Hadithi: Kesi ya Mzee Mnyoka

Hadithi: Kesi ya Mzee Mnyoka

Mtani mbona nilikuita mwanz bas mda mwingine tag zinasumbua kwanza haziji Hii story hutojutia kabisa. .
Naanza sasa kusoma. Labda ulitag wakati niko banned. Nilikuja kuta nofifications nyingi, nikazitema 😒
 
Naanza sasa kusoma. Labda ulitag wakati niko banned. Nilikuja kuta nofifications nyingi, nikazitema 😒
Nakutag sana kwenye story nzuri unapitw 😀 humu ndio sehem za kutolea stress

Utakuja chukua ubingwa tuzo za kuwa banned😀 acha ukorofi bas mtan
 
KESI YA MZEE MNYOKA 30

Rajabu aliondoa gari pole pole pale hotelini Kisha wakachukua barabara kuelekea mwenge Rajabu aliongeza mwendo sasa Kama kawaida yake mita Kama mia tatu mbele kulikua na makutano ya barabara ya hivyo alitaka kupunguza mwendo ili aingie kulia maana bosi wake alikua Ana 'kikao' kingine maeneo ya mwenge

Kwanza alidhani hajakanyaga vizuri breki, lakini baada ya kujaribu na breki ya mkono sasa Rajabu alipiga kelele,

"Bosi funga mkanda breki zimegomaa!"

"Unasemaje wewe!?"

Shija sasa alichanganyikiwa,


***************

Tito alitoka pale barazani halafu akarudi chumbani kwake, aliwasha TV huku akipangusa uso kwa viganja vyake jasho lilikua linamtoka,


Alifungulia kituo Cha Televisheni Cha Dar TV,

Naam baada ya dakika nane hivi maandishi ya "BREAKING NEWS"

yalitokea,

"Habari za wakati huu ndugu mtazamaji wa dar TV, habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa waziri wa miundo mbinu , mheshimiwa Anthony shija, amepata ajali ya gari na kupata majeraha makubwa, mwandishi wetu Brian Kidude yupo eneo la ajali,

"Brian tuambie Hali ipoje hapo....



"Farida, kwakweli Hali ya hapa Ni majonzi kweli kweli mashuhuda wa tukio wanadai gari ya mheshimiwa ilitokea maeneo ya kimara hivi, na ilipita kwa Kasi kabla ya Dereva kushindwa kukata Kona kuelekea hii njia ya kawe, na hatimaye likagonga nguzo ya umeme na kupinduka hapa darajani Kama unavyoona"

"Sasa Hali ya majeruhi ikoje mpaka sasa?"

"Aah Farida nikujuze tu kwamba , Dereva alifariki papo hapo lakini mheshimiwa yeye amepata majeraha na hivyo tutasubiri ripoti ya madaktari pale Alfa ambapo ndipo anapofanyiwa matibabu, "


" Nikushukuru Sana Brian Ni matumaini yetu kuwa utafika hapo Alfa hospital ili utupe mrejesho zaidi"

Alisema mtangazaji wa Dar TV

Tito alihisi furaha, hofu na huzuni kwa pamoja,

"Huyu mshenzi asije akapona tuu"

Alijisemea Tito sasa akitoka pale Hotelini ili aende huko hospitali kumuona Shija.


************

Mzee Mkude aliingia kwenye Gari lake na kuondoka, alipitia kijijini na kutoa "pole"

Kwa familia ya Mzee Mnyoka huku akiagiza mtendaji wa Kijiji na viongozi wengine kushirikiana ili Mzee Mnyoka apatikane

"Uongozi wa tarafa unasikitika Sana,
Tukio hili Ni la kwanza kutokea katika Kijiji chetu hivyo tushirikiane kuhakikisha mwenzetu anapatikana"

Alisema Mzee Mkude huku akionyesha Hali ya huzuni,

*******************

Josephine pamoja na Askari wenzake wanne walikua kwenye Gari huku wanne wengine wakiwa kwenye piki piki walifika mpaka Kinjeki na kupitiliza kuelekea msituni

Maeneo Yale hayakuwa mageni kwao hivyo walifika na kuacha Gari umbali wa mita Kama Mia tano hivi Kisha Askari ambao hawakua na yunifomu wakatangulia kwenye piki piki,

Na kuacha piki piki zao mita Mia mbili Kisha wakashuka na kuelekea ilipo nyumba,

Josephine alijongea na wenzake huku wakiwa wanajificha mti mmoja baada ya mwingine,

Askari wale walifika na kuwaona walinzi wawili wakiwa wamekaa tu wakivuta sigara,..

"Mpo chini ya ulinzi"

Walistuka huku mmoja akijaribu kukamata bunduki yake ambayo alikua ameiweka chini,

"Usijidanganye kugusa iyo bunduki, wekeni mikono juu na msogee hatua moja mbele"

Walitii sasa huku wakiacha bunduki zao

Askari mmoja alisogea na kuwafunga pingu Kisha wakawasachi na kutoa bastola moja na visu viwili pamoja na vipisi vya sigara,

Wakati huo huo Josephine alifika na wenzake,

Askari walikua 7 huku Dereva pekee akiwa amebaki kwenye Gari,

"Mzee Mnyoka Yuko wapi?"

Aliuwauliza Askari mmoja huku akiwanyooshea bunduki,

"Yupo kule stoo, sisi hatuna makosa afande"

Alisema yule jamaa mmoja

Askari wawili walienda na kufungua na kumtoa Mzee Mnyoka ambaye sasa aliona miujiza mingine inazidi kumtokea kwenye maisha yake,

Polisi walimpa maji ya kunywa ambayo Mzee Mnyoka alikua Ana hamu nayo kuliko kawaida,

walimkokota Mzee Mnyoka na kurudi nae huku wakiwasindikiza wale jamaa kuelekea kwenye gari

Tito akiwa kwenye Gari alipigiwa Simu na Askofu Majimbi,

Alimpa pole kutokana na ajali iliyokuwa imempata waziri mwenzao,


Tito nae alimjibu kuwa Yuko njiani kuelekea hospitali kumuona,

Hii ilikua ni mbinu tu ya kuwasiliana ili Kama yupo anayefuatilia maongezi yao asiweze kutambua chochote,


Dakika 12 zilimtosha Tito kufika hospitali ya Alfa, alishuka haraka huku waandishi wa habari wakiendelea kuripoti tukio Hilo, alifika na kuelekea wodi alipokuwa waziri Shija hata hivyo alishindwa kumuona kwani tayari alikua chini ya uangalizi wa madaktari kwenye chumba mahututi,


Tito alikua anaomba mizimu yake itokee miujiza yoyote Shija apoteze uhai wake,

Baada ya muda mfupi sauti ya ving'ora ilisikika na Raisi nae alifika kumjulia Hali waziri Shija, ndipo sasa Tito akapata nafasi ya kujichomeka kwenye msafara wa raisi ambaye baada ya taratibu ndogo kufanyika aliruhusiwa kumuona Shija

Alikua amezungushiwa mipira pamoja na bandeji karibia mwili mzima, mashine za kupumulia ziliendelea kufanya kazi yake na Raisi hakukaa Sana alitoka nje ya hospitali na kutoa hotuba fupi,

"Kwahiyo nimemuagiza IGP afanye uchunguzi haraka kujua chanzo Cha ajali , na nani aliyesababisha, maana kamanda wa barabarani anasema waligundua breki zote zilikatwa kabisa, haiwezekani Gari ya waziri ikatwe breki zote hivi hivi na huyo mtu asijulikane, kwahiyo niseme hatua zinachukuliwa na niseme tu ndugu zangu waandishi mripoti hili Jambo vizuri maana mmekua na kawaida ya kupindisha pindisha

Alisema Raisi
Sasa Tito alikua anajisikia tumbo kunguruma, aliona wazi wazi sasa mambo yanataka kumgeukia....

