Hadithi: Kesi ya Mzee Mnyoka

Hadithi: Kesi ya Mzee Mnyoka

KESI YA MZEE MNYOKA 07

Aliwaza na kuwazua Kisha akapiga moyo konde,

"Liwalo na liwe Kama mbwai na iwe mbwai"
Alijisemea akielekea Nyumbani kwake,

Alifika na kujituliza Kwenye Kochi lake lililochakaa kidogo hivi, macho yake Sasa yalitazama juu ya dari ya nyumba yake , kulikua na michirizi yenye rangi Nyeusi iliyotokana na matone ya maji kulikua na tobo Kwenye bati ambalo lilisababisha kuvuja Mara kwa Mara mvua inaponyesha,

Mzee Mnyoka Sasa alijaribu kufumba macho,

Na kuvuta hisia kuhusu mpango wake huo ,

Alimfikiria Mzee Pembe ambaye Jana tu walikua wote,
Ni wazi kuwa usipotetea maisha yako Basi unanenepesha kifo chako,..
Mzee Mnyoka Sasa alihitimisha mpango wake kichwani na wakati wa kutekeleza Sasa umefika,


***********

Mama Monica nae Kama wanakijiji wengine alikua ameenda msibani,

Baada ya kurejea aliamua kupitiliza jikoni moja kwa moja na kuandaa chakula Cha jioni,

Ni wakati anaingia sebuleni ndipo akamuona Mzee Mnyoka akiwa ameanguka chini!
Huku akipumua kwa shida!
Mzee Mnyoka alikua alisumbuliwa na presha na muda mrefu ,
Lakini Ni mwaka mmoja na miezi mitatu Sasa Mzee Mnyoka hakuwahi kuanguka presha,.

Alijitahidi kufuata ushauri wa daktari ikiwemo kula chakula kisichokua na mafuta Sana,
Na kuhusu mazoezi Mzee Mnyoka aliamua kuwa "mzururaji" mzuri tu! Na ndio maana alipenda Sana kutembea tembea!

Kuna wakati Mzee Mnyoka alikua anawatania marafiki zake kuwa
Anaogopa kulala!

Ndio maana anarudi Nyumbani kwa kuchelewa ili "alale kidogo"

Kwa ufupi Mzee Mnyoka alijali Hali yake Sana na hata Mara ya mwisho aliporudi hospital kucheki afya yake daktari alimpongeza Sana,...

Mama Monica hakusubiri,

Alitoka nje haraka na kupiga kelele kuita majirani,
Ni nusu saa baadae Mzee Mnyoka alishafikishwa zahanati ya Kijiji na kuwekewa madripu ya maji,

Baadae Mganga wa Ile Zahanati alishauri Mzee Mnyoka apelekwe hospital kuu ya wilaya Kama mgonjwa wa rufaa na hivyo walipiga simu kwa ajili ya kuletewa ambulance,
Mzee Mnyoka alikua kitandani kimya tu hakujitingisha Wala kufumbua macho,
Mke wake Sasa alikua akilia tu,
Masaa matatu baadae Mzee Mnyoka , mkewe na Mzee Omari pamoja na manesi wawili walikuwa Kwenye ambulance wakikatisha mitaa kuelekea hospital ya wilaya,

"Atapona tu mumeo mama usilie"
Manesi walijaribu kumbembeleza mama Monica,

*****

SAA 5:50 usiku ,
Hospital ya wilaya Kiomboi

Mzee Mnyoka alipelekwa haraka Kwenye wodi ya wagonjwa mahututi, na kilichowangaza madaktari vipimo vyote vilionyesha Mzee Mnyoka hakuwa na tatizo lolote!

Hata hivyo mzee Mnyoka hakufumbua macho kabisa,

Ni wakati Sasa madaktari wakiwa wanashauriana
"Aitwe dokta Kimei"...

"Yeah, Mpigie"
"Ngoja nimfuate , hajafika mbali"

Madaktari Sasa walikua wanazungumza, na mwishowe walimpigia simu dk Kimei,..
Hayo yote Mzee Mnyoka aliyasikia,.
Na hicho ndicho alichokusudia,.

"Dokta Kimei"

Ndio,

Huyu alikua daktari wake Mzee Mnyoka, wakati wote aliokua anaumwa presha alikua Ni yeye alikua akimtibia,

Ilipelekea Sasa Mzee Mnyoka hata alipokua anakuja wilayani Kwenye vikao vya ushirika,

Hakuishia huko tu Bali alifika hospital kumtembelea dokta Kimei,

Na hivyo ilikua rahisi tu dokta Kimei kuweza kuja haraka kumuangalia Mgonjwa "wake"


"Ooh Mzee Mnyoka!
Vipi mama Mzee amekuwaje Tena"
Dokta Kimei aliongea baada ya Kumuona mama Monica
"Baba nilitoka msibani ndio nikamkuta katika Hali hiyo , mpaka Sasa alikua ameanguka sakafuni dokta msaidie"
Mama Monica alianza kusema huku machozi yakimlenga lenga

Dokta Kimei alisogea alipokua mgonjwa wake na kuanza kumkagua , alianza na mapigo ya moyo ,na kuangalia Mambo mengine ya kidaktari,

"Hebu nione faili lake"

Dokta Kimei alisema,
Alikagua faili la Mzee Mnyoka Kisha akaendelea na vipimo Ni wakati anaendelea na "kumkagua"

Mzee Mnyoka Sasa Dokta Kimei alijiridhisha kuwa Mzee Mnyoka hakuwa na ugonjwa wowote!

