KESI YA MZEE MNYOKA 06
kutoka kwa Mzee Mnyoka kwenda kanisani ilikua Ni dakika tano tu lakini Mzee Mnyoka hakupenda kuonekana akienda kwa Padri asubuh Ile, zaidi Sana hakupenda mke wake ajue kwanza hizi harakati zake,
Hivyo alivaa mabuti yake ya shambani na kuchukua panga lake akidai anaenda kupunguza Miche yake ya kahawa ,
Mzee Mnyoka alinyoosha njia ya shambani baadae akavuka mto na kurudi kando kando kuelekea kanisani,
Ni wakati anatokea ndipo Padri John alikua anawasha piki piki yake ili atoke,
Kwa bahati alimuona Mzee Mnyoka na akasimamisha safari yake Sasa
"Nzee Nyoka,. Pole kwa Mikasa ya junia , junia imejaa Dhambi na uonevu uko mwingi"!
Padri John aliongea kwa lafudhi yake ya kizungu....
Alishakaa Sana pale kijijini na ndio hata kwa msaada wake baadhi ya huduma pale kijijini Kama umeme na zahanati zilikuwepo,
Zamani Mzee Mnyoka alikuwa muumini mzuri lakini bila sababu za msingi alijikuta anakuwa mvivu wa kanisa na mwishowe akajiwekea ratiba yake "ya kipuuzi" ya kwenda kanisani Mara moja kwa mwezi!
Na pengine hiki ndicho kilimsababisha Padri John kusitisha safari yake hii akidhani labda mwanakondoo wake anarudi...
"Ooh Padri Tumsifu Yesu Kristo!"
Mzee Mnyoka alisalimia
"Milele Amina"
Nzee Nyoka!
Padri alijibu
"Padri Ni Mzee Mnyoka sio Nzee Nyoka! Kumbe hujaweza tu bado!"
Mzee Mnyoka alisema Sasa wakiingia ndani,
"Nyoka Ni Nyoka tu nzee"
Hahahaha
Walicheka wote ..
"Imefurahi kukuona, kila siku naambia mama nzee iko wapi, kwanini inakuja kila mwezi na hapa Hakuna nshahara nzee Nyoka"
Padri alisema Tena kwa utani!
Baada ya maelezo mafupi Sasa Mzee Mnyoka alimuambia Padri kuwa ana Jambo la msingi Sana,
"Nadhani unakumbuka Ile kesi yangu ....Basi Sasa Kuna watu walinifuata......"
Mzee Mnyoka alieleza kila kitu mpaka Ile Jana alipoenda kwa Mzee Pembe
"Sasa nafikiri Mambo mawili kwanza nahisi kwenye vile vitalu hayo madini kweli yapo, na wanaficha ili serikali isijue ili waweze kuvuna taratibu na baadae waseme kuwa hawajagundua kitu,
Ama, waseme wamepata kidogo,..
Sasa itakuwa ng'ombe wa Mzee Pembe kwa bahati mbaya alikunywa maji yenye baadhi ya izo kemikali, Sasa Ni wazi kuwa huyo ng'ombe angekufa muda mfupi, na lazima uchunguzi ungefanyika maana Bwana mifugo Yuko karibu tu,
Hivyo Siri ingegundulika, ndio hapo Sasa wakaona lazima ng'ombe huyo apotee,
Tatizo lilikuja Sasa namna ya kumpata ikabidi ashawishiwe mwenyekiti "
Mzee Mnyoka sasa aliongea huku akimtazama Padri ambaye alikua ametulia tu akimsikiliza kwa Makini,
"Nzee Nyoka hili Jambo kubwa na hatari sana, kuliko vile unadhani" alisema Padri John
"Ni kweli Padri"
Mzee Mnyoka alisema,
"Sikiliza kesho kutwa njoo , usiku saa mbili kuna rafiki yangu atakuja hapa Ni mtu ya serikali lakini iko mwaminifu Sana"
Itaweza kukusaidia Ila Sasa Ni hatari sana nzee Nyoka...
Alisema Padri na Mzee Mnyoka akaondoka zake na kurudi nyumbani,
Ni wakati anavuka barabara ndipo aliona kundi la watu wakikimbia kuelekea mtaa wa kule kwenye vitalu,
Mzee Mnyoka alihisi labda Kuna wageni, lakini umati ule umlimtisha Sana nae akamuua kuunga,...