*****************

Polisi waliwasili kijijini Kinjeki na Mzee Mnyoka alienda nyumbani kwake kupata chakula na kubadili nguo Kisha akaongozana na polisi kwenda kutoa maelezo ,

Mzee Mnyoka alieleza kila kitu kuanzia siku ile anatekwa na kupelekwa kule porini, isipokuwa mambo ya mgodi wa Kinjeki hakutaja,

Polisi walichukua maelezo na Kisha wakampeleka hospitali kufanyiwa vipimo zaidi,

Mzee Mnyoka hakuonekana na madhara mengi zaidi ya michubuko tu na maumivu kidogo kichwani hivyo aliruhusiwa na kurudi kwake,

Wale vijana baada ya kuhojiwa walikiri kutumwa na Mzee Mkude na hivyo bila kuchelewa amri ya kumkamata Mzee Mkude ambaye alikua katibu tarafa ya Kinjeki sasa ilitolewa,


Wanakijiji walipigwa na butwaa kusikia Mzee Mkude ndie aliyefanya mipango yote Tangu mwanzo ya kumtengenezea kesi Mzee Mnyoka,..


****************

Mzee Mkude alipata taarifa kutoka kwa shushushu wake kuwa Mzee Mnyoka alipona na vijana walimtaja,

Sasa hakuwa na namna zaidi ya kufanya Jambo...
 
KESI YA MZEE MNYOKA 31

Shija Yuko mahututi hospitali, Raisi anaagiza uchunguzi ufanyike, Tito sasa tumbo Joto,

Mzee Mkude nae anataka kutiwa nguvuni,


Sasa endelea,


Mzee Mkude alikua katika kufanya Jambo ghafla ujumbe mfupi uliingia kwenye Simu yake,

"Kubali kujisalimisha ila usitaje chochote, tupe siku tatu tunakutoa hapo
Chief"

Mzee Mkude sasa alipumua, alijua wazi wenzake wasingeweza kumtelekeza maana anaweza kuwataja hivyo sasa alijiweka sawa kabisa kukamatwa na polisi,

Ambao walifika muda mfupi, kwanza polisi wenyewe walishangaa kukuta Mzee Mkude anawasubiri na Kisha akatoka nao bila kuonyesha ukaidi wowote,

Mzee Mkude baada ya mahojiano mafupi alisema hajui chochote, na hata hao vijana hawafahamu,

Aliendelea kubaki kituoni huku mawasiliano yakifanyika ili aweze kupelekwa kwenye gereza kuu la wilaya ili asafirishwe kwani kituo kidogo Cha polisi hawakuwa na mamlaka ya kushikilia mtuhimiwa wa utekaji,


**************

Wakiwa pale hospitali askofu Majimbi nae alifika akiwa ameongozana na walinzi wake Kama ilivyokua kawaida yake, Tito alikua amebaki pale huku akisubiri kujua hatma ya Shija Kama anakufa au anapona, asingeweza kutoa mguu wake pale hospitali kabla hajaelewa Hali ya Shija, na hivyo waandishi na madaktari walimchukulia Kama waziri aliyekuwa ameguswa na ajali ya rafiki yake kipenzi,

Askofu Majimbi alimsalimia Tito huku akimpa mkono,


"Poleni Sana , na pole Sana na wewe kwa ajali ya rafiki yako, Mimi najua mlivyokua mnapendana kwakweli Mungu akutie nguvu Ndugu waziri"


Aliongea askofu Majimbi, maneno haya yalitaka kumfanya Tito acheke lakini akajikaza tu kutokana na msururu wa waandishi wa habari waliokuwepo,

Baada ya muda sasa daktari alitoka kutoka chumba Cha upasuaji alipokuwepo Shija,

Waandishi sasa walisogea alipokuwepo huku Tito nae akikimbia kusikiliza


"Yeah kwakweli Kama mlivyoona kwenye ajali , Mheshimiwa alipata majeraha mengi makubwa, alikuja hapa akiwa amepasuka fuvu la kichwa na damu nyingi imevuja kwa ndani, tumejitahidi Sana kumfanyia upasuaji kwa kuondoa damu iliyokuwa imevujia ndani, lakini pia tumemfanyia Skull check up, na niseme kwa sasa mheshimiwa bado Yuko unconscious kwa maana kwamba bado hajitambui lakini tunaamini lolote linaweza kutokea Tuzidi kumuombea kwa Mungu"

Alimaliza daktari huku waandishi wakiuliza maswali


"Kwa maana hiyo kwa Hali yake mnavyoiona, hakuna haja ya kumsafirisha nje ya nchi?"

Aliuliza mwandishi mmoja,

"Kwasasa Ni mapema mno, maana kinachoendelea kwa sasa sio matibabu Bali Ni recovery process! Kwa maana kwanza tunajaribu kurudisha fahamu zake kwanza, ndipo utaratibu mwingine sasa utafuata, "


Alijibu daktari,

"Kwahiyo tuseme sasa anaweza kuchukua siku ngapi Hadi kuzinduka?"
Mwandishi mwingine aliuliza


"Kuzinduka Kama nilivyosema Ni process, Ni mchakato, unategemea vitu vingi, mawasiliano ya ubongo, uti wa mgongo, na vitu vingi, naomba kwanza mtupe muda siwezi kusema kabisa exactly lini , siwezi kusema atazinduka Leo au kesho, "

Alijibu daktari

Sasa Tito alijisikia viungo kulegea na akamfuata Majimbi wakashuka ngazi kutoka nje..


*************

Mzee Mnyoka sasa alikua anawaza namna alivyonusurika, imekuwaje polisi wakajua nilipo?

Sasa Mzee Mnyoka aliingiza mkono kwenye pindo la bukta yake na kutoa kile kidude Cha mviringo,


Alikikagua Kisha akaona maandishi madogo "GPS" alikirudishia sehemu yake Kisha akatoka na kwenda chumbani kwa mwanae James ambako kulikua na vitabu vingi vingi ikiwemo kamusi,

Alitafuta Hilo neno GPS na kukuta kumbe Ni ufupisho wa Global Positioning System

Sasa Mzee Mnyoka alikumbuka neno hili halikua geni masikioni mwake,


Ndipo sasa akakumbuka alipokuwa Hospitali Dokta Kimei aligusia kuhusu usambazi wa Dawa ambapo magari mengi ya dawa yamefungwa GPS kwa ajili ya kujua yalipo..