Sasa aliamua kufanya Jambo la kubahatisha!

"Hebu naomba mnipishe na huyu mgonjwa!"

Madaktari wenzake sasa walipigwa na butwaa!

Kisha Kama waliambizana wakatoka nje kwa pamoja!

Baada ya kutoka nje dokta Kimei Sasa aliamua kufunga mlango kabisa!

******
Miaka minne iliyopita

Dokta Kimei akiwa pale pale hospital aliletewa mgonjwa mmoja siku hiyo kwa dharula,

Tofauti na Mzee Mnyoka, mgonjwa wa siku hiyo alikua Ni mwanamke,
Walidai amezimia kwa ghafla,
Walifanya vipimo vyote na hakukua na ugonjwa wowote,
Ni wakati dokta Kimei amewatoa nje wauguzi ili amfanyie vipimo vya ziada ndipo yule mama akafumbua macho!
Dokta Kimei hakustuka Sana lakini baadae yule mgonjwa alimuita na kumueleza kila kitu,
Alisema wazi hakua akiumwa popote lakini alichoka maisha yake ya ndoa na mumewe , na ndugu zake hawakumuelewa na ameona Kama atajiua atakua hajawatendea haki watoto wake,

Na hivyo njia pekee aliona Ni kujifanya anaumwa ili apumzikie hospital!

Dokta Kimei Sasa alikumbuka kesi hiyo huku akirudi kitandani alipo Mzee Mnyoka..
"Haya Mzee Mnyoka niambie Sasa kuna inshu gani?"
Dokta Kimei aliongea akitabasamu na kukaa kitandani!
Itaendelea
 
KESI YA MZEE MNYOKA 08

Kama utani vile...

Mzee Mnyoka akakaa kitandani ...

"We Mzee kiboko, walah utasababisha nicheke Hadi nife"
Dokta Kimei alisema Sasa kwa sauti ya chini,
"Usiniambie vioja vyote hivi mzee Mnyoka Ni mbwembwe tu"
Dokta aliongea Sasa Mara hii Mzee Mnyoka akijiweka sawa,

"Dokta Kuna Jambo kubwa linatokea huko kijijini, naomba fanya ufanyavyo uniletee mtu wa usalama wa Taifa hapa,

Kuna Mambo mazito nimuambie"
Mzee Mnyoka alisema kwa sauti ya chini,

"Mzee Mnyoka unajua hao jamaa sio rahisi kupatikana kwa haraka hivyo"
Dokta Kimei aliongea kwa upole,..


"Dokta fanya Jambo, kesho niletee huyo mtu hapa"

Na ili kuonyesha Mzee Mnyoka alikua hatanii alirudi kulala Kama mwanzo Kisha akafumba macho!

Sasa Dokta Kimei alichoka kabisa ..

********

Dokta Kimei alitoka nje,

Kisha akamnong'oneza kitu daktari mwenzake ambaye baadae alimpatia ufunguo wa Gari,

"Mama usijali kuhusu mgonjwa atapata nafuu ngoja kuna dawa Fulani nikazichukue mjini hapo Mara moja"
Dokta Kimei alimwambia mke wa Mzee Mnyoka Kisha akatoka nje ya hospital na kuingia kwenye Gari..


Hakujua aende wapi,

Ofisi za usalama wa Taifa alizifahamu zilikua jirani tu na hospitali yao,
Lakini kutokana na Jambo lenyewe hakuona Kama Ni busara kwenda ofisini kwao moja kwa moja, alihitaji kupata mtu moja kwa moja ikibidi usiku ule, ampeleke kwa Mzee Mnyoka,

Ghafla alipata wazo,
Alikua na rafiki yake ambaye ni polisi, na huyu hakuwa rafiki tu Bali alikua katika mahusiano ya kimapenzi ya Siri,
Hivyo akaamua kupaki Gari pembeni na kuwasha taa za tahadhari tu,

Kazi yake dokta Kimei na Polisi ilikua sawa tu,

Hivyo hakutegemea usiku huo Kama Josephine atakua amelala,

Alitoa simu yake,
Samsung Galaxy nakutafuta namba ya Josephine,

Iliita kwa sekunde kadhaa Kisha ikapokelewa,

"We mwanaume usiniambie usiku huu umenimisi tu, au mmevamiwa na majambazi usiku huu?

Alisema Josephine,..

Kwa namna ya pekee Hakuna siku hawa watu wamepeana salamu,

Kila anayepiga simu anaeleza shida zake tu,

"Sikiliza Jose, uko job ama?"

"No nimetoka saa 5 hivi nilikua najiandaa kulala kesho tunamsindikiza mheshimiwa mkuu wa mkoa, " alisema Afande Josephine..