"Ajali! Ajali! Ooh oooh ,jamani ! Jamani!"
Zilikua Ni kelele za watu wakikimbia kuelekea upande wa msitu kwenye mradi,
Kwa mbele kundi kubwa la watu lilikua barabarani limezunguuka,.
Bila shaka ilikua Ni Ajali,..
Mzee Mnyoka alifika na kuuliza kulikoni,..
"Mzee Pembe kagongwa na Gari!"
"Nini weweeee?"
Mzee Mnyoka alihamaki
"Yaani hiyo Gari ilikua paleee, wakati Mzee Pembe anakatisha ndio ikatoka kwa spidi Kali na kumgonga,"
Kijana mmoja aliongea,...
Jitihada za kumpeleka zahanati hazikufaa kwani Mzee Pembe alifariki pale pale,
Hakika Sasa ilikua simanzi kila Kona,
Mwili wa Mzee Pembe ulifunikwa pale pale chini huku polisi wakisubiriwa wafike,
Ndio hapo Sasa Mzee Mnyoka akamvuta yule kijana pembeni,
"Wewe ulikua wapi wakati ulipoona iyo Gari" Mzee Mnyoka alianza,
"Kiukweli Ile Gari ilinipita pale, wakati Mimi namalizia kuchimba mfereji kwa ajili ya kuweka Bomba, Mara chache Sana magari yanafika hapa nyakati za mchana kwani Mara nyingi Ni asubuh na jioni, na Mara chache labda wakija mabosi kukagua, au viongozi wakija kutembelea,
Sasa nilivyoona Gari imepaki Mimi nikaendelea na shughuli zangu,
Lakini Mzee nahisi wale jamaa walidhamiria kumgonga Mzee Pembe, maana Ile anatokea tu nao wakawasha Gari"
"Sikiliza kijana, usije kumueleza mtu Hili Jambo hata polisi usiwaambie"
Mzee Mnyoka aliongea Kisha akaondoka zake,
Itakuwa wameamua kumuua Mzee Pembe ili kuficha Siri zao zaidi,
Mzee Mnyoka aliwaza,
Kwasasa Mzee Mnyoka alikua na hofu ya wazi wazi,
Alishaanza kuhisi dalili mbaya,
Hawa watu wapo tayari kutoa uhai wa wengine kwa ajili ya kulinda maslahi yao,
Ni kweli endapo majibu ya utafiti yangetoka mapema, na kubainisha kuwa eneo Hilo Lina urenium Basi Ni wazi kuwa serikali ingeingilia Kati, na pengine Sasa eneo lingetaifishwa rasmi, lakini huwezi kujua labda kampuni hii inashirikiana na nchi za mbali huko kuhujumu Mali asili za nchi yetu,
Mzee Mnyoka Sasa alishindwa pa kuanzia
"Kwanini Mimi wameniacha hai?"
Mzee Mnyoka aliwaza,
Mzee Mnyoka Sasa aliulaumu ule usiku wa alhamis aliposhuhudia wizi wa Ng'ombe,
Ni wazi kuwa mlolongo wa Mambo yote haya Ni yeye!
Na Sasa mpaka uhai wa Mzee Pembe , umechukuliwa, Tena bila kosa lolote,
Sasa bila shaka anayefuatia Ni yeye!
Ni katikati ya mawazo hayo Sasa akakumbuka kuwa amepewa wiki moja tu ya "kufanya maamuzi ya kuamua kubaki au kuondoka"
Pale kijijini,
Lakini pamoja na hayo ,
Tayari ameshagundua Siri nzito, ambayo pengine kuzidi kimo chake!
Ni ukweli usiopingika kuwa Sasa Mzee Mnyoka alihitaji kulifikisha Jambo Hili sehemu "husika" Tena kwa muda muafaka,
"Padri ataweza?"
Mzee Mnyoka Sasa aliona Padri John anaweza kuchelewa kumpatia msaada,
Alikua na siku 4 mbele tu kabla wiki haijaisha,
Zaidi ya yote ,
Usalama wake yeye na familia yake aliuzingatia Sana,
"Lazima nifanye Jambo"
Mzee Mnyoka Sasa aliwaza