Mzee Mnyoka alielewa somo,


Mzee Mnyoka aligundua kifaa kile ndio kilimsaidia kuweza kuokolewa,

Watu waliendelea kuja nyumbani kwake alikua amesimulia kuhusu kutekwa kwake mpaka amechoka,

Baadae aliamua kurudi ofisini na kuendelea na kazi zake Kama mwenyekiti wa muda,

Moyoni alikuwa akitamani Sana Mzee Mkude na genge lake waweze kuchukuliwa hatua Kali Sana,

****************


"Naona umejaa hofu na wasi wasi kwani mipango ilikuwaje?"
Sasa alikua anauliza Askofu Majimbi wakati wakiwa nje ya geti kuu,


"Niliagiza vijana wawili ambao wakati Shija anakuja pale hotelini mmoja alikua Ni mwanamke akamzuga Rajabu Dereva wa Shija akatoka nae kwenda sehemu ya kuogelea, halafu mponda yeye akiwa amevaa nguo za mafundi gereji ndio akaingia chini ya Gari akafanya alichofanya, alipomaliza akanitumia ujumbe na uzuri Ni kuwa hakuna mtu aliyekuwa amemshuku

Kwahiyo walipoingia kwenye gari ndio breki zikafeli wakapata ajali"


Alikuwa anaongea sasa Tito huku akiangalia huko na huko kuona Kama Kuna mtu anafuatilia maongezi yao,

"Umefanya sehemu yako lakini ujue Mimi sijaja hivi hivi hapa hospitali nimekuja na kijana mmoja ambaye nilitoka nae Korea ya kusini juzi na anamaliza hii kazi hapa hapa hospitali muda huu , unajua nilikua nataka...............

Ghafla walikatishwa na kundi la waandishi wa habari waliokuwa wanakimbilia ndani ya hospitali,


Sasa waliangaliana Kisha nao wakakimbilia ndani,


Walifika sasa na kukuta Mganga Mkuu wa hospitali akiwa amezunguukwa na waandishi wa habari,


"Kwahiyo sasa kwa Hali ikawa imebadilika na madaktari walifanya kila walichoweza ila ndio hivyo tena kuwa Mungu alimpenda zaidi"

Sasa Tito alimtazama Majimbi Kisha akashusha pumzi ndefu,


waandishi wa habari walizidi kumiminika pale hospitali na baadae serikali ilitangaza Rasmi kutokea kwa kifo Cha waziri wa miundo mbinu Bwana Anthony shija


***************

Mzee Mkude alipelekwa kituo Cha kati Cha polisi kwa ajili ya mahojiano na pamoja na kuhojiwa na kupewa kipigo bado mzee Mkude alisema hajui chochote,

Hatimaye iliamuriwa Mzee Mkude ahamishiwe kwenye kituo kingine ambako polisi wa Kanda maalumu wangeweza kumuhoji, hii ilitokana na Aina ya silaha ambazo walikuwa wamekutwa nazo wale vijana, hii ilipelekea polisi kupata wasi wasi kuhusu uwepo wa genge la kihalifu,

Mzee Mkude aliongozana na polisi wa Nne waliokuwa na bunduki, walitumia Gari ya polisi ambayo ilikua inatumika kupeleka wafungwa wachache kwenda mahakamani,

Waliendelea na Safari huku Mzee Mkude akitegemea kuwaona watu wake muda sio mrefu,


Ni wakati wanakatisha kwenye pori kabla ya kutokea Bomang'ombe ndipo kwa mbali akaonekana Mzee akichechemea Kati Kati ya barabara,


Dereva wa polisi alipunguza mwendo na kusimama kabisa huku akisubiri Mzee apite,

Lakini kwa ghafla Mzee yule alitupa koti lake na kusimama wima na Kisha alitoa bunduki kubwa ya kivita Aina ya ak 47 akamimina risasi nyingi , kufumba na kufumbua walitokea wengine wanne wakiwa na bunduki huku wamejifunika sura zao,


Polisi hawakupata muda wa kujitetea kwenye shambulizi Hilo la ghafla,
Sasa wale watu walisogea kwenye Gari ambapo Mzee Mkude alikua amelala akiwa amechafuka kwa damu za Askari wale waliokuwa maiti tayari,


"Twende chief"

Alisema mmoja huku akimpa mkono Mzee Mkude

Mzee Mkude alishuka kwenye Gari Kisha wakamfungulia pingu na kuingia kwenye pori,


Kwa bahati mbaya Askari mmoja hakuwa amejeruhiwa Sana alivuta bunduki yake Kisha akamlenga Mzee Mkude kichwani na kuachia risasi mbili
Mzee Mkude akaanguka chini akiwa maiti,


Aliachia risasi nyingine ambayo ilimpata mtu mwingine kwenye shingo,

Kabla hajaachia nyingine na yeye alianguka chini baada ya kupigwa risasi ya kichwa,


Watatu waliobaki walikimbilia porini na kutokomea...
 
KESI YA MZEE MNYOKA 32


Mzee Mnyoka alikua amepata taarifa zote jinsi Mzee Mkude alivyopoteza maisha, zaidi Sana Mzee Mnyoka alipigwa na butwaa jinsi Mzee Mkude alivyokuwa na mtandao Mpana wa uhalifu,

Haikuishia hapo polisi walifika mpaka nyumbani kwa mzee Mkude na kufanya msako ambako walikuta bunduki moja na kiasi Cha pesa shilingi millioni 5

Mke wa Mzee Mkude alisema hakujua chochote kwani alidai mumewe alikua na biashara zake ambazo yeye hakuzijua,

Ni Mzee Mnyoka pekee pale kijijini aliyekuwa anajua madudu ya Mzee Mkude, na chanzo Cha utajiri wake huo wa ghafla.


***************


Mgodini Kinjeki sasa katika ukumbi wa mikutano kulikua na kikao Cha dharula haswa baada ya kupoteza watu kadhaa katika mapigano na polisi,


Sasa Bill alikua amekasirika Sana

"Frank na Jacob hii Ni Mara ya pili mnaniangusha ndani ya mwezi mmoja, ifikie hatua sasa niwapige chini, naona mnaanza kuzeeka kuliko mimi

Mmeshindwaje kuja na Mhusika hapa, muone na wewe Jacob hivi kwanini wasingekupiga tu risasi ya kichwa wanakupiga begani? Nasema hivi siku yoyote kuanzia sasa nitabadilisha kazi zenu, mmekuwa wazembe Sana, haya ondokeni hapa!"

Aliamuru Mr Bill,

Huku akiwasha sigara yake Kama ilivyo kuwa kawaida yake,

Kama walidhani Mr Bill alikuwa amekasirika sababu ya kupoteza vijana wake Basi watakua wamekosea Sana,


Mr Bill alishaona hatari ya kazi yake ambayo anaifanya ya kulinda maslahi ya watu wengine huku yeye akipata posho ambayo yeye aliona haimtoshi, ndipo sasa wakati waziri Shija anakuja kuzindua barabara ya kunganisha wilaya ya Komboi na wilaya ya Mkomazi kupitia Kinjeki,


Alikaa nae na kumpa huo mchongo wa mgodi,


Makubaliano yao yalikuwa kila mwezi alipwe milioni Mia mbili, halafu waziri apate milioni Mia moja, hivyo walipatana kila mwezi "wawapige" Akina Tito shilingi milioni Mia tatu!