'okay naomba njoo mpaka hapo kwenye mti mkubwa mi Niko jirani na kwako hapa,"

Kimei aliongea huku akiwasha Gari kusogea pole pole,

"Okay dakika mbili"
Josephine aliongea,..

Haikua Mara moja wanakutana hapo kwenye mti mkubwa, nyakati Kama hizi,

Hivyo Josephine alitoka tu akiwa na track yake ya kulalia na Sweta akatoka nje na kusogea nje kwenye mti mkubwa na kuona Gari la akafungua mlango na kuingia ndani,

"Hi"
"Hi d"
"Naona Gari jipya leo"
"Hapana ni la James"
Kimei alijibu,

"Niambie nimekumisije we mwanaume!"
Alisema Josephine,

" Josephine naisikilize kidogo"

Alisema dokta Kimei Kisha akamsimulia habari zote za Mzee Mnyoka..

"Kwahiyo Nisaidie mama, yule Mzee nahisi ana Jambo serious,

"Sikiliza, ngoja kuna rafiki yangu tulisoma wote ,yeye akaenda huko , na amekuja na msafara wa mkuu wa mkoa, Ila Sasa ukimuona usije ukacheka"

Alisema Josephine huku akitabasamu,..
"Hahaha kwanini"
Kimei aliuliza..
"Yaani kwanza hiyo kazi yake anayofanya kwa sasa huwez kumdhania Ila anapenda Sana hayo Mambo ya kesi kesi Kama hizo subiri "
Nakutumia namba yake ,Ila tafadhali Sana iwe inshu serious, please nakuomba"
Alisema Josephine,
"Utamtumia sms hivi,
Hello, tembo mmoja amepotea njia"
Ukiona imepokelewa kimbia sehemu ambayo kabisa Hakuna watu maana atakupigia .
Josephine aliongea huku akishuka kwenye Gari,

"Mh Josephine kwani siwez kumpigia moja kwa moja"
Dokta Kimei aliongea Sasa akiwa ameshangaa

"Hello tembo mmoja amepotea njia"

Fanya hivyo bhana, kila sehemu na utaratibu wake,
Hata wewe pale huwezi kuletewa mgonjwa halafu ukampasua tu tumbo,..
"Okay Mama umeshinda"
Alisema dokta Kimei huku akigeuza Gari na kuondoka.

" Dunia hii, Basi tu, Sasa tembo Tena, anyway"
Dokta Kimei alijisemea kimoyo moyo,

Alisimamisha Gari mita Kama Mia tatu hivi karibu na hospital Kisha akatoa simu yake,

Alifungua sehemu ya kutuma ujumbe mfupi,

"HELLO, TEMBO MMOJA AMEPOTEA NJIA"

Kisha akatafuta Kwenye Kitabu Cha majina "tembo"

Kisha akatuma sms,

Na Sasa akapandisha vioo kusubiria....

******


Mama Monica Sasa alishalia mpaka amechoka alibaki pale nje mapokezi pamoja na Mzee Omari,

Huku Sasa madaktari wakiwa huko ndani na Mzee Mnyoka,

"Kwakweli Kijiji Chetu Sasa kinapatwa na mikosi gani, Jana tulimzika Pembe, Leo Tena Mzee Mnyoka jamani yupo mahututi"

Alisema Mzee Omari kwa uchungu,

"Mama wewe unaweza kutafuta pa kulala, mgonjwa anaendelea vizuri wewe Mzee Omari Sasa unaweza kwenda kulala na mgonjwa"

Ilikua Ni sauti ya Nurse aliyekuja kuwapa taarifa,.

Mzee Omari alienda chumbani kwa Mzee Mnyoka na kulala kitanda Cha pembeni yake,

Huku mama Monica akimfuata yule Nurse ili kupatiwa pa kulala apitishe huo usiku..

********

Dokta Kimei aliitazama simu yake kwa hamu kubwa ,

"God will make a way, where it seems to be no way, he works in ways , we can not see....."

Ilikua Ni sauti ya wimbo kutoka kwenye simu ya dokta Kimei,

Haraka Sana alipokea na kuweka sikioni,

sauti ya kiume upande wa pili ikasikika,

"Niambie,"
"Tunaweza kuonana hapa Hospital ya wilaya Kiomboi? Just right now?"

"Poa, "

Baada ya dakika 10 hivi Dokta Kimei alisogeza Gari karibu na lango kuu la hospital ili amuone "mgeni wake"

Aliangalia huko na huko lakini hakuona mwanga wa Gari au piki piki au pengine hata mtu aliyekuwa anakaribia lango la hospital,

Hivyo akaamua kushuka kwenye Gari ili kwenda mapokezi,

Ni wakati anakatisha ndipo akamuona mgeni wake, akiwa amesimama karibu na dirisha la kutolea dawa,

Dokta Kimei alipigwa na mshangao,

Alifanya kazi pale Kama miaka 11 hivi,

Hivyo manesi wote na madaktari aliwafahamu vizuri, kuanzia wale wa kudumu Hadi wale wa kujitolea,

Hivyo "daktari" huyu hapa mbele yake alijua fika ndie mgeni wake,


Alipigilia koti lake jeupe vizuri kabisa,

"Tembo!"

