donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,128
- 21,885
Salaam wakuu,
Leo nataka tutengeneze hadithi ambayo kila comment itakua ni mwendelezo wake lakini tutastick na mahadhi (genre) ya hadithi hii.
Naanza:
ilikua ni siku ya mvua isiyokatika na miungurumo ya radi katika jiji la dar es salaam. siku hii haikua njema sana kwangu kutokana na biashara yangu ya kahawa na kashata kutouzika kwa siku kama hizi. nikiwa katika chumba changu cha kupanga maeneo ya kwa mnyamani, nikiutafuta usingizi kwa mbali huku mawazo Mungu yakiitawala nafsi yangu hususani kero ya mama mwenye nyumba kuhusu kodi yake ghafla nikastushwa na hodi iliyokua ikigongwa mlangoni mwangu. sikutarajia ugeni wa aina yeyote na wala sikua na ndugu wala rafiki ambaye angekuja kunitembelea. wakati bado naendelea kujiuliza, hodi iliendelea kupigwa na safari hii nikasikia sauti ya kike ikiomba nifungue mlango....