Ni wakati Shija anarudi kwenye Gari akaona "hawezi kula" kidogo na Mr Bill ndipo yeye akapandisha dau mpaka milioni 500 kwa Tito ili yeye awe anachukua millioni Mia tatu kila mwezi,



Shija alikua na malengo pia ya kuja kummaliza Mr Bill hapo baadae ili awe anachukua mgawo wote Peke yake,


Kitu ambacho mr Bill hakufahamu!


Billi hakutaka kujulikana kuwa ameuza Siri kwa Shija, na hata njia zao za mawasiliano hawakutumia Simu kabisa,

Sasa kusikia kifo Cha kutatanisha Cha Shija, Billi alizidi kuwachukia wakuu wake.

***************


Viongozi mbali mbali wa serikali sasa walikuwa kurasini jijini Dar es salaam tayari kabisa kwa ajili ya kuaga mwili wa Mheshimiwa Anthony Shija,


Waziri Tito Kama kawaida yake alikua amevaa suti yake nyeusi na miwani ya jua,


Nyimbo za maombolezo zilikua zinasikika na viongozi mbali mbali wa dini na kisiasa walikua wanaendelea kufika,

Ni wakati huo sasa Kamanda wa Kanda maalumu alifika na moja kwa moja alifika kwa waziri Tito,


"Samahani mheshimiwa naomba tufuatane kwenda kituoni"


Alisema Kamanda

"Kamanda Kuna nini maana Kama unavyoona hapa Kuna Jambo muhimu"


Alisema Tito sasa akionyesha kushtuka


"Nasikitika kuwa wewe Ni miongoni mwa washukiwa wa katika kusababisha ajali ya kifo Cha waziri Shija"

Alisema Kamanda.

"Ha Kamanda, utakua umekosea Sana, ! "
Sasa alisema Tito kwa sauti ya chini huku akielekea kwenye gari la polisi,

Mapigo ya Moyo yaliongezeka..

"Mheshimiwa waziri kwanza tunahitaji tu ushirikiano wako ili tuweze kumaliza mapema "

Alianza Kamanda wa Kanda maalum,

"Kwanza afande Mimi nahusikaje katika Jambo hili?"

Aliuliza Tito,

"Sikiliza mheshimiwa, wewe ndio ulikua na marehemu pale Rombo Bar, na hata mawasiliano kwenye Simu yake yalionyesha wewe ndio ulikua umempigia Simu"

Alisema afande

"Kwahiyo Mimi kumpigia Simu aje Rombo hotel ndio nahusika? Kwani Ni Mara ya kwanza Mimi nawasiliana nae? Au hakuna watu wengine waliokuwa na mawasiliano nae? This is ridiculous!"

Alisema Tito akimalizia na Kingereza Kama ilivyo kawaida yake..

"Sisi hatusemi Kama wewe umemuua, lakini polisi kazi yetu Ni kuchunguza Kama ........"

Afande nae alikatishwa na kijana wake aliyekuja na kumnong'oneza Jambo na Kisha akaondoka,

"Sasa mheshimiwa waziri tukiwa na Jambo lolote Tena tafadhali tunaomba ushirikiano wako kwasasa tuseme kwamba tunaweza kuishia hapa kwa leo"

Alisema afande Kisha akatoa mkono kumpa Tito ambaye aliukataa..

"Jiangalie Sana Kamanda"

Tito aliongea huku akitoka pale kituoni Kisha akaangaza macho na tayari alimuona Dereva wake akiwa anamsubiri Kisha akarudi msibani.

***********


"Nadhani kila kitu tayari, George ameenda Nairobi Mara moja Kuna mzigo wetu kutoka China ameufuata kutokana na vifaa vyenyewe vilikuja kwa ajili ya serikali ya Kenya na ya kwetu pia,

Hivyo kwasasa tunakutegemea Sana Oscar, Sina Shaka na uwezo wako , na jitahidi kufanya Jambo hili liishe salama na baada ya hapo nitafikiria kukupa Ile likizo yako , naamini this time around utaenda kuoa kabisa kupitia hiyo likizo yako"

Ilikua ni hotuba fupi ya mr Allan akimueleza kijana wake Oscar,


"Yeah, kwa namna Tito anavyoelekea Ni kuwa siku si nyingi Mr Johnson atakuja, ingawa sijajua kiuhalisia atakaa siku ngapi na Ni lini atatembelea mgodi wa Kinjeki,"

Alisema Oscar,

" Kesho jioni nitajaribu kuangalia kama kuna booking yoyote yenye jina la Mr Johnson imefanyika halafu tutajua, Kama ndio yeye daima imetupasa kuwa mbele yao, kabla ya mtu mwingine, sidhani Kama Nina haja ya kukumbusha hili Oscar"

Alisema Mr Allan,

"Sawa Mkuu Mimi ngoja nimpitie Tito naona Yuko bize na msiba wa Rafiki yake Shija,"

Alisema Oscar

"Ah Tena umenikumbusha, Leo bado kidogo wale wapuuzi wangetuharibia mambo,"


"Walimuita Tito kumhoji kuhusiana na kifo Cha Shija, Kuna jicho pale Rombo , ambaye aliniambia kuwa Tito alikaa na Shija kwenye meza moja, baada ya hapo Kuna vijana wawili walikuja mmoja alikua msichana alienda kwa Dereva wa Shija na kutoka nae na baadae huyo mmoja alijifanya Fundi na kukata breki"

Alikua anasema sasa Mr Allan,

Oscar alikua amevuta picha sasa bosi wake Tangu atoke Dodoma alikua amebadilika mno, hakuwa na furaha Kama Yule Tito aliyekuwa anamjua,

"Kuna kila dalili Tito anahusika na Kifo Cha Shija, Ila wangemtibua Sasa hivi wangetuharibia ndio maana nilizuia asihojiwe kwanza"

Alisema Mr Allan,

"Mmhhhh nahisi huko mbele tutapata mengi kuhusu Tito"

Alisema Oscar huku akisimama na kuondoka zake,

Alishuka ngazi na kuingia kwenye bajaji moja

"Twende zetu buguruni"

Alisema Oscar,

Akili yake sasa ilishaanza kutamani kazi, kukaa tu bila kazi kwa mpelelezi Kama yeye hakutaka kabisa , na hivyo akaona apekenyue kidogo kuhusu kuhusika kwa Tito katika kifo Cha Shija labda akapata kitu fulani,

Walifika mpaka buguruni ,Kisha wakaingia malapa,

Angalia pale wanapochonga vitanda pale niache,

Alisema Oscar Kisha akatoka na kulipa halafu akaingia mitaani mpaka kwenye nyumba moja hivi iliyokua imechoka choka,

Aliruka matairi yaliyoukuwa yamewekwa kwa ajili ya kukanyaga wakati wa mvua,

Alitokea kwenye chumba chenye mlango wa bati ambapo nje kulikuwa na maspea ya tv na redio mbovu,

Kisha akagonga ule mlango..
 
KESI YA MZEE MNYOKA 33

"Boss kwani Polisi walikua wanasemaje,"

Aliuliza Dereva wake Tito
"Ah polisi bhana , si unajua kila mmoja anataka apate sifa siku hizi, wanadai eti Simu yake ya mwisho ilitoka kwangu,"

Aliongea Tito huku akiweka sawa tai yake,

Dereva alishaona Bosi wake hakupenda kuendelea na Yale maongezi hivyo alikatisha mitaa huku akiongeza sauti kidogo ya muziki,

Kuelekea moja kwa moja Kurasini kwenye msiba,

Tito moyoni alifurahi Sana kwani hakukuwa Tena na kidudu mtu kwenye mipango yake,



"Nadhani Baada ya mazishi sasa Johnson aje achukue mzigo wake, kabla mambo hayajaharibika"

Alijisemea moyoni


**************


"Oya jini uko wapi man!"