Dokta Kimei alimpa mkono huku akitangulia ndani,

Walipita kwenye korido "madaktari" hawa wawili mpaka ofisini kwa dokta Kimei,

Na kwa sauti ya chini dokta Kimei alimsimulia kila kitu kuhusu Mzee Mnyoka

"Okay andaa mazingira tukamsikilize"

Alisema na Dokta Kimei alienda kwa Mzee Mnyoka na kukuta Mzee Omari alishalala, kwa tahadhari kabisa Dokta Kimei aliamua kumpeleka Mzee Mnyoka ofisini kwake,

"Ingia hapo Kwanza tumlete Mzee"

Dokta Kimei aliongea akimuonyeshea yule jamaa sehemu ya kujificha kwanza,

Baada ya dakika kadhaa Mzee Mnyoka aliletwa Sasa,

Baada ya Nurse kuondoka

Dokta Kimei Sasa alimwambia Mzee Mnyoka kuwa mtu wake amepatikana,

Mzee Mnyoka akakaa kitandani
"Ndio Mzee Mimi naitwa Oscar,
Naamini naweza kukusaidia"
Alisema Sasa yule mtu kwa upole,

Mzee Mnyoka alisimulia matukio yote kuanzia siku alipoona yule ng'ombe akiburutwa na mzee Mkude,

Alieleza kila kitu mpaka jinsi Mzee Pembe alivyouwawa na mashaka yake kuhusu uwepo wa madini na mengine mengi aliyohisi yanaweza kuwa msaada,
Dokta Kimei alishangaa Sana uzito wa Jambo lenyewe, wakati yule jamaa yeye sura yake ilikua vile vile tu Kama mwanzo,
Baada ya maelezo Sasa Oscar akatoa muelekeo..
"Mzee pole Sana, na hongera kwa mbinu hii, maana hao jamaa watajua unaumwa kiukweli kweli,
"Wamejenga ofisi hapo kwenye huo mradi?"
Oscar aliuliza
"Ndio kuja jengo wanatumia kama ofisi hivi na hata mafundi na vibarua ndio wanalipwa humo," Mzee Mnyoka alijibu,

" Kuna ulinzi?"
Aliuliza Tena Oscar
"Kwakweli sijawahi kuona askari pale, labda Mara moja moja wakija viongozi" Mzee Mnyoka alisema
"Mmh hapana, hii sehemu itakuwa inalindwa Sana Mzee Mnyoka, sema kilichotokea Ni kuwa hawajeweka ulinzi wa kuonekana maana wangestukiwa kuwa ipo Mali hapo, Sasa sikia huyo kijana ambaye alikuletea flash nadhani ukimuona utamkumbuka?
 
KESI YA MZEE MNYOKA 09

"Ndio yule kijana alipoleta flash, sura yake haikua ngeni kabisa, Ila Sasa nilisahau wapi nilipomuona Mara ya kwanza, Ila hata akija hapa namkumbuka kabisa"


"Okay Sasa Mzee Mnyoka , kazi hii inaweza kuchukua muda wa wiki moja au mbili hivi mpaka kumalizika, kwasasa sikushauri urudi kule kwanza, hivyo unaweza kuendelea "kuumwa" hapa kwa siku kadhaa na nikihitaji chochote nitawasiliana na Dokta Kimei lakini pia ukiwa na taarifa nyingine ambazo unahisi zitasaidia Basi tutawasiliana, vinginevyo usimuambie mtu yoyote , na vile vile Mimi na wewe hatujawahi kuonana na hatujuani kabisa, Sasa kila la kheri"

Oscar alitoka na kuaga, dokta Kimei alimtoa mgeni wake Hadi nje ya hospital ,

"Kesho saa sita na nusu pitia kwenye dustbin lililo nje ya ofisi yako, utakuta chupa ya kibox kidogo kutakua na maelezo yako kuhusu hatua inayofuata, vinginevyo kila la kheri na mgonjwa wako, "

Alisema Oscar Kisha akapotelea zake gizani...

**********


Kesho yake asubuh dokta Kimei alifika kwa Mzee Mnyoka na kuweka mipango yao sawa,

Habari za Mzee Mnyoka kuumwa Sasa zilienea Kijiji kizima na watu Sasa walimiminika hospital kumjulia Hali Mzee Mnyoka,
Ni watu wawili pale hospital ndio walijua undani wa ugonjwa wa Mzee Mnyoka,
Dokta Kimei aliendelea na kazi zake Kama kawaida ambapo ilipofika saa sita na nusu alitoka nje kwenda Kwenye ndoo ya kutupia taka taka ambazo si hatarishi Sana,
Alivaa baada ya kutupa jicho huko na huko, ndipo akavaa gloves zake na kuingiza Mikono kwenye ndoo,
Alitabasamu baada ya kuona kibox kidogo hivi , akakitoa na kuweka kwenye mfuko wa koti lake Kisha akavua gloves na kuzitupia humo...


Alirudi ofisini kwake Kisha akakifungua

Ndani yake kulikua na kikaratasi kidogo tu
"Zoezi litaisha baada ya wiki moja,

Usiamini mtu , kwenye chumba Cha Mzee mnyoka ,
Na jiangalie wewe mwenyewe,.

