kwa ustadi mkubwa

Umelogwa kijinga sana !
 
Umesema kweli tupu.Wengi wanaolalamika,walikuwa hawalipi kodi ,ndio hao wanaolalamika.Wapo watu,wanaojifanya hawana kipato,kumbe biashara zao ndogo ndogo,zinaingiza kuliko mwenye biashara kubwa,ambaye ana madeni ,na mikopo mingi ya Benki.
Upo sahihi kabisa.
 
Siku 100. Zilimtosha sana huyu bibi. Huku anakotupeleka sasa si salama. Yani hata miezi6 hana ashapoteza mvuto
 
Kwa hiyo lile agizo la mawaziri wanaohusika na tozo ya Miamala kukaa na kuliangalia suala hilo na kuliangalia utaratibu ilikuwa geresha tuu? By the way, ni lini wananchi walikubaliana na tozo hizo? Sisi Wana CCM tunaumia kwa yanayoendelea, ninyi mnaofaidika na mfumo mnafanya Kampeni ya 2025 iwe ngumu kwa chama Cha Mapinduzi. Mshaurini vizur mama.
 
Uko sahihi tunakosa agenda ndio maana si rahisi kusimamia mtu alichosema jana.
Leo tupige nyungu kisa boss wako hataki chanjo akija boss mwingine unabadilika badal ya kujiuzulu.
Tunaongozwa na maslahi tu bila kuwa na nia ya dhati ya kupigania nchi.
 
Suala la kumsifia mtu linategemea.
" Aisifuye mvua imemnyea"
Kizuri kwako kibaya kwa mwenzako.
 
Wanaomshuku na kumponda Rais Samia ni jamaa zangu wale waumini kindakindaki wa mfumo dume.

Anafanya kazi kistaarabu bila ya kupaniki.
 
Sio tu dawa, wanalalamika ubovu wa miundombinu, ukosefu wa Zahanati na Hospitali alafu hawataki kulipa kodi. Wanataka kodi walipe wafanyakazi na wafanyabiashara wachache wenye biashara rasmi.
Tunapenda sana vitu vya dezo. Hao wafadhili wa uchumi inafika mahali wanatuchoka.
 
Nani amesema ilikuwa geresha?
Kampeni za 2025 zitakuwaje ngumu wakati wananchi watakuwa wanaona zahanati, shule bora, barabara Nzuri na miradi mikubwa ya kuwapelekea mahitaji ya msingi?
 
Kwa nini muda wote unawaza kuibiwa tu? Kwani wapi imeandikwa lazima hela ziibwe?
Bado hawajaweka wazi zilizopigwa na wajanja kama kawaida. Watuambie pia wajanja wamepiga ngapi so far kutoka kwenye makato ya wanyonge?
 
Wewe kama humpendi na kumkubali Samia basi Kama mtu anampenda na kumkubali kwako unamuita nyumbu???

Hilo ni Tatizo lako binafsi! Kwani Hospitali , barabara na miradi mingine inayofanywa kwa hela za tozo sio kwa maslahi mapana ya umma???

Kwako maslahi ya umma ni nini?? Ni kina mdude kutukana wazi au kuwa na maandamo kila siku???

Una shida sana! Kumchukia kwako Samia kutakupa msongo wa mawazo
 
Wewe kama humpendi na kumkubali Samia basi Kama mtu anampenda na kumkubali kwako unamuita nyumbu???

Hilo ni Tatizo lako binafsi! Kwani Hospitali , barabara na miradi mingine inayofanywa kwa hela za tozo sio kwa maslahi mapana ya umma???

Kwako maslahi ya umma ni nini?? Ni kina mdude kutukana wazi au kuwa na maandamo kila siku???

Una shida sana! Kumchukia kwako Samia kutakupa msongo wa mawazo
 
Nani amesema ilikuwa geresha?
Kampeni za 2025 zitakuwaje ngumu wakati wananchi watakuwa wanaona zahanati, shule bora, barabara Nzuri na miradi mikubwa ya kuwapelekea mahitaji ya msingi?
Kuna somo la nidhamu ya matumizi tunapewa kupitia hizi kodi tunazotozwa. Somo hili wazungu wanalijua miaka mingi iliyopita, linawafanya waishi kwa ratiba ndefu.
 
Kuna somo la nidhamu ya matumizi tunapewa kupitia hizi kodi tunazotozwa. Somo hili wazungu wanalijua miaka mingi iliyopita, linawafanya waishi kwa ratiba ndefu.
Watu wanajitoa ufahamu Au hawajui tu! Hakuna nchi zenye kodi kama nchi za Ulaya na Marekani. Na wako very serious kwenye matumizi ya kodi husika na Ndo mana leo tunaziona zina maendeleo makubwa sana.

Huku kwetu kila siku wanabanwa wafanyakazi na wafanyabiashara wachache alafu watu wanataka maendeleo ya haraka.

Lazima tujifunze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…