Oscar alibisha hodi huku akijaribu kushika mlango,


"Dah mwanangu mwenyewe, umenitosa Sana baharia wako, aisee "

Ilisikika sauti ndani yenye uchovu kiasi,


" Dah man vipi Tena mguu aisee?"

Aliuliza Oscar sasa akiangalia yule mtu ambaye alikua amelala kitandani huku mguu ukiwa na bandeji kiasi,

Chumba kilijaa vifaa vya umeme zikiwemo komputa na televisheni zilizokuwa zimefunguliwa funguliwa, na vifaa vingine vikiwa vimezagaa chini,

"Basi tu majanga ya kibaharia mwanangu, Ila kwakua umekuja najua Leo nitapata hela ya msosi kabisa"

"Hilo Tena hata usiwaze sasa Kuna fala mmoja hivi nataka unichekie meseji zake za Jana na juzi, hivi "

Alisema Oscar huku akitoa Simu yake,

"We boya si unajua dili zako zinavyokuwa za hatari juzi Kati ukasababisha niuze mpaka cpu yangu kutokana na kufuatiliwa, sema Basi tu wewe Ni mwanangu"

Alisema yule jamaa huku akikaa pale kitandani Kisha akavaa miwani yake halafu akasogea mezani kwenye komputa moja iliyochakaa hivi akaiwasha,


"Lete izo namba na sasa iwe bahati yako apokee, vaa hizi halafu unataka tumpigie kutoka wapi?"

Aliuliza

"Itokee Bamida- Ujemi"

Alisema Oscar, Oscar angeweza kufanya kazi hii ofisini kwao lakini hakutaka kuonyesha mambo mengi Sana maana kwa uzoefu wake asingeweza kumuamini kila mtu,

Ndipo sasa alikuja kwa huyu mtu wake ambaye wengi walimjua Kama Fundi TV na komputa lakini Oscar alimfahamu vizuri John,

Mwaka 1998 John alimaliza chuo kikuu nchini Thailand katika maswala ya teknolojia ya mawasiliano, alirudi nchini na kuajiriwa na benki kuu, mwaka 2000 John pamoja na wenzake sita walihukumiwa kifungo Cha maisha jela kwa kuitia hasara serikali trillioni zaidi ya 2,

John alifanikiwa kumpenyezea Mr Allan ukweli wote wa mambo kuhusiana na upotevu ule, Gavana wa benki kuu aliondolewa kwenye nafasi yake na hatimaye akafariki katika ajali ya kutatanisha, John alitoka gerezani lakini siku moja baadae alivamiwa nyumbani kwake na nyumba yake kuchomwa Moto, Ni bahati Oscar alikua amewahi na kumuokoa na ndipo sasa akafanyiwa upasuaji mdogo wa sura na kubaki Kama kibarua wa Mr Allan, kwa kazi mbali mbali,


John alikuwa na uwezo wa kipekee wa kucheza na komputa na ndio maana Oscar akamuita Jini..


"Haya ongea nae"

Alisema "Jini" huku akiwa anabonyeza bonyeza komputa yake,

"Oscar aliongea na Tito huku sauti yake ikiwa imebadilishwa, alijatambulisha kama mwenyekiti wa wazazi wa kata anayotoka waziri Tito na alikuwa na Shida,


Haya yote yalifanyika ili kuunganisha Simu ya Tito mpaka kwenye vifaa vya Jini,
Aliendelea kuongea kwa nusu dakika mpaka Jini alipomuonyeshea alama ya dole gumba ..


****************************************

Mgodini Kinjeki sasa Hali ya mambo ilikua shwari kabisa,

Walipewa wiki moja ya kujiandaa kwa ajili ya kupokea ugeni wa Mr Johnson, kutoka uingereza, yeye angefika kwa ajili ya kuona Kama kampuni yake imefanikiwa kugundua chochote katika utafutaji wa Ureniamu pale kijijini,

Kila kitu kilishapangwa tayari na Askofu Majimbi na mwenzake Tito, zikiwemo Nyaraka feki za matokeo ya utafiti wao,

Kwanza mwanzoni Tito alishauri kwenye ripoti yao waonyeshe kuwa hakukua na dalili ya kuwepo kwa urenium, lakini kwa kusema hivyo wangekosa pesa endelevu kwa maana mgodi ungefungwa, ndipo sasa kwa kushauriana wakaamua kuja na ripoti kuwa wamegundua kiasi kidogo Sana katika eneo lile, na kampuni hiyo ipewe muda zaidi wa kuendelea na utafiti kwani wanaweza kupata mafanikio zaidi, na hivyo wangekabidhi kiasi hicho kidogo kwa serikali halafu Tito kwa niaba ya serikali angepokea kiasi hicho na kushukuru,


Wakati huo huo askofu Majimbi nae angejitokeza hadharani kuunga mkono juhudi za serikali katika mgodi huo kwa kutoa million 500 kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye utafiti huo ..


Hii ndio ilikua mipango yao na Mara baada ya Bwana Johnson kupata mpango huo aliwapongeza Sana Akina Majimbi na ndipo sasa akapanga kuja kuitembelea Tanzania...



****************

Meseji zake za Jana hazikua nyinyi Sana kwenye hii laini,
Kama Oscar alivyodhani hata hivyo alizipitia kwa baadhi na baadae akaona meseji alizokuwa akitafuta,
"Njoo Rombo hotel brother"

"Mkishamaliza kula mnibu "tayari"
Muwe makini na Aina ya chakula,"

Oscar alizipitia hizo meseji Kisha akamuambia amfungulie faili lingine aone majibu ya watumaji,

"On my way"

"Sawa Bosi huu Ni uji tu sio chakula"

Zilikua Ni meseji ambazo Oscar alizihifadhi kichwani mwake,

"TAYARI"

Aliona meseji nyingine ambayo ilikua imetumwa na namba Ile Ile kwa tofauti ya dakika 13,

Oscar sasa alitabasamu,.

Alitoa kiasi Cha pesa na kumpa John Kisha akatoka zake kuelekea nyumbani kwake.


****************

Mzee Mnyoka alipata ujumbe kutoka kwa Diwani kuhusu kuandaa mazingira pale kijijini kwa ajili ya ujio wa Mheshimiwa waziri,

Katika barua yake hiyo kwa mzee Mnyoka, Diwani alisisitiza usafi kwenye kila kitongoji pamoja na usafi pembezoni mwa barabara,

Mzee Mnyoka sasa alikua huru, hata kesi yake iliyokua imemuandama hakujua ilipoishia,

Baada ya kufunga ofisi alitamani kwenda kumuona padri John,

Aliamini Safari hii Padri angekuwa mkweli, Ni wakati anafika ndipo macho yake yakagongana na mtu mmoja hivi ambaye Mzee Mnyoka alihisi kumfahamu, walinyoosheana mikono tu Kisha Mzee Mnyoka akaingia ndani kwa Padri John

Ndipo sasa Mzee Mnyoka akakumbuka sura ya yule mtu,

Ndio, hakuwa anamfananisha hata kidogo,.lakini je pale alikua amefuata nini?
 