Kwa chochote piga hii namba, "0002004006"
Unaitwa TEMBO
Dokta Kimei Sasa alikua ameingia kwenye majukumu mazito ambayo binafsi hakutarajia,
Aliamua kuweka utaratibu wake mzuri wa kumuhudumia Mzee Mnyoka,
Ambapo alimuandalia chakula kule ofisini kwake, na Kisha Mzee Mnyoka alikua analetwa anakula halafu anarudishwa Tena Kama mgonjwa mahututi!

*******

Siku mbili baadae

Kijijini Kinjeki... 8:34 asubuhi

Vijana wengi walikua kwenye foleni kwa ajili ya kupata vibarua kwenye mradi uliokua unaendelea pale kijijini,
Zipo kazi ambazo zilihitaji watu wanne, zingine watatu, na zingine mmoja,
Mnyapara Sasa alikua akitangaza kila kazi na idadi ya watu,
"Mtaro deep, wanne!"
Square round kuchimba wanne!"

"Kusogeza mabomba kumi na mbili!"

"Free role mmoja"
"Niko hapa boss" Kijana mmoja aliruka mbele kwa Kasi ya ajabu, Ni wazi kuwa alikua anasubiri hiyo nafasi ....

"Wa ndani sita"
Mnyapara aliendelea na mwishowe geti likafungwa,

Vijana hawa waliobahatika kupata kazi siku hiyo waliingia ndani kabisa ya uzio kwa ajili ya kuanza kazi...
Kila mmoja alikua na hamasa kwani malipo si haba, Kibarua alilipwa 18,000 ama 15,000 Kama atakula chakula Cha mchana pale pale,

Oscar alikua miongoni mwa vijana hao ambaye kwa makusudi kabisa alichagua kuwa free role siku hiyo,


Oscar alifika Jana usiku akiwa full na ndipo alimtafuta Kijana mmoja na ndie aliyempa utaratibu mzima wa kupata kazi na Aina ya kazi pale "mgodini"
Oscar alipewa muongozo wa kazi yake ambaye kwa uzoefu wake aliokuwa nao ilikua Ni kazi simple sana kwake,
Kwanza ilikua Ni kupata sample, kwenye maji ya visima vimojawapo, na , na pia kujua mhusika au wahusika wanaongoza hiyo oparesheni ya kuibia nchi,
Hivyo asubuhi hii alivaa Kama vijana wengine , kaptura ya jeans, na raba, pamoja na shati lililokatwa Mikono,

Alichagua kitengo Cha kutokuwa na kazi maalumu kwanza,

Kutokana na maelezo ya yule Kijana kitengo kile kilikua na kazi nyingi na malipo yalikua Ni elf 10 kwa siku,..

"Siku nyingine unaweza kutumwa na mabosi uwapelekee sigara au maji"

Ndio maana Oscar alivyorukia iyo nafasi asubuhi Ile vijana wenzake walimshangaa!


Kazi iliendelea Kama kawaida, vijana waliendelea kufanya kazi Kama mchwa, kutokana na section zao,

Ni Oscar pekee yake ambaye alikua yupo "kazini" kivyake vyake, hata hivyo usingeweza kumdhania kwa namna alivyokuwa akipiga kazi Kama mzoefu, aliweza kufanya kazi zote alizotumwa kwa haraka na weledi mkubwa ,

Mpaka muda wa mchana Sasa, alianza kutabasamu baada ya kuona kazi yake inakwenda vizuri,


Mosi, aligundua kuwa sehemu Ile inalindwa Sana,

Kwa haraka alishapishana na walinzi zaidi ya ishirini, kwa namna wanavyotembea na kuongea na miili yao, Oscar Kama mpelelezi mzoefu alishaona, zaidi ya yote pia aliona CCTV camera zaidi ya nane, kwa maana hivyo kila tukio lilikua linaonekana mahali Fulani, na hivyo asingeweza kutoka na "sample" kirahisi kwa mchana ule,

Kitu pekee ambacho aliamini Ni kuwa kuna Ofisi mahali kubwa kuliko hii ambayo inaonekana hapa, kwa uzoefu wake alihisi lazima jengo Hili liwe Ni kiini macho tu,

"Oya baharia hatujaja kukaa kizembe hapa, nenda Pembe Ile ukamshikie mjomba pale ngazi"

Oscar alistuliwa na nyapara wakati akiwa katika fikra nzito,

"Poa poa bosi" Oscar alisema akinyanyuka haraka, na kuelekea kule...

***********
SAA 12 jioni ilikua Ni mwisho wa kazi ambapo vibarua walisogea kwa Nyapara wao na kupewa malipo yao,
Oscar alichukua elfu kumi yake nae na kutoka nje ya mgodi, ....

"Baadae kidogo tutaonana"

Alijisemea kisha akaingia zake mtaani kwenda mahali alipokua amejihifadhi,


*********

Hospital Kiomboi saa 1 usiku,

Dokta Kimei na Mzee Mnyoka Sasa walishaanza kuzoeana na ilifika mahali wa kupeana "huduma" Yale maongezi hayakuwa katika sauti ya chini Tena,

Mzee Mnyoka alitamani kumwambia mkewe, kuwa yeye Ni mzima wa afya tele, lakini aliogopa mkewe anaweza kutibua Mambo,

"Ah wanawake Ni wanawake tu, " Mzee Mnyoka alijisemea ,

Dokta Kimei aliendelea kumsisitiza mama Monica kuwa mgonjwa Sasa alikua na nafuu,

Wakati wakiendelea na story zao Kama kawaida baadhi ya manesi kutokana na haraka zao au kuzoeana na madaktari huwa hawapigi hodi,


Mzee Mnyoka na Dokta Kimei wakiwa wanaendelea na story zao Mara ghafla mlango unafunguliwa! Nesi Furaha alipigwa na butwa kumuona Mzee Mnyoka akiwa amekaa kitandani buheri wa afya! Lakini zaidi ya yote alisikia wazi wakiwa wanaongea, hata huu mshtuko anaona hapa Ni baada ya kuwafumania wakiwa wanaongea,

Hata hivyo alijifanya hajui kinachoendelea..

"Dokta nilikua naomba maelekezo ya contrimazole mg 200 kwa yule mtoto wa miaka 12"

Nesi Furaha aliongea..

"Hiyo ni antibiotics kwahiyo unaweza kumpa moja Mara mbili, au umpe amoxicillin mbili Mara mbili" dokta Kimei alijibu nesi Furaha akaondoka,
"Mzee Mnyoka endelea bhana na story ya Uganda , Ehh kwahyo mkafika kwenye nyumba aliyokuwemo Idd Amini"
Dokta Kimei Sasa alikua anainjoy story za Mzee Mnyoka huko vitani Uganda mwaka 1978..
"Mimi na Meja Msuguri, ndio tulikua na kamisheni 23 c,
Kwanza wenzetu wa kamisheni 19 kombaini walifika mapema Ila hawakuingia,. Ile tunashuka tu kwenye Gari ya jeshi meja Msuguri akapiga kelele dauuuniiii! Basi wote tukalala chini huku tukiwa tumeilenga nyumba ya Nduli!"


Dokta Kimei sasa alikua amekaukia kwa kicheko jinsi Mzee Mnyoka alivyokua anasimulia kwa vitendo,

"Haki ya Mungu we Mzee Ni hatari sana,. Walahi natamani ukae hapa mwezi mzima"

Dokta Kimei aliongea machozi yakimtoka kwa kucheka

*********

SAA 5:30 usiku "mgodini"

Oscar alitega vifaa vyake vizuri Kisha akavaa nguo zake za kazi, huku akimalizia na gloves zake ,

Mdogo mdogo alisogea kuelekea mgodini,


Kulikua na ukimya wa Hali ya juu mazingira ya Kijijini hakukua na pilika nyingi zaidi ya kelele kadhaa za ngoma na walevi kadhaa waliokua kilabuni.....
 
KESI YA MZEE MNYOKA 10

Oscar alizunguuka nyuma kabisa ambapo taa hazikua nyingi Kisha akajisogeza kuingia maeneo ya mgodi, alipanga kuchukua sample kwenye kichupa kidogo, na Kisha akifanikiwa kutoka ayatie dawa Fulani hivi aliyopewa, Kama yatageuka rangi na kuwa blue Basi urenium ilikuwepo kwa wingi, na Kama yatageuka kuwa njano au nyekundu Basi urenium ilikuwepo kwa kiwango kidogo na Kama yakibaki vile vile Basi Hakuna urenium kabisa,

Hii ndio ilikuwa misheni yake ya kwanza, kuhakikisha Kama madini yapo au hamna,...

Katika misheni hii Oscar alisisitizwa Sana kutumia akili kuliko nguvu, na ikiwezekana kabisa apate hizo sample bila kumwaga damu, Kwani kuwastua kokote kule kungemaanisha kufeli kwa zoezi zima,....

Oscar kwa Kunyata alisogea mti mmoja Hadi mti mwingine, alibonyeza bonyeza saa yake Kisha akaendelea mbele,..

Alisogea sogea mbele zaidi na ndipo Sasa kengele ya tahadhari ikaanza kugonga kichwani mwake,

"Sehemu Kama hii lazima itegwe"

Aliwaza huku Sasa akitembea kwa tahadhari kubwa, alitembea kwa mtindo wa 1,2 4,3 huku akisogea zaidi kuelekea kwenye visima...

Naam Kama alivyowaza kulikua na jumla ya visima 10, vitano upande wa kulia na vitano upande wa kushoto, akili zake za kipelelezi zilimuambia kuwa pengine visima vyenye Mali vikawa viwili tu au kimoja! Na vingine vimewekwa kwa ajili ya kuzuga,

Ilkuweza kuchukua sample kutoka kwenye visima vyote ingemchukua dakika 10! Taa zilikua zinawaka Sana na Sasa alikua umbali wa mita Kama 80 hivi kutoka visima vilipo na kama mita 100 hivi kuelekea kwenye majengo ya ofisi,..

Akili yake Sasa ilifanya kazi haraka, alirudi nyuma kidogo Kisha akatoa vifaa vyake vya kazi, aliunga unga na kung'ata baadhi ya viwaya hivi Kisha akatengeneza Kama kibox fulani hivi akakifunga kwenye tawi mojawapo la mti Kisha akabonyeza bonyeza saa yake Tena, halafu akazunguuka upande wa mbele wa geti,...