KESI YA MZEE MNYOKA 34

Maandalizi yalikua yanaendelea kwa Kasi kubwa,

Kama ilivyokua kijijini taarifa zilikua zinageuzwa Mara kwa Mara wapo waliokuwa wanasema anakuja Raisi, wengine walisema Waziri Mkuu,


Na wengine walisema atakuja Raisi pamoja Makamu wake,

Ili mradi tu kila mmoja alihakikisha anaweka mazingira yake sawa,


Viongozi wa kata walianza sasa kuitembelea Kinjeki Mara kwa Mara na sasa ulinzi uliimarishwa pale Kinjeki mgodini.

***********

Baada ya siku tatu

Oscar alikuwa nyumbani kwa Tito Ni Rasmi serikali ilitangaza ujio wa Bwana Johnson, ambaye angefika nchini baada ya wiki moja,

Serikali kupitia wizara ya nishati hususani Bwana Tito,

Walikua bize kuinadi kampuni ya ureFact ,

"Ujio wa Bwana Johnson, mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ureFact utakuwa Ni chachu ya mafanikio makubwa zaidi kuwahi kutokea nchini kwa miongo kadhaa sasa, tunategemea kupata Majibu kuhusu utafiti mkubwa uliofanywa na serikali kupitia ufadhili wa asilimia 100 wa kampuni hii"

Ilikuwa Ni habari iliyokuwa inaendelea kwenye televisheni kubwa pale sebuleni kwa Tito,


Oscar alitabasamu moyoni huku akiwa na hamu ya kumaliza kazi hii mapema mno,

Baada ya dakika chache alikuja Tito na kuanza maongezi,

"Oscar Kama ujuavyo tuna mgeni muhimu Sana wiki ijayo, niseme wazi mpaka sasa nimekuamini hivyo, kipekee mbali na kwamba mgeni huyo Ni wa kiserikali lakini ujue mgeni huyo anakuja kwa ajili yangu Mimi, na Kuna Nyakati nyingine nitajitahidi ulinzi wako Binafsi juu yake, kikubwa aje salama na aondoke salama,"


Tito alianza hotuba yake,

"Kama unakumbuka nilikuambia siku ile kuwa, usione watu wamekalia hizi nafasi, Kuna Siri nyingi mno, na hivyo Basi lazima uelewe kuwa hata Mimi Kuna mambo mengi ambayo wakati mwingine Sina namna Ila inabidi niyafanye,

Kwahiyo naamini hutaniangusha,

Hebu kwasasa tufanye Hili zoezi nataka nikuambie Oscar, ukifanikiwa kufanya vizuri na Mr Johnson akarudi salama uingereza, Kuna zawadi kubwa ipo kwa ajili yako"


Wewe nenda kajiandae na chukua mizigo yako muhimu uhamie Rasmi hapa nyumbani mpaka tumalize Hili ,zoezi,

"

Alisema Tito huku akimruhusu Oscar kuondoka,


*************

Gongo la mboto -Majohe- saa 2 usiku


Kikao kizito kilikua kinaendelea Kati ya Bwana Allan pamoja na jopo lake, mkakati mzito wa kumtia mikononi Tito pamoja na genge lake Sasa ulikua unaendelea

"Yeah Ila suala la Msingi Ni kuwatia mbaroni wakiwa pamoja"

Alisema mjumbe wa kikao,

"Ndio lakini, yanaweza kutokea mapigano,
Nishauri tuwe na kikosi kingine mapema, huku wengine wakizingira nyumbani kwa Tito kuhakikisha mzigo hautolewi au kuharibiwa"


Waliendelea na majadiliano mpaka usiku wa manane, Kisha walitoka kwenye Ile nyumba na kumuacha Bwana Allan Peke yake,

Kama walivyokuwa wengine na yeye pia alikua na mawazo tele juu ya zoezi hili


******************

Maandalizi yote yamekamilika , sasa Oscar anataka kuhamia Rasmi kwa Tito ili kumpokea mgeni, Bwana Johnson

Sasa Endelea


Saa 2: 17 usiku,

Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere


Waziri Tito akiwa na Oscar pamoja na viongozi wengine wa serikali walikua tayari kabisa kupokea ugeni huo uliokadiriwa kuwa na takribani watu ishirini,

Bwana Johnson alitarajiwa kuwasili nchini muda mfupi ujao, na kutokana na taarifa kutoka serikalini ilisema kwamba, Bwana Johnson atafanya ziara sehemu mbali mbali za kitalii Kama Serengeti, na Kisha ataenda Zanzibar,


Halafu Bwana Johnson angemalizia ziara yake kwa kutembelea mgodi wa Kinjeki, ambako angekaa kwa siku moja halafu kesho yake angerudi uingereza!


Waziri Tito aliangalia saa yake kila Mara huku mapigo yake ya moyo yakienda Kasi, bila kuelewa alijikuta anapata hofu,

Hofu ambayo hata yeye mwenyewe hakujua ilitoka wapi,

Naaam

Hatimaye ndege kubwa Aina ya Airbus ya shirika la ndege la Qatar airways,
Ilitua na sasa Tito alitabasamu huku akisogea eneo maalum la kupokea wageni muhimu

Pamoja na kuwasiliana na Mr Johnson kwa kipindi chote, hakuwahi kuonana nae Ana kwa Ana,
Alijisikia fahari Sana kukutana na tajiri mkubwa duniani,

Alijiweka vizuri sasa koti lake, huku akisogea kupeana mikono na Bwana Johnson,


Mr Johnson, alikua na walinzi Binafsi wanne ambao wote walikua na vifaa vyao mawasiliano na kwa kuwatazama tu walionyesha Ni watu wakakamavu kweli,


Oscar alianza kuhisi ugumu katika zoezi lenyewe,

Kwanza walinzi wenyewe hawakusalimiana na watu, walikua bize tu kupepesa macho huko na huko,

***************
Bwana Allan alikua anafuatilia kila kitu pale uwanjani ,

Tofauti na wengine yeye alikua akimfuatilia Tito,

Kuna wakati alijaribu hata kuwaza kile anachowaza Tito,

Alijua kupitia Tito Milango yote itafunguka, na kila kitu kingejulikana,


Ni wakati anaangalia huko na huko alimuona Oscar akiwa karibu na Tito,

Sasa alifunika komputa yake Kisha akatabasamu,


Alitoka mle ofisini mwake Kisha akaingia kwenye ofisi yake ya Kanisa kwa ajili ya mkesha wa mwisho wa mwezi Kama ilivyo kawaida ya Kanisa lake la winners chapel Hill,


*************

Mgodini Kinjeki maandalizi yote yalikua yamekamilika,

Kazi kubwa ilikua Ni kufunga mizigo kwenye katoni mbali mbali, kuyapanga kwa ajili ya usafirishaji,

Timu maalumu kutoka uingereza, ilikua ndani ya maabara kuhakikisha mzigo unafungwa vizuri na hakuna athari zozote zinazoweza kujitokeza,..
 