Kwa kawaida maeneo Kama Yale adui hawezi kupita upande wa mbele, lazima atapitia pembeni au nyuma, na ndio maana upande huu wa geti kubwa hakukuwa na walinzi wengi, Kama wale ambao alihisi watakuwepo upande wa nyuma,...


Taa zilikua zinawaka na geti lenyewe lilikuwa la kawaida tu, Oscar alipita upande wa mbele kabisa kwa kujiamini,


"Heey baharia subiri kwanza wapi saa hii?"


Alistuliwa na sauti,

"Ah broo, nisaidie Mwanao, ndio nimekuja Sasa hivi ndugu yako Sina pa kulala Kaka"

Oscar alisema kinyonge akisogea,

"Dogo hapa hatulazi watu, katafute makazi huko mtaani " alisema huku akijaribu kumzuia Oscar,

"Angalia broo Sasa hivi saa ....."

Oscar alijifanya kubonyeza saa yake na ghafla mlipuko mdogo ukatokea,..



"Dogo subiri hapa chap mtu asiingiee sawa?"

Alisema yule Mlinzi akikimbia kuelekea kule kwenye mlipuko!

Bila kupoteza sekunde Oscar alishusha mask yake usoni Sasa akawa Kama ninja na kwa spidi ya ajabu akaenda kwenye visima, ...

Havikufungwa kutokana na tahadhari, vilikua na mifuniko ya kawaida tu, alitoa vichupa vyake na kuchukua sample kwenye visima vyote , Kisha akaweka kwenye begi lake akapote akarudi kwenye geti kubwa akatoka nje na kupotelea gizani!..


"Safi Sana Oscar "

Alijisemea huku akivua Ile maski na kuitupa kwenye mtaro wa maji machafu,


Alirudi mpaka Kwenye geto lake la muda mfupi Kisha akatoa vichupa vyake,

**************

"Ni mlipuko wa baruti mkuu, ulifungwa hapa"
Mlinzi mmoja alimuonyesha boss wake sehemu ambayo alihisi bomu Hilo dogo lilitegwa

"Control room, !"
Ilikua Ni sauti ya mtu mwingine kupitia kwenye redio call,

Walinzi Sasa walirudi kwenye sehemu zao,..

Sasa Hali ya tahadhari ilitanda kwenye eneo lote,

"Mkuu, ona hapa"

Kijana wa kwenye chumba Cha kuangalizia matukio Sasa alimuonyesha boss wake ...

"Huyu hapa anachota, huyo anapitia geti la mbele anasepa!

"Shenzi kabisa ,! Shenzi Kabisa"

Aliongea yule mtu Kisha akatoka mpaka geti la mbele...

"We mwanaharamu imekuwaje mtu anapita anafika mpaka Kwenye visima halafu wewe upo hapa? Nilikuambiaje siku ya kwanza nakupa kazi hapa?" Yule mtu aliongea Sasa akitoa bastola yake na kumuelekezea yule Mlinzi,..

"Nisaheme boss nilimkatalia kuingia Ila ukatokea mlipuko nikakimbilia kule kuokoa boss"

Alijaribu kujitetea,

"Sasa sikia yule mshenzi kaja kuiba vitu muhimu Sana wewe na wenzako mumtafute usiku huu huu vinginevyo mnajua kazi yangu"

Alisema Kisha akarudi ndani

************


Oscar alikua bize kupima zile sample zake na tofauti na matarajio yake vichupa vinne tu ndivyo vilikua na nyekundu na njano,


Wakati vichupa sita vilikua na rangi ya bluu....

"Washenzi Sana hawa"

Oscar alijisemea na Kisha akatoa simu yake.....

**************************
"Ooh nzee Nyoka ilikua ntu njema, Nini Tena imepata?"
Aliuliza Padri John wakati alipomtembelea Mzee Mnyoka hospitali,


Alipewa maelezo na mama Monica na akamuonea huruma Sana,

"Basi mama ngoja tuombe Mungu asaidie Nzee Nyoka ipone,.

Mama Bikra Maria, utuombee sisi kosefu tumekosa, angalia Nzee Nyoka,. Imelala, Kuna maumivu au ugonjwa sisi hapana jua, lakini wewe Mungu unaona, msaidie, na msaidie mke wake , Mama Monica, mpe nguvu , ..tunaomba haya katika Jina la Mwanao Yesu Kristu Mokozi wetu, ameen"


Padri John alimalizia maombi yake huku Mzee Mnyoka akitamani kuangua kicheko pale kitandani,..


Sasa Ni siku ya 5 Mzee Mnyoka akiwa kitandani kimya,

Mkewe Sasa alianza kupata matumaini baada ya Mzee Mnyoka kuanza kufumbua macho na kuangalia huko na huko, ingawa alikua hawezi kuongea lakini mkewe alipata matumaini,..

*******

Msako mkali uliendelea kule msituni pamoja na maeneo ya Karibu kumtafuta Oscar lakini hakukuwa hata na dalili kuonekana kwake,


Sasa kikao Cha dharula kikaitishwa ili kujadili Hali iliyojitokeza...