KESI YA MZEE MNYOKA 35

Bwana Johnson aliandaliwa Gari maalum ambalo angepanda pamoja na Tito na walinzi wake wawili, huku Gari nyingine ikiwa na walinzi waliobaki pamoja na Oscar
Na Kisha wageni wengine walifuata kwenye magari mengine, kwa hivyo ilitengeneza msururu mdogo hivi uliokua na magari Kama nane ,


Kutoka uwanja wa Ndege , msururu ulinyoosha Kati Kati ya mji ambapo kulikua na hotel ya Twiga ambapo ndipo Mr Johnson pamoja na watu wake walikua wametafutiwa

Oscar alitulia nyuma kabisa akiwa na walinzi Hawa kadhaa ambao wote hawakujishughulisha nae kila mmoja alikua na hamsini zake, Kuna wakati Gari ilipunguza mwendo kidogo au kusimama kidogo Basi wale walinzi wangehamaki na kuweka silaha zao, kwa hivi wakati mwingine Oscar alitamani kucheka,

Lakini yeye alifahamu kuwa kanuni ya kwanza ya Mambo ya ulinzi Ni kutilia Shaka kila kitu,

Waliendelea na Safari na kufika Hoteli ya Twiga salama.

Tito alimsindikiza mgeni wake mpaka kwenye chumba chake Kisha akarudi nyumbani kwake kupumzika.


************

Bwana Bill nae alikua anapanga mipango yake, akili yake ilimuambia kuwa baada ya kazi hiyo nzito Kwisha anaweza akasahaulika, lakini si kusahaulika tu Bali hata kupotezwa kabisa,

Na hivyo alihakikisha kazi hii anaifanya kwa uwezo mkubwa, asingeweza kutoa jasho lake kwa miaka yote Ile halafu faida wapate wengine,

Sasa mkakati wake uliiva kichwani mwake,

Bwana Bill au Kama walivyokuwa wanamuita "Carlos" wakaimfananisha na jambazi hatari na mlanguzi wa madawa ya kulevya,

Unaweza kusema tofauti yao ilikua rangi tu!

Lakini akili zao zilikua karibu kabisa kufanana,


Mkakati wake aliokua ameundaa aliamini lazima utaawacha mabosi zake Hawa mikono kichwani,

Sasa alikumbuka zoezi ambalo aliambiwa alifanye wiki moja iliyopita alipokutana na Tito,

Zoezi lenyewe ilikuwa kuandaa magari mawili yanayofanana kwa ajili ya kuondoka na mzigo nyumbani kwa Tito kupeleka uwanja wa Ndege,

Ndipo sasa yeye akandaa Magari matatu, huku moja akilificha mahali anapojua yeye,

Kisha magari mawili akayaleta mpaka mgodini Kinjeki kusubiri siku ya tukio,


Tayari mabox ambayo yalitakiwa kupeleka mzigo mpaka nyumbani kwa Tito yalishaandaliwa,

Mzigo huu ulitakiwa kuondoka na Bwana Bill siku chache zijazo mpaka nyumbani kwa Tito ambapo angeunganisha na mizigo mingine Kisha kupakia kwenye ndege,

Kwanza kabisa Bwana Johnson alifanya mazungumzo Rasmi na waziri wa nishati Bwana Tito,

Maongezi haya yalikua mubashara kabisa kupitia vyombo vya habari na Tito alisema kwa niaba ya serikali kuwa baada ya Bwana Johnson kumaliza ziara yake wataalamu wake watatoa taarifa Rasmi kuhusu kupatikana kwa urenium ama la,

Waziri Tito alisisitiza kuwa serikali iko bega kwa bega na kampuni hiyo ili kufanikisha mipango yote kwa ajili ya manufaa ya taifa,


"Kwahiyo Kama nilivyosema, mradi huu utakuwa na mafanikio makubwa endapo kiasi urenium kidogo kitagunduliwa, Dunia inabadilika siku hizi tutapata nishati ya uhakika ya umeme, tutapata mapato , tutapata wawekezaji wengi na mambo mengine kwahiyo Mimi niseme watanzania tuwe watu wa kuvuta subra Mambo mengi mazuri yanakuja"


Alimaliza hotuba yake Bwana Tito huku akipeana mikono na Bwana Johnson kwa ajili ya kumaliza kipindi.

***************


Kati Kati ya jiji la Dar es salaam
Oscar alikua na rafiki yake George wakimalizia kupanga mipango yao ,

Walikubaliana George atangulie kijijini akaandae mazingira ili kwamba Oscar akienda na Tito kazi iwe nyepesi,

Alimpa maelezo yote muhimu na watu wa kufanya nao kazi kwa siku zote atakazokuwa pale Kijijini,


"Tumalize hii inshu Kaka na Bila Shaka baada ya hapa sasa naweza kutulia angalau niangalie maisha mengine"

Alisema Oscar

"Kaka hujawahi kusema hivyo kabisa, tumefanya kazi ngumu, lakini daima hujawahi kutamani kupumzika!"
Alisema George


"Unajua nimewaza Sana na sisi Ni Binadamu pia lazima tuishi Kama wengine , we nenda naamini tutamaliza salama"

Alisema Oscar wakati huo alitoa Simu yake baada ya kutingishika kuashiria ujumbe mfupi uliingia,

Aliifungua na ilikua Ni ujumbe kupitia WhatsApp

"Kesho nakuja bongo"

Ujumbe huo ukitoka kwa Joyce,


Sasa kwa Mara ya kwanza Oscar akahisi kukosa amani,

Bila kujielewa akajikuta anaanza kumfikiria Joyce,

Aliwaza sekunde kadhaa Kisha akamjibu,


"Kwanini? Bado hujamaliza hata mwezi?"


"It's an emergency, we will talk"
Alijibu Joyce akimaanisha Ni dharula, wataongea akija,


"Huyu mtoto anakuja kufanya nini?"

Aliwaza Oscar akiingia kwenye Gari lake na kurudi nyumbani kwa Tito.



*******************


Mzee Mnyoka akiwa ofisini kwake , sasa wiki hii alipokea wageni wa kutosha, kuanzia waandishi wa redio, magazeti na hata wageni mbali mbali wa serikali,


Hivyo wakati anaelezwa Kuna mgeni mwingine yupo nyumbani kwake anamsubiri, Mzee Mnyoka hakuwa na haraka ya kurudi nyumbani,

Hata hivyo alishapokea wageni wengi nyumbani na ofisini, na tayari cheo Cha mwenyekiti kilianza kumkaa vizuri,


Mzee Mnyoka alirudi nyumbani kwake na kumkuta mgeni wake,

Tofauti na wageni wote mgeni huyu aliomba sehemu ya kujihifadhi kwa muda wa siku tano,

Yeye alidai alitoka shirika lisilo la kiserikali na alikua anafanya shughuli kwa kujitolea na alikua mafunzoni na kazi yake ya kwanza ilikuwa Ni kuripoti matukio hayo ya ziara ya Bwana Johnson na hivyo anaomba msaada wa Kijiji kwa mwenyekiti,

Mzee Mnyoka alitoka kuongea na mkewe Kisha wakakubaliana wampe chumba Cha James kwani hata hivyo siku tano zisingekuwa nyingi.....
 
KESI YA MZEE MNYOKA 35

Bwana Johnson aliandaliwa Gari maalum ambalo angepanda pamoja na Tito na walinzi wake wawili, huku Gari nyingine ikiwa na walinzi waliobaki pamoja na Oscar
Na Kisha wageni wengine walifuata kwenye magari mengine, kwa hivyo ilitengeneza msururu mdogo hivi uliokua na magari Kama nane ,


Kutoka uwanja wa Ndege , msururu ulinyoosha Kati Kati ya mji ambapo kulikua na hotel ya Twiga ambapo ndipo Mr Johnson pamoja na watu wake walikua wametafutiwa

Oscar alitulia nyuma kabisa akiwa na walinzi Hawa kadhaa ambao wote hawakujishughulisha nae kila mmoja alikua na hamsini zake, Kuna wakati Gari ilipunguza mwendo kidogo au kusimama kidogo Basi wale walinzi wangehamaki na kuweka silaha zao, kwa hivi wakati mwingine Oscar alitamani kucheka,

Lakini yeye alifahamu kuwa kanuni ya kwanza ya Mambo ya ulinzi Ni kutilia Shaka kila kitu,

Waliendelea na Safari na kufika Hoteli ya Twiga salama.

Tito alimsindikiza mgeni wake mpaka kwenye chumba chake Kisha akarudi nyumbani kwake kupumzika.


************

Bwana Bill nae alikua anapanga mipango yake, akili yake ilimuambia kuwa baada ya kazi hiyo nzito Kwisha anaweza akasahaulika, lakini si kusahaulika tu Bali hata kupotezwa kabisa,

Na hivyo alihakikisha kazi hii anaifanya kwa uwezo mkubwa, asingeweza kutoa jasho lake kwa miaka yote Ile halafu faida wapate wengine,

Sasa mkakati wake uliiva kichwani mwake,

Bwana Bill au Kama walivyokuwa wanamuita "Carlos" wakaimfananisha na jambazi hatari na mlanguzi wa madawa ya kulevya,

Unaweza kusema tofauti yao ilikua rangi tu!

Lakini akili zao zilikua karibu kabisa kufanana,


Mkakati wake aliokua ameundaa aliamini lazima utaawacha mabosi zake Hawa mikono kichwani,

Sasa alikumbuka zoezi ambalo aliambiwa alifanye wiki moja iliyopita alipokutana na Tito,

Zoezi lenyewe ilikuwa kuandaa magari mawili yanayofanana kwa ajili ya kuondoka na mzigo nyumbani kwa Tito kupeleka uwanja wa Ndege,

Ndipo sasa yeye akandaa Magari matatu, huku moja akilificha mahali anapojua yeye,

Kisha magari mawili akayaleta mpaka mgodini Kinjeki kusubiri siku ya tukio,


Tayari mabox ambayo yalitakiwa kupeleka mzigo mpaka nyumbani kwa Tito yalishaandaliwa,

Mzigo huu ulitakiwa kuondoka na Bwana Bill siku chache zijazo mpaka nyumbani kwa Tito ambapo angeunganisha na mizigo mingine Kisha kupakia kwenye ndege,

Kwanza kabisa Bwana Johnson alifanya mazungumzo Rasmi na waziri wa nishati Bwana Tito,

Maongezi haya yalikua mubashara kabisa kupitia vyombo vya habari na Tito alisema kwa niaba ya serikali kuwa baada ya Bwana Johnson kumaliza ziara yake wataalamu wake watatoa taarifa Rasmi kuhusu kupatikana kwa urenium ama la,

Waziri Tito alisisitiza kuwa serikali iko bega kwa bega na kampuni hiyo ili kufanikisha mipango yote kwa ajili ya manufaa ya taifa,


"Kwahiyo Kama nilivyosema, mradi huu utakuwa na mafanikio makubwa endapo kiasi urenium kidogo kitagunduliwa, Dunia inabadilika siku hizi tutapata nishati ya uhakika ya umeme, tutapata mapato , tutapata wawekezaji wengi na mambo mengine kwahiyo Mimi niseme watanzania tuwe watu wa kuvuta subra Mambo mengi mazuri yanakuja"


Alimaliza hotuba yake Bwana Tito huku akipeana mikono na Bwana Johnson kwa ajili ya kumaliza kipindi.

***************


Kati Kati ya jiji la Dar es salaam
Oscar alikua na rafiki yake George wakimalizia kupanga mipango yao ,

Walikubaliana George atangulie kijijini akaandae mazingira ili kwamba Oscar akienda na Tito kazi iwe nyepesi,

Alimpa maelezo yote muhimu na watu wa kufanya nao kazi kwa siku zote atakazokuwa pale Kijijini,


"Tumalize hii inshu Kaka na Bila Shaka baada ya hapa sasa naweza kutulia angalau niangalie maisha mengine"

Alisema Oscar

"Kaka hujawahi kusema hivyo kabisa, tumefanya kazi ngumu, lakini daima hujawahi kutamani kupumzika!"
Alisema George


"Unajua nimewaza Sana na sisi Ni Binadamu pia lazima tuishi Kama wengine , we nenda naamini tutamaliza salama"

Alisema Oscar wakati huo alitoa Simu yake baada ya kutingishika kuashiria ujumbe mfupi uliingia,

Aliifungua na ilikua Ni ujumbe kupitia WhatsApp

"Kesho nakuja bongo"

Ujumbe huo ukitoka kwa Joyce,


Sasa kwa Mara ya kwanza Oscar akahisi kukosa amani,

Bila kujielewa akajikuta anaanza kumfikiria Joyce,

Aliwaza sekunde kadhaa Kisha akamjibu,


"Kwanini? Bado hujamaliza hata mwezi?"


"It's an emergency, we will talk"
Alijibu Joyce akimaanisha Ni dharula, wataongea akija,


"Huyu mtoto anakuja kufanya nini?"

Aliwaza Oscar akiingia kwenye Gari lake na kurudi nyumbani kwa Tito.



*******************


Mzee Mnyoka akiwa ofisini kwake , sasa wiki hii alipokea wageni wa kutosha, kuanzia waandishi wa redio, magazeti na hata wageni mbali mbali wa serikali,


Hivyo wakati anaelezwa Kuna mgeni mwingine yupo nyumbani kwake anamsubiri, Mzee Mnyoka hakuwa na haraka ya kurudi nyumbani,

Hata hivyo alishapokea wageni wengi nyumbani na ofisini, na tayari cheo Cha mwenyekiti kilianza kumkaa vizuri,


Mzee Mnyoka alirudi nyumbani kwake na kumkuta mgeni wake,

Tofauti na wageni wote mgeni huyu aliomba sehemu ya kujihifadhi kwa muda wa siku tano,

Yeye alidai alitoka shirika lisilo la kiserikali na alikua anafanya shughuli kwa kujitolea na alikua mafunzoni na kazi yake ya kwanza ilikuwa Ni kuripoti matukio hayo ya ziara ya Bwana Johnson na hivyo anaomba msaada wa Kijiji kwa mwenyekiti,

Mzee Mnyoka alitoka kuongea na mkewe Kisha wakakubaliana wampe chumba Cha James kwani hata hivyo siku tano zisingekuwa nyingi.....
Hongera kwa uandishi mzuri mkuu, naenjoy[emoji126][emoji126][emoji126]
 
Back
Top Bottom