"Huu Ni uzembe wa Hali ya juu, sote tunafahamu madhara yake endapo yule mshenzi atafikisha sample hiyo serikalini"

Mr Bill au "Carlos" Kama wapambe wake walivyozoea kumuita Sasa aligonga meza ..


"Yaani Tony, Frank, Jacob, eeh, mtu anaingiaje hapa na kuchukua sampuli?"

Hivi vifua vyenu mnavyojazia hapa mnamjazia Nani?

Mpuuzi mmoja tu anawazubaisha na baruti za kitoto anaiba sample anaondoka halafu mnajiita vidume!"

Mr Bill aliongea huku akiwa amekasirika Sasa, hakuna aliyeongea chochote,

"Boss Mimi nahisi kuna mtu katoa taarifa huko serikalini na ndio wakamtuma huyu mpelelezi"

"Eehee mi nilishasema yule Mzee Mnyoka tumpoteze, tangu mwanzo kabisa"


"Mzee yule hajiwezi...."


"Pumbavu sijasema mtu aongee.....


Frank, kesho asubuh mpaka kufika saa nne uniletee habari za Mzee Mnyoka kupitia simu, ulishasema Kuna nesi una mahusiano nae pale Sasa jifanye upendo unakuzidi nguvu, unanijua vizuri,..


Halafu iwe Mzee Mnyoka anaumwa kweli au anajifanya nataka kesho usiku uniambie yule Mzee Ni maiti, Tony wewe utakuwa na vibarua hapa na hakikisha kila sura unayotilia mashaka unadili nayo,

Jacob, utakuwa na Mimi kwenye main,. Haya toeni vifua vyenu hapa, "


Alisema Mr Bill vijana wale wakatoka mle,

Bill au Carlos Kama ambavyo wapambe wake walimuita ndie alikua muangalizi wa kituo hiki lakini kiuhalisia wamiliki wa kitalu hiki walikuwa watatu,

Mr Johnson ambaye ndie mmiliki wa kampuni ya UreFact yeye aliishi uingereza na Bwana Tito Kimbikile, waziri wa Nishati na Madini,

Huyu kazi yake kubwa ilikua kuipamba kampuni hii kwenye vyombo vya habari, na vile vile kuitetea huko serikalini kuwa bado utafiti haujakamilika na hivyo wasamehewe kodi, huku akiendelea kulipwa mamilioni kwa Siri,

Na mtu wa tatu alikua Askofu Majimbi, huyu alimiliki makanisa zaidi ya Mia tano, lakini nyuma yake alikua ndie mwakilishi wa kampuni ya UreFact nchini Tanzania...

Bill yeye alikua msimamizi wa kitalu Kama mkuu wa kituo....
 
Episodes nyingine zitaendelea baada ya game ya watani kupita!!
mwandishi anaandika vizuri , hakuna matukio fikirishi yenye utata katika maisha yetu ya kila siku

Kuna story ukisoma sura mbili tatu unaona kabisa hapa no tunapigwa , ila hii inatililika na maisha halisi japo kwenye case procedure kwenye kesi ya mzee kuna ukakasi kidogo

Imeanza kama story za kijijini za visa vya uchawi wa kibabu kibabu, mwandishi kapiga change kota juu kwa juu , imekuwa ya kijasusi

Kama we ndio mwandishi heshima kwako, uwe unanitag
 
mwandishi anaandika vizuri , hakuna matukio fikirishi yenye utata katika maisha yetu ya kila siku

Kuna story ukisoma sura mbili tatu unaona kabisa hapa no tunapigwa , ila hii inatililika na maisha halisi japo kwenye case procedure kwenye kesi ya mzee kuna ukakasi kidogo

Imeanza kama story za kijijini za visa vya uchawi wa kibabu kibabu, mwandishi kapiga change kota juu kwa juu , imekuwa ya kijasusi

Kama we ndio mwandishi heshima kwako, uwe unanitai
Hamuwezi Jutia kusoma hii story wanangu wa faida. Waswahili wanaita Bonge la story na mwandishi anamaliza hajawahi zingua. .

Analyse Half american Watu8 Numbisa Amehlo Depal wao ni wao Shunie Kalpana Dejane leadermoe Antonnia Lovelovie Depal Darlin Nuzulati Synod Binadamu Mtakatifu Johnnie Walker Glenn Mamaya Dahan moneytalk Cee Omar B Salum Dr Restart Numbisa Mo mp5 Santos06 Angel Nylon baby zu shikamkono01
 
mwandishi anaandika vizuri , hakuna matukio fikirishi yenye utata katika maisha yetu ya kila siku

Kuna story ukisoma sura mbili tatu unaona kabisa hapa no tunapigwa , ila hii inatililika na maisha halisi japo kwenye case procedure kwenye kesi ya mzee kuna ukakasi kidogo

Imeanza kama story za kijijini za visa vya uchawi wa kibabu kibabu, mwandishi kapiga change kota juu kwa juu , imekuwa ya kijasusi

Kama we ndio mwandishi heshima kwako, uwe unanitag
Karibu mkuu story naandika Mimi mwenyewe
 
Back
Top